MAOMBI YA KUWATEKETEZA WAKUU WA GIZA.

Na Mtumishi Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Katika maombi ya mkesha jana nilipata ufunuo ambao uliniamsha katika maombi. Ufunuo huo ulisema ''OMBA UKIHARIBU WAKUU WA GIZA''
Ghafla nilichangamka katika maombi hayo na kuanza kuomba nikiwatoboa macho yao yote wakuu wote wa giza wanaofuatilia huduma yangu, wakuu wa giza wote wanaofuatilia afya yangu, wakuu wa giza wote wanaofuatilia familia na ukoo wangu, wakuu wa giza wote wanaofuatilia uchumi wangu, na hakika nilichangamka katika kuwashambulia wakuu wote wa giza.

Waefeso 6:12 ''Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.''

Ni muhimu sana kujua siri hii ya maombi inayotokana na neno la MUNGU.
Wakuu wa giza ni wale ambao hutuma nguvu za giza.
Mara nyingi tumekuwa tukipambana na nguvu za giza zilizotumwa na wakuu wa giza na kuwaacha salama wakuu wa giza.
Unaweza ukapambana na jini aliyetumwa kwako lakini ukasahau kumwangamiza aliyemtuma jini huyo, aliyemtuma jini huyo anaitwa mkuu wa giza. Anaweza kuwa mwanadamu au anaweza kuwa roho ya kuzimu iliyo na maroho mengine mengi ya kukusumbua. Mfano kama utapambana na jini aliyetumwa kwako ili kukuharibia ndoa na kwa maombi yako hakika ukamwangamiza huyo jini lakini baada ya muda anatumwa jini mwingine. unaweza kwa mwaka mzima ukawa unapambana na majini na hayaishi hata kama unayashinda kila siku, lakini ukimponda anayetuma majini hayo ndio mwisho wa vita yako. Pambana leo ili ushinde.

Ni ufunuo mpana sana na hakika jana nilishangaa sana.
Kama mchawi ndiye anayekusumbua  kwa kukutumia mapepo na wewe kila siku unapambana na mapepo  lakini anayeyatuma mapepo hayo kwako yuko salama maana hujamgusa. Anayetuma nguvu za giza kwako huyo ndio mkuu wa giza, pambana na huyo ndipo utashinda katika hiyo vita yako, kama utakuwa unapambana na waliotumwa tu basi wewe utaendelea na vita siku zote maana anayetuma nguvu hizo za giza anazo nyingi hivyo wewe utazipunguza tu na sio kuzimaliza, lakini ukipambana na anayetuma nguvu za giza hakika umeshinda na vita itakoma. Ndio maana Biblia inatushauri kupambana na wakuu wa pepo wabaya na kupambana na wakuu wa giza. ukimwangamiza mkuu wa giza hakika umeshinda maana anaowatuma hata hawatakuja maana kama mkuu wao umemuweza basi wao wataogopa na utaendelea kuwa mshindi daima.
BWANA YESU anasema ''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya MWANA. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. Yohana 14:13-14 ''
Kwa sababu jina la YESU KRISTO lipo leo na sisi waombaji tupo leo basi twende tukaombe. Anza na kutubu na kuokoka kama bado hujaokoka, kisha omba kwa imani katika jina la YESU KRISTO.

Maombi haya ni muhimu sana lakini pia maombi haya ni dira kwako ambaye ni mwombaji mchanga ili kukufundisha ili wewe ukaombe zaidi ya haya katika hitaji lako mwenyewe.

Maombi.

 BABA wa mbinguni pokea sifa milele. Asante BWANA maana fadhili zako ni za milele. Asante kwa kunilinda katika maisha yangu yote. Ninaishi kwa sababu JEHOVHA BWANA umeamuru niishi. nakutukuza mfalme wa Mbinguni kwa neema yako kwangu.
Asante BWANA YESU kwa ufunuo huu wa kunitaka mimi niwaharibu na kuwateketeza wakuu wote wa giza wanaonifuatilia.
Kwa jina la YESU KRISTO ninawafuata wakuu wote wa giza na kuwatoboa macho yao yote na kuanzia sasa hawataniona kamwe maana damu ya YESU inawaharibu sana.
Kila mkuu wa giza anayefuatilia ndoa yangu, ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayemfuatilia mchumba wangu,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayefuatilia afya yangu,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayefuatilia biashara yangu,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayefuatilia wazazi wangu, ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayefuatilia masomo yangu na ufahamu wangu, ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayefuatilia familia yangu na ukoo wangu,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayefuatilia uchumi wangu,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayefuatilia kanisa letu,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anyelrta magonjwa na mikosi,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza anayeleta roho ya kukataliwa,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa kiza anayeleta balaa na majanga kwangu,ninamtoboa macho yake yote kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mkuu wa giza na kazi zake zote naziharibu na kuziangamiza kwa jina la YESU KRISTO.
Asante BWANA YESU maana umenipa ushindi leo.
Ninakutukuza mfalme wa mbinguni maana ushindi wangu umedhihilika leo.
Asante MUNGU uliye hai uliyekuja kunishindia,
Asante BABA wa mbinguni maana umewatuma malaika wako kunisaidia kushinda vita hii.
Ni katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi,.
Amen Amen.

''Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye(MUNGU) ataisikia sauti yangu.-Zanuri 55:17''

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
+255714252292.
mabula1986@gmail.com


Comments