KULIENDEA JESHI

UFUFUO NA UZIMA MOROGORO

 

Na:  STEVEN NAMPUNJU (AP)
& DR. GODSON ISSA ZACHARIA (SNP)
Utangulizi: Daudi na jeshi lake walilia sana baada ya kukutana na changamoto nyumbani kwao, badala ya kusherekea ushindi walioupata hapo kabla, badala yake wakakutana na familia zao zimetekwa na maadui wao na kupelekewa wasikokujua. Hata hivyo, pamoja na maombolezo kuwa makubwa na shutuma nyingi kuelekezwa kwa Daudi, ilimbidi Daudi amuulize Bwana kama yafaa kulifuatilia jeshi au la!!?  Walipata ruhusa kutoka kwa Bwana, waliliendea jeshi la maadui, wakawakuta wakiwa wamejisahau, wamechoka na huku  wakisherehekea nyara na mateka wao.
Imeandikwa katika 1SAMWEL 30:1-20…[Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Siklagi siku ya tatu, hao Waamaleki walikuwa wameshambulia Negebu, na Siklagi, nao wameupiga Siklagi, na kuuchoma moto; 2 nao wamewachukua mateka wanawake waliokuwamo wakubwa kwa wadogo; hawakuwaua wo wote, ila wakawachukua, wakaenda zao. 3 Basi Daudi na watu wake walipoufikilia mji, tazama, ulikuwa umechomwa moto; na wake zao, na watoto wao, waume kwa wake, wamechukuliwa mateka. 4 Ndipo Daudi na watu waliokuwa pamoja naye wakainua sauti zao na kulia, hata walipokuwa hawana nguvu za kulia tena. 5 Na hao wake wawili wa Daudi walikuwa wamechukuliwa mateka, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, aliyekuwa mkewe Nabali, wa Karmeli. 6 Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana nafsi za hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. 7 Kisha Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, Tafadhali niletee hapa hiyo naivera. Naye Abiathari akamletea Daudi naivera huko. 8 Daudi akauliza kwa Bwana, akasema, Je! Nikiwafuata jeshi hili, nitawapata? Naye akamjibu, Fuata; kwa kuwa hakika utawapata, nawe hukosi utawapokonya wote. 9 Basi Daudi akaenda, yeye na wale watu mia sita waliokuwa pamoja naye, nao wakakifikilia kijito Besori, ambapo wale walioachwa nyuma walikaa. 10 Lakini Daudi akakaza kufuata, yeye na watu mia nne; kwa maana watu mia mbili walikaa nyuma, ambao walitaka kuzimia hata hawakuweza kukivuka hicho kijito Besori. 11 Nao wakamkuta Mmisri mavueni, wakamleta kwa Daudi, na kumpa chakula, naye akala; nao wakampa maji ya kunywa; 12 kisha wakampa kipande cha mkate wa tini, na vishada viwili vya zabibu; naye akiisha kula roho yake ikamrudia; kwa maana alikuwa hakula chakula wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku. 13 Ndipo Daudi akamwuliza, Wewe u mtu wa nani; nawe umetoka wapi? Naye akasema, Mimi ni kijana wa Misri, mtumwa wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu tangu siku hizi tatu nalishikwa na ugonjwa. 14 Sisi tulishambulia Negebu ya Wakerethi, na ya milki ya Yuda, na Negebu ya Kalebu; na huo mji wa Siklagi tukauchoma moto. 15 Daudi akamwambia, Je! Wewe utaniongoza chini hata nilifikilie jeshi hilo? Naye akasema, Uniapie kwa Mungu, ya kwamba hutaniua, wala kunitia mikononi mwa huyo bwana wangu, nami nitakuongoza chini hata kulifikilia jeshi hilo. 16 Na hapo alipokuwa amewaongoza chini, tazama, hao walikuwa wametawanyika juu ya nchi yote, wakila na kunywa, na kufanya karamu, kwa sababu ya hizo nyara kubwa walizochukua katika nchi ya Wafilisti, na katika nchi ya Yuda. 17 Naye Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia. 18 Daudi akawapokonya wote waliokuwa wamechukuliwa na Waamaleki; naye Daudi akawaokoa wakeze wawili. 19 Wala hawakupotewa na kitu, mdogo wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala cho chote walichojitwalia hao; Daudi akavirudisha vyote. 20 Naye Daudi akatwaa makundi yote ya kondoo na ng'ombe, ambao waliwatanguliza mbele ya wanyama wale wengine, wakasema, Hao ndio nyara za Daudi.]…..Tunajifunza kuwa usipochoka utakutana na adui yako akiwa ametelekezwa na Bwana wake, na utakapomsaidia atakupa siri zote za upande wa pili. Kwa nini kuna haja ya kulifuatia jeshi? Mungu wetu ni Bwana wa Majeshi,  na hivyo hufuatilia kwa wakati wake ili  kufanya  jambo fulani.
KWA NINI TULIENDEE JESHI?
Sababu ya kwanza: Wapo  waliofungwa, wamekamatwa na walipaswa wafikie hatima fulani  ila  wamekwisha kutekwa. Tunapolifuata jeshi tunakomboa vilivyo vyetu kwa  Jina la Yesu.  Kama ilivyoandikaw katika ISAYA 42:22…[Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo,  wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.]… Mungu anataka  kupitia sisi leo tufuatilie hizo kambi za adui na kurudisha vile vyetu walivyopora.

ISAYA 14:17..[Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?]…Mungu  anataka akutoe katika hayo mateso ili uingie katika utele wako. Shetani  ni bwana jela asiyeruhusu watu waende kwenye hatima zao.

Unapo kwako ila adui zako wamekufanya usipaone. Siyo  kwenye hali  uliyo nayo ndiyo Mungu amekuandikia. Hapana. Adui amekuwekea na walinzi wakulinde  ili kuhakikisha  ‘mtu huyu haponi, mtu huyu haoelewi/haoi, mtu huyu hamiliki nyumba’ n.k. Adui anao uwezo wa kuona hatima yako hata kabla ya wewe kuiona. Tazama jinsi ambvyo mamajusi walisafiri muda mrefu  kuja Yerusalem kwa ajili  ya kumuona mfalme atakayezaliwa (Yesu Kristo). Ina maana kuwa, kitendo cha wao kusafri muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, walikuwa na uwezo wa kuona mambo ambayo hata mama wa Yesu asingeweza kuyaona kipindi  kile.
Adui anao uwezo wa kuona hatima yako hata kabla ya wewe kuiona. Tazama jinsi ambvyo mamajusi walisafiri muda mrefu  kuja Yerusalemkwa ajili  ya kumuona mfalme atakayezaliwa (Yesu Kristo). Ina maana kuwa, kitendo cha wao kusafri muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwa Yesu, na kufika  Yerusalem bila kutumia usafiri  wa kawaida (bila ndege),ni chamaadalizi ya muda mrefu sana.

UKIRI
Yeyote aliyekamata hatima nyota,leo achia kwa Jina la Yesu. Naziapisha mamlaka  zote za kuzimu, kwenye ulimwengu wa roho, yeyeote aliyekamata baraka zangu,leo aniachie kwa Jina la Yesu.
Yeyote aliyekamata hatima yako, nyota yako, leo achia kwa Jina la Yesu. Naziapisha mamlaka  zote za kuzimu, kwenye ulimwengu wa roho, yeyeote aliyekamata baraka zangu,leo aniachie kwa Jina la Yesu. Amen

Taabu uliyo nayo  siyo kwa Mungu aliipanga ajili yako. Mtu  mwingine unatamani  kula aina fulani za chakula lakini unashindwa kwa sababu shetani amekuwekea vidonda vya tumbo na kukuzuia usile unachotamani kula.
UKIRI
Namkataa mgombea wa kiroho, ambaye amenishawishi ili  anitawale kwa Jina la Yesu. Kuanzia leo na kuanzia sasa,kila mtenda kazi wa ibilisi uliyetwaa nyuara nakunyang’anya, achia kwa Jina la Yesu. Amen.

Sababu ya pili:Wapo adui zetu walioteka mali zetu

Inabidi tutoke tuzifuate nyara zetu mahali zilipo kwa Jina la Yesu. imeandikwa,  “Taabu ya mkono wako  hakika utaila”. Haifai kutaabikia
2WAFALME 7:1-11…[Elisha akasema, Lisikieni neno la Bwana; Bwana asema hivi, Kesho panapo saa hii, kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, langoni pa Samaria. 2 Basi yule akida, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama Bwana angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula. 3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe? 4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu. 5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha Washami, kumbe! Hapana mtu. 6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi. 7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi zao, na punda zao, na kimo chao vile vile kama kilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao. 8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha. 9 Ndipo wakaambiana, Mambo haya tufanyayo si mema; leo ni siku ya habari njema, na sisi tunanyamaza; mkingoja hata kutakapopambazuka, madhara yatatupata; basi twende tukawaambie watu wa nyumba ya mfalme. 10 Basi wakaenda, wakawaita mabawabu wa mji; wakawaambia, Tulifika kituo cha Washami, na tazama, hapana mtu ye yote huko, wala sauti ya mtu, ila farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na hema zao kama walivyoziacha. 11 Na mabawabu wakaita wakawaambia watu wa nyumba ya mfalme.]… Wakoma wanne hawa walikuwa wametengwa kwa sababu haikutakiwa wachangamane na jamii nzima. Wakoma katika huu mji  walikuwepo wengi sana, lakini  ni hawa wanne tu walipata ujasiri na kuchukua hatua ya kulifuatilia jeshi, huku wakihatarisha maisha yao. Sababu kubwa ya wakoma kulifuatia jeshi ilikuwa NJAA.
Adui ana mtaji wako. Ni afadhali kumfuataia adui yako kuliko rafiki  yako  kwa sababu adui yako ndiye mwenye mali zako, baraka zako na kila kitu chako. Ukikataliwa na watu usife moyo. Ukimwamini Bwana yote yanawezekana.

Wakoma wanne walikataliwa na jamii yao, lakini  hatimaye wao ndio waliosababisha wale waliowatenga wapate ukombozi, chakula na utajiri wote.  Chochote unachokitafuta, utakipata kwa adui zako wala siyo rafiki zako. Tatizo la Wakristo wengi leo hii ni kuwa, hawataki kufuatia jeshi la adui zao. Wewe unayetafuta ajira kwa muda mrefu, ingia kwenye maombi na kuliendea jeshi la Washami kuwalazimisha waachie nyara zako  kwa Jina la Yesu.
Kuna wakati ule ambapo chakula kilikuwa ngumu sana kukipata, ikafikia wakati ambapo wamama  walikubaliana wale watoto wao wa kuzaa kwa zamu, na wakafanya hivyo‼! Je, iweje leo hii ukose ajira kwa kipindi kifupi  tu na ukubali kuutoa mwili  wako kama rushwa ili  upate ajira!!?
Mji  ule wa Siklagi  ulivyovamiwa, mji wote ulichomwa kwa moto. Silaha zipo nyingi ambazo adui hupenda kuzitumia. Wengine leo hii hutumia hirizi kama silaha / zana ya kukuteka au kuiteka familia yako.
Ibilisi hutaka kuchoma moto vitu/taaluma/vipawa vyako, vilivyokufanya uwe mahali fulani. Mathalani, kwa kuwa ibilisi anajua akikuachia hiyo nyara (kipawa) utafanikiwa hupenda kuondoka nayo.  Mfano,  mama yake Yusufu alikuwa hapati watoto, lakini baada ya kumzaaYusufu, unaona kuwa Yusufu ndiye aliyekuja kusababisha wokovu kwa ndugu zake na wazazi wake pia.
Mpende adui yako. Kumbuka kuwa unapompenda aduia yako, utakaa karibu naye na kukuwia rahisi kuichukua amani  yako, mali  zako,  baraka zako ambazo alikuwa amezibeba. Unachopaswa kubeba ni JINA LA YESU. Ipo nguvu katika hili  jina. Kumbuka kuwa,  wakati wa Matendo yaMitume, wanafunzi wa Yesu walikatazwa wasilitumie Jina la Yesu  kuhubiri, kwa sababu lina nguvu mno!!.

UKIRI
Ewe jeshi uliyeweka kambi ofisini kwangu, achia kwa Jina la Yesu. Ewe jeshi uliyeweka kambi kwa watoto wangu, achia kwa Jina la Yesu. Mahali popote nilipokamatwa ili nisiende kwangu, na jambo lolote lilinikamata nalikataaa leo kwa Jina la Yesu. Kuanzia leo natoka kwenye ngome yako, natoka kwenye dhiki yako, Kwa Jina la Yesu. Ninaamuru utawala wa Yesu uwe dhahiri, kwa nguvu ya Damu ya Yesu ya kuteka nyara iwe dhahiri  kwa Jina la Yesu. Amen

FAIDA ZA KULIENDEA JESHI.

1.      Utarejesha mateka. Mtu aliendeae jeshi atarejesha mateka. Kuna watu waliokufa katika mazingira tata, leo hii ukiliendea jeshi utawaona tena kwa Jina la Yesu.
2.      Utaongeza hazina yako: Hayupo aliyeliendea jeshi akarudi tupu.  Daudi alipoliendea jeshi, alipata nyara za adui zake.  Ukimpiga adui unapata vyombo vya adui  zako. Hata hivyo, unapaswa kujiweka tayari kama ambavyo Dauidi alivaa naivera na kumuuliza Bwana  kuhusu kuliendea jeshi. Muongoza vita yetu  leo ni Bwana Yesu, na hivyo inabidi umkubali kwanza ili upate kibali cha kuliendea jeshi na kulishinda kwa Jina la Yesu, hadi tufikie pale ambapo adui zako wanafanya sherehe zao.
Endapo wewe hujamuamini Yesu Kristo, ni vyema ukafanya maamuzi ya kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana   na  Mwokozi wa maisha yako leo.

Comments