ONDOLEO LA DHAMBI (MSAMAHA WA DHAMBI)

Na Godfrey Miyonjo.

“Maana ujapojiosha kwamagadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu asema Bwana MUNGU” YEREMIA 2:22.
BWANA YESU asifiwe,
Duniani kuna dhana nyingi sana juu ya ondoleo la dhambi (msamahawadhambi),
Wapo wanaoamini kuwa kwa kunawa maji uovu unaondoka ndani yao,
Wengine huamini kuwa kwa kutimiza maagizo flaniflani waliyopewa na viongozi wao wa dini kama vile kusalisa la ya baba yetu mara kadhaa, kusali sala ya ninasadiki, au kufanya usafi ndani au nje ya kanisa kuna weza kuwasaidia kupata ondoleo la dhambi,
Wengi pasipo kujua kuwa kumbukumbu ya matendo ya wanadamu zipo mbele za MUNGU, waohufanya mambo ya kidunia tu na kujiridhisha kuwa wamesamehewa dhambizao,

MUNGU ANASEMA
“Maana ujapojiosha kwa magadi, na kujipatia sabuni nyingi, lakini uovu wako umeandikwa mbele zangu asema Bwana MUNGU” YEREMIA 2:22.
Anayasema hayo akimaanisha kuwa uovu wa mtu hauondolewi kwa maji,
Wala kwa sabuni,
Wala kwa magadi,
Wala kwa kufanya usafi ndani ya kanisa,
Wala nje ya kanisa,
Wala kwa kusali baba yetu,
Wala kwa ninasadiki,
Wala kwa atukuzwe,
Wala kwa salamu Maria,
Bali ni kwa kutubu uovu wetu mbeleza MUNGU na kumaanisha kuachaa.
KWA MAANA IMEANDIKWA
“Mimi, naam, mimi ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili ya ngumwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako” ISAYA 43:25.
Ninaomba ifahamike kuwa, ni Mungu pekee kupitia Kristo Yesu ndiye anayesamehe dhambi, tena huwasamehe wanaotubu na kunyenyekea kwake.

Na ndiyo maana Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
MLINUNULIWA KWA THAMANI; MSIWE WATUMWA WA WANADAMU.
………… TUBU LEO……..
Ni mimi ndugu yenu katika Kristo,
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu)
WhatsApp 0757649495.

Comments