MASAA NANE(8) MBINGUNI



na Ricardo Cid  Bwana akasema, “Ninatuma ujumbe huu kwa watu wangu katika dunia,kwa sababu mimi niko hai katika ulimwengu wa roho.” Ufunuo 4:1 Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. Ufunuo 5:11-12 Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi sana, idadi isiyohesabika, maelfu na maelfu. Walikuwa wamekaa kuzunguka kiti cha enzi, wale viumbe hai wanne na wale wazee; wakasema kwa sauti kuu: “Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, utukufu na sifa.” Tafadhali, kanisa sikilizeni nini kilichotokea katika maisha yangu. Katika ndoto, Bwana alianza kushughulika nami. Nakumbuka katika ndoto hiyo, Nilitembea nje ya nyumba yangu. Nilitembea katika mitaa kwa jirani zangu na mara nilihisi kwamba mtu akiniinua mikono yangu juu angani nami nilikuwa nikitembea mbio juu ya mawingu na nikimtukuza Mungu. Mwangaza mkubwa alikuja juu yangu na sauti ilisema nje ya mwangaza huo, "Ricardo, Ricardo, acha kazi yako kwa sababu nataka kufanya kitu kwa maisha yako na kwa kanisa langu juu ya dunia." Baada ya kusikia maneno haya, mimi nilitetemeka na nikaamka kutoka katika ndoto yangu. Nikainuka na mimi nikaanza kulia kwa Mungu na kuuliza, "ni kitu gani, hiki Bwana?" Sauti hiyo ilikuja kwangu kwa nguvu sana. Ilitokea kwangu kwa siku nyingi. Kisha nikaendelea kulala tena na nikaota ndoto hiyohiyo moja na Bwana alirudia mara kwa mara ujumbe huo kwangu. Baada ya mara kwa mara kurudia, niliamka na kupiga mayowe kwa sababu sauti ya Mungu iliongezeka kwa kiasi kila wakati. Niliamka nikiwa natetemeka, nilipiga kelele na wazazi wangu waliniuliza, "Je, kuna tatizo gani?" Niliwaambia kuhusu ndoto na mama yangu aliniombea na aliniambia, "Kama Bwana anazungumza na wewe, basi Yeye atakupa ufahamu. "Tuliendelea kuomba usiku kutwa mpaka wakati wa mimi kwenda kazini asubuhi. Mama yangu aliniambia nijiandae kwenda kazini. Tulimuomba Bwana 2 ishara ili tujue kama yeye ndiye alizungumza na mimi. Nilioga, nikajiandaa, na nikaenda kazini. Nilikuwa nafanya kazi katika "maabara ya Chile". Mimi kwa kweli napenda kazi yangu. Nilikuwa nikipitiwa katika kituo cha basi na kwenda kazini. Mara niliposhuka, mtu mmoja aliniambia kwa haraka, "Unafanya nini hapa? Hautakiwi kuwa mahali hapa tena. "Katika matukio kadhaa, wengine waliniambia kitu hiko. Jambo la kushangaza ni kwamba wao hawakuwa wamezaliwa mara ya pili. Hii ni ishara ambayo Mungu alinipa. Baada ya ishara hii, niliamua kwenda kwa bosi wangu ili niache kazi. Nikamwambia, "Mimi menipasa kuondoka katika kampuni kwa sababu Mungu ameniagiza kujiondoa." Bwana anapotupa amri, ni LAZIMA kutii. Bosi wangu alikuwa na wasiwasi kwa ajili yangu na aliuliza, "Je,utakwenda kufanya nini? Wapi utapata kazi nyingine nzuri kama hii? "Nilimwambia imenipasa kumtii Mungu. Basi, walinifanyia mahafali makubwa ya kuniaga ya watu elfu mbili kwa ajili yangu. Baada ya hapo, nilikusanya vitu vyangu vyote na kurudi nyumbani. Nilifika nikiwa nalia, mama yangu alikuwa tayari ananisubiri kwa mbele ya nyumba. Nilimwambia kuwa niliamua kuacha kazi yangu kwa sababu Bwana alithibitisha ndoto zangu kupitia watu hao. Yeye akajibu, "Kama Bwana amekuambia, basi namuomba afanye katika maisha yako vile apendavyo." Tuliingia ndani na tukaongea mpaka usiku. Basi, niliimuambia ninahitaji kwenda kitandani kwa sababu Mungu atazungumza na mimi usiku wa leo katika ndoto. Nilidhani angeongea nami katika ndoto, lakini haikutokea kama nilivyowaza. Lakini alisema nami kwa njia ya tofauti. Nilipokwenda katika chumba cha kulala na nilipotoa nguo zangu, chumba kikaanza kutikisika. Na nilianza kupiga kelele, "Ni tetemeko linaikumba Santiago, Chile." Nilijaribu kuondoka katika chumba changu, lakini mtu asiyeonekana alinizuia kupita mlangoni. Nilikuwa na uwezo wa kumuona mama yangu na familia yangu katika chumba hicho na nilipiga kelele kwa msaada lakini hakuna mtu aliyeweza kunisikia. Sasa najua, kiumbe huyu asiyeonekana alikuwa ni malaika wa Bwana. Nilirudi nyuma na kujilaza juu ya kitanda changu na nikalmlilia Mungu, nikaomba aniambie nini kinaendelea. Sauti ikasema nami. Roho mtakatifu akaanza kusema nami katika sauti nzuri sana, akisema, “Ricardo, Kwa kuwa umeacha kazi kwa sasa, nitahitaji wewe uende kanisani na uwe unaomba kwa muda wa saa saba kila siku kwa maisha yako, na kwa kanisa langu duniani.” Baada ya Bwana kuacha kuongea nami, chumba kikaacha kutikisika. Nikaainua mkono wangu na kuona ya kuwa ninaweza kuondoka chumbani tena. Kishanikamkimbilia mama yangu na kumueleza “ Nimesikia sauti ya Roho mtakatifu” na nikatoka nikaanza kuongea kwa sauti nje ya nyumba. Watu hawaamini kuwa Mungu bado anaongea na watu hata leo lakini nakueleza ni kweli, Anaongea na watu! Kama Bwana aliweza kuongea na Abrahamu, anaweza kuongea nasi pia na kanisa lake leo. Nikaenda kanisani na kuongea na Askofu na tukakubaliana kufungua kanisa kila siku asubuhi saa 2 ili niweze kutii agizo la Mungu alilonipa. Kila asubuhi nilikwenda kanisani na nikaomba saa moja, mawili na kwa mara ya tatu sikuwa na chochote cha kuombea na nikawa nikimuuliza Mungu, “ Bwana ni kitu gani kingine niombee?Nimebakiwa na masaa manne yaliyobakia!” Kisha, nikasikia tetemeko linatokea nyuma ya mlango wa kanisa. Nikahisi kanisa linayumba kushoto na kuliakama mtu aliyelewa. Lilipokuwa likiyumba, nikasikia sauti ikiongea nami lakini wakati huu haikuwa sauti kama ile ya kwanzaniliyokuwa kwenye maono. Suti ile ya kwanza ilikuwa ya mamlaka, lakini wakati huu aliongea nami kwa sauti ya huzuni. Akasema, “Ricardo, Ricardo omba kwa ajili ya kanisa langu! Kanisa langu si kama lilivyokuwa kabisa, Kanisa langu duniani limebadilika. Kanisa 3 langu limepoteza imani yake. Kanisa langu haliamini kuhusu mimi na wala kuamini kama mimi ni hai hata leo . Liambie kanisa langu kwamba nipo ni hai!! Omba kwa ajili ya kanisa, kwa sababu kanisa langu haliombi wala kufunga tena!” Mtikisiko uliacha baada ya yeye kumaliza.Nikaanza tena kuomba na kutembea juu na chini kwa muda wa masaa manne yaliyobakia nikiwasihi watu wa Mungu wawe na uhamsho. Siku ya Alhamisi ya wiki ya pili ya maombi, niliamka na maumivu makubwa katika mifupa yangu na viungo vyangu na sikutaka kuinuka. Mama yangu alikuwa akiniamsha kwenda kanisani kuomba, lakini nililalamika kuwa mwili wangu na mifupa yangu ilikuwa ina maumivu. Basi akanishauri kuwa niombee pale nyumbani. Hata hivyo nilimkumbusha kuwa Mungu ameniambia niombee kanisani. Hivyo akanisaidia kunivalisha na kunipeleka kanisani. Asubuhi ile kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakiomba pale kanisani, nami nikawaomba waniombee kwa ajili ya mwili wangu kwa sababu ya maumivu katika mwili wangu. Niliwaeleza kuwa nilikuwa mdhaifu sana kuweza kufanya maombi. Hivyo walinipaka mafuta na kuniombea mwili wangu na nikapata nguvu za ajabu kutoka kwa Mungu!!Haleluya! Nikaanza kuomba nikitembea mbele na kurudi nyuma, nikiomba rehema za Mungu kwa taifa la Chile na kwa familia na watu walioathiriwa na madawa na kwa kanisa. Nilimaliza maombi na kisha nikarudi tena baadae kwa ajili ya ibada ya usiku. Baada ya Baraka za askofu,niliinua mikono yangu na nikahisi mtu fulani alipita na kuugusa mgongo wangu. Lilipotokea jambo hili nilipoteza nguvu zangu zote na nikaanguka sakafuni.Askofu aliniuridha nini kilikuwa ni tatizo na mimi, na nikajibu hata sifahamu, nikamueleza kuwa sina nguvu na siwezi kuzumgumza vizuri. Kisha kanisa likanizunguka na kuanza kuniombea kwa lugha huku wengine wakiomba kwa sauti. Baadhi ya watu walianza kuona malaika akija na kuniuliza niuache mwili wangu. Askofu akakemmea, “Hautauacha mwili wako!” Aliposema hivyo, Malaika waliacha kuniita ili niuache mwili wangu. Unaona, Mtu yeyote mwenye mamlaka katika Yesu ataheshimiwa na malaika wa Bwana. Askofu akaniomba pia, “Kwa muda gani malaika anahitaji akuchukue kutoka katika mwili wako?” Nikamuuliza malaika, “unanichukua kwa saa moja?mawili?Matatu?”Malaika akajibu, “ hapana, utaondoka kwa muda wa masaa 8 kwenda kumuona Yesu katika mbingu ya tatu kwa sababu anataka kuongea nawe.”Kisha malaika akanieleza, “Mimi siye ambaye nitakuongoza wewe kwenda mbinguni, kwa sababu mimi ni malaika wako ambaye nimekulinda wewe kila siku tokea kuzaliwa katika dunia hii. Malaika wawili watakuja kutokea mbinguni ili kukuchukua wewe mpaka mbingu ya tatu usiku wa manane.” Nikamueleza hili askofu na na akaazimia kunichukua mimi kwa gari ya ndugu mmoja katika kristo kwa nyumba ya mchungaji katika ghorofa ya pili. Nilipofika tu chumbani, tuliweza kusikia mbwa wakibweka na watu wakilia. Baada ya maono yangu nilielezwa kuwa wanaume wawili waliovalia mavazi mazuri meupe yanayong’aa walionekana mtaani na wakaja hadi ghorofa ya kwanza ya nyumba na wakapanda hadi ghorofa ya pili nilipokuwepo. Malaika hawa ni wazuri. walikuwa na nywele nyeupe zinazong’aa, nyeupe zaidi ya barafu/theluji, na macho yao yalipendeza kama lulu.Ngozi yao ilikuwa nyororo kama ya mtoto lakini bado walikuwa wakionekana kuwa na misuli kama wanyayuaji wa vitu vizito(bodybuilders). Malaika hawa walikuwa na nguvu!! Kisha nikamueleza Askofu, malaika hawa wako mahali hapa walotumwa kunichukua twende mbinguni.Malaika mmoja akaanza kunisihi niuache mwili wangu. Lilipokuwa likitokea hili, mifupa yangu ilianza kuniuma tena. kwa hiyo ndugu wangu katika Kristo pembeni mwangu walianza kunichua na kunieleza kuwa walihisi baridi ikiongezeka katika mwili wangu.Kwa hiyo walichukua hita ili kuupa joto mwili wangu, nilianza kuogopa na kuanza kwenda huku 4 na huku. Nilianza kuhisi kifo kinanichukua na nikasema kwa sauti wa ndugu zangu hawa katika Kristo, “ Msinizike, nitarudi tena!” Niliuacha mwili wangu na nikarukia kitandani. Niliwaona ndugu hawa wakiushikamwili wangu na kusema, “Ameondoka, “Ameuacha mwili wake!” Lakini nilikuwa pembeni yao nikiwaeleza “niko hapa!” Lakini hawakuweza kuniona kwa sababu ulikuwa ni mwili usioharibika wa kiroho. Ndugu hawa walianza kuufunika mwili wangu katika blanketi. Malaika mmoja aliniambia, “Ni wakati wa kuondoka sasa kwa kuwa Bwana anakusubiri!” Kila mmoja aliushika mkono wangu na kuninyanyua kwenda mbinguni na tulipita katika anga kwa mwendo wa mwanga. Nitakueleza wewe hivi, hata kama hauamini mojawapo ya mambo haya, Yesu Kristo yupo na anaishi milele!! Baadae ,Bwana aliponieleza niurudie mwili wangu , nikimueleza,, “ Ni nani katika dunia ataniamini, niache tu niishi na wewe!! hakuna atakaye amini huu ufunuo, hakuna atakayeamini kwa sababu hawana imani! Tatikzo la kukosekana kwa imani ni kubwa sana, ni nani ataamini huu ufunuo?” Bwana akajibu, “ Kuna mtu fulani ataamini maono haya, ni wale walio wa kanisa langu la kweli wataamini.” Nilipokuwa nimeuachaa mwili wangu usiku ule nilikuwa nikipaa kwa spidi ya ajabu nikiwa naenda kwa Bwana. Niliweza kuangalia chini na kuona sayari dunia. Kisha nikapita karibu kabisa na mwezi, Mwezi huu mzuri uliiangaza anga usiku katika dunia. Kisha, niliweza kuona jua na ukubwa wake kwa macho yangu; Niliweza kuona miali ya moto ilivyokuwa ikilipuka na kutoa joto mpaka kwenye dunia. Kisha tuliendelea na kuona nyota nyingi tulizozipita. Mungu aliruhusu mimi nione jua, mwezi na nyota kwa kusudi: Kusudi hilo ni kuuambia nyinyi nyote kwamba Mungu wetu ni muumbaji mkuu wa Ulimwengu!!! Si mdogo kwa namna yeyote ile! Tuliendelea kusafiri kwa mwendo huu mkali hadi tulipofika mahali ambapo hakukuwa na nyota tena. hakukuwa na uumbaji wowote, ilikuwa ni Giza tu.Niliweza kuangalia chini na kuona nyote zote zikiwa chini. Nilianza kuogopa na nikawauliza malaika, “Mnanipeleka wapi? Nirudisheni kwenye kitanda changu duniani” walinishika na kunibana zaidi na kuniwekea miguu yao kwa miguu yangu na kunishika. Nilianza kulegea kwa sababu ya hofu niliyokuwanayo. Malaika wakaniambia “ Nyamaza Kimya! Tunakupeleka kwenye mbingu ya tatu ambapo Yesu anakusubiri ili aongee nawe!” Malaika walisimama na wakati huu niliangalia pande zote na sikuona chochote cha uumbaji, sifahamu nilikuwa wapi, nafikiri ilikuwa ni mbingu ya pili. Kisha nikiwa katika hali ya kujiachia malaika wakiwa wamenishika na mara nikajisikia na kusikia kelele za kutisha juu yangu. Malaika wakanibana na kusema, “ Ricardo, usiogope, Yesu yuko pamoja nasi!” walipokuwa wakiongea,walisema, “ Inua kichwa chako na uangalie juu yako!” Nilishangazwa sana na kile nilichokiona kwa sababu kulikuwa na viumbe vilivyokuwa katika mwendo juu yetu. Malaika mmoja akasema, “ Angalia, tutakuonyesha wewe kile ambacho unakiona juu yetu! Malaika mmoja akanyoosha mkono wake akapunga huku na huku ili kutoa mwanga uangaze sehemu yote ile ya anga ili kuona kitu kilichokuwepo mahali pale. Anga lilipokuwa na muangaza hakukuwa na kitu chochote ila mapepo na mashetani yalikuwa yamezunguka anga lote lile. BWANA AWAKEMEE WOTE KWA JINA LA YESU!!Biblia ni kweli!! Kila kitu kinachoendelea katika ulimwengu huu ndo kile ambacho unakiona katika Ufunuo. Yesu anakuja hivi karibuni!! Nawezaje kukushawishi, ni hivi KARIBUNI!!Nikamuuliza malaika, “Mahali hapa ni wapi?Mmoja akajibu, “ Hapa ni mahali pa ulimwengu wa Giza ambapo Shetani na malaika zake ( mapepo) wanaishi,” Akaanza kusema, “ Ndio maana kuna uharibifu mwingi duniani! Mapepo haya yanakuja duniani kutokea mahali hapa na kusababisha uharibifu na uovu wa kila 5 aina na uovu katika makabila ya wanadamu!” Dunia imejaa mapepo!” Kuna mapepo milioni na milioni , idadi haihesabiki. Kisha malaika, alianza kunipeleka niangalie kwa ukaribu na kunionyesha sura za viumbe hivi na nyingi ya hivi viumbe vimekwisha onekana kwenye Runinga. Viumbe hivi ni VIBAYA!! Niliona viumbe vilivyofanana na viumb vya kwenye michezo ya runinga ya Thundercats na Power Rangers na katuni ya caricatures ambavyo ni halisi kabisa kwa maisha ya duniani. Wabunifu wote wa muvi na michezo hii wameweka mkataba na shetani kutoa vitu hivi kwenye runinga na sinema!! Michoro yote ile inatokea katika ulimwengu war oho ambao niliuona. Unafikiri kwa nini watoto wa siku hizi wamekuwa wakaidi?? ni kwa sababu mapepo haya yanawanigia watoto hawa wanapokuwa wakiangalia maonyesho haya ambayo yanawaoyesha wao (mapepo). Ndiyo maana imetupasa kuwafundisha watoto kuchagua nini cha kuangalia kwenye TV. Malaika aliniambia hiki ni halisi na kweli. Mapepo haya yote yapo na watu wanafanya makubaliano na shetani ili kuleta mapepo haya duniani. Haya mapepo yanaanza kunitukana mimi, na kanisa, na Baba, na Bwana Yesu na Dunia kwa sababu hawamuheshimu Mungu au uumbaji wake wowote. Kisha nikaona kiumbe halisi kabisa kiitwacho Hugo, huyu ni katuni maarufu sana nchini Chile. Ilikuwa inaogopesha kuangalia. Alikuja karibu yangu na kunieleza, “Tutaenda duniani na kuwaua watoto wote!” Kwa nini unafikiri watoto wanaua watoto wenzao? Ni kwa sababu baadhi yao husema kuna kitu kilikuja kutoka katika runinga na kuniambia nifanye hivi au vile. Mapepo haya hupanda chuki duniani, Bwana akomboe na kusafisha Chile!! Mmoja wa malaika akaniambia “Endelea kuangalia!” Na mapepo yakasema, “Tumejaribu kuharibu kanisa, lakini hatuwezi kwa sababu tunapomuuua mmoja, basi wanainuka maelfu kuchukua nafasi ya kifo chake!” Tokea kuanza kwa kanisa, Shetani amejaribu kuliharibu, kanisa ambalo huubiri injili ya kweli na kufanya kazi ya Mungu, lakini hawezi kwa sababu Yesu anatulinda! Utukufu kwa Mungu! Kisha mapepo yakasema, “Ngoja tufanya jambo jipya, ngoja tuingie makanisani, kwa sababu pale kuna wengi ambao ni wetu! Tutaenda kuwatumia watu hawa kusambaza umbea na kuleta migawanyiko katikati ya ndugu ndani ya kanisa.” Shetani anazunguka kila mahali akitafuta kuharibu wale wanaopenda haki ya Mungu. Kama andiko linavyosema: 1Petro 5:8 Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mawindo. Sikutaka kuendelea kuona tena, lakini malaika akaniambia niendelee kuangalia matukio yanayotokea. Niliona mapepo yakiruka kila kona pindi nyota moja ing’aayo ilipokuwa inakuja. nyota hii ilipokuwa inatokeza na kusogea, ilikuwa inaleta sifa nyingi na ibada kwa Bwana. Hii haikuwa nyota kama nyota, kumbe ilikuwa ni mamilioni ya malaikawakiwa juu ya farasi weupe wakimtukuza Mungu wa Majeshi!! Walikuwa wakiimba “Mtakatifu,Mtakatifu, Mtakatifu, ni yeye aishie enzi na enzi! Bwana ndiye Alpha na Omega, Mwanzo na Mwisho na kila chenye pumzi na kimsifu Bwana!” Kisha nikaaona vita kubwa na 6 sikuona mapepo tena. “Usiogope kabisa kwa sababu kuna malaika wengi zaidi upande wetu zaidi ya upande wa adui!” Malaika walifa ya njia mpaka mbingu ya tatu. Walijigawa katika makundi mawili, moja kulia na jingine kushoto.Ilikuwa ni njia iliyowazi mpaka mbingu ya Tatu! Njia hii ilinyooka mpaka mbinguni na uliweza kuona Mji mtakatifu wa Mungu. (Kuna picha ya satellite duniani ambayo imechukua picha kutokea katika mji huu. Mji huu Mtakatifu upo! Hii imetokea kwenye radio na TV.) Nilweza kuona njia ya utukufu na malaika wa ajabu. Waliisafisha njia yote kuwafukuza mapepo na hawakuacha kumsifu Mungu na kubariki Jina lake! Malaika wakaniweka mbele yao na kuniambia, “ Imekupasa kusubiri hapa!” Kwa mbali, niliangalia na kutokea katika mji huu niliona mtu fulani akiwa na mazazi mazuri meupe amepanda farasi mweupe. Mtu huyu alipokuwa akizidi kunisogelea, malaika waliendelea kusifu jina la Mungu na kumtukuza. Mtu huyu alikuja mpaka umbali wa mita 4 tokea nilipo. Kiumbe huyu alikuwa mzuri, alikuwa ni mzuri zaidi ya wale malaika wengine. Nilitegemea angeongea nami, lakini alichokifanya ilikuwa ni kuniangalia na kusema kwa sauti, “Mimi ni malaika mkuu Mikaeli ambaye ninajukumu la kukulinda wewe pamoja na kanisa la Duniani!” Nilimuona malaika mkuu Mikaeli uso kwa uso na alikuwa ni kiumbe cha thamani sana! Aligeukia upande wake na kuonyesha njia ya mimi kuingia mji Mtakatifu. Alisema, “Ingia! Bwana Yesu anakusubiri!” Nilikuwa nikitembea katika njia ile nikifuata mji ule na nilipokuwa nikitembea, Malaika walikuwa wakiimba na kumsifu Bwana. Nililia na kulia nilipokuwa nikiuangalia mji ule. Mji ulikuwa umeumbwa kwa dhahabu halisi angavu na mlango wa kuingilia ulikuwa umeundwa kwa lulu. Sakafu ilikuwa ni ya muonekano wa kioo angavu(crystal). Sijawahi kuona kitu kama hiki duniani na hakuna mwanadamu awezaye kukiunda. Msanifu wa majengo ya mbinguni ni Bwana wetu na Mungu wa Ulimwengu wote.Nilikuwa nje ya mji na milango yote ilikuwa imefunguliwa. Na milango hiyo ikiwa bado hii wazi, niliweza kuona ndani na katika kuta kulikuwa na madini ya Rubi na safira na lulu ambayo yaling’aa. Na ndani ya mji ule kulikuwa na sauti milioni na milioni ya sauti zikimsifu Mungu! Nilitetemeka kutokea nje ya mji niliposikia hivi. nilisikia sauti moja ambayo ilitikisa mbingu na nyuma ya sauti hii ilikuwa ni mamilioni na mamilioni ya sifa kwa Mungu yakisifu “Mtakatifu, MtakatifuMtakatifu ndiye mwanakondoo wa Mungu na Baba ambaye utukufu una yeye na heshima milele na milele AMEN!” Sauti kubwa ikasikika ikisema “IWENI WATAKATIFU KWA SABABU MIMI NI MTAKATIFU! NI WATAKATIFU TU NDIO WATAKAOINGIA KATIKA MJI HUU!KWA SABABU PASIPO UTAKATIFU HAKUNA ATAKAYEMWONA BWANA.” Bila utakatifu hakuna atakayemuona Bwana. Sauti ikasikika ikisema, “Ingia” na nikaingia ndani ya mji ule. Na nikaona Kiti cha ajabu cha enzi kimezungukwa na moto. Na moto unatoka katika kiti kile cha enzi, Nikatulia kimya na nikamuona Yesu , Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana! Nilijihisi mdhaifu mbele zake na nikaanguka chini nikaishiwa na nguvu.Mkono wake ukatoka kwenye miali ile ya moto na kunishika na akasema, “Simama kwa miguu yako!” Nilipata nguvu na nikasimama. Nilianza kugusa miguu yake na mikono yake na mwili. Nilipoona uso wake, muonekano wake ni tofauti sana na wachoraji wa dunia wanavyochora katika michoro yao! Watu wengi wanaunda miungu ya mbaona wengine taswira mbalimbali! Lakini nataka nikuambie hivi ndugu yangu, Yesu Yule hafanani na taswira hizo. Ni Mungu mwenye misuli na nguvu! Si Mungu wa ukawaida, Ni Mungu mwenye nguvu zote!! Anasema, “Mimi si Mungu niliyeumba na mbao, au chaki,Ni Mungu ninayeishi!” Anaendelea, “Liambie kanisa langu duniani mimi ni halisi!! Ni kweli ninaishi na nipo! Waambie watu wangu kuwa Mbinguni ni Halisi na ninawasubiri!” Aliniambia,“Njoo, tembea pamoja nami na nitakuonyesha jambo moja kubwa. 7 Tuliangalia chini na niliweza kuona dunia na vitu vyote vilivyofanywa kwenye dunia. Yesu akasema, “Ninaweza kuona kila kitu ambacho kanisa langu linafanya!” Anajua kila kitu tunachokifanya na mimi niliweza kuona wengi wenu kutokea mbinguni. Yesu akaniambia, “Angalia katika kanisa langu!” Niliweza kuona ndugu kwa ndugu, na makanisa kwa makanisa. Yesu akaniambia, “Kanisa langu limepoteza imani yake,hawataki kuniamini, uovu umeongezeka duniani na watu hawataki kuamini kuwa nipo. Waambie watu wangu ninakwenda kufanya kitu kikubwa duniani! Kanisa langu linarudi nyuma badala ya kukua.” Bwana alianza kulia kwa ajili ya kanisa lake na akasema, “ Hili kanisa si kanisa langu! Nikamuambia Bwana, “Bwana usiseme hivyo! Wewe unajua kuwa tu kanisa lako.” Bwana Yesu akajibu, “Hapana kanisa langu linatembea kwa nguvu za miujiza,ishara na maajabu! Kanisa langu limepungua! Hatahivyo, waambie, nitakuja kuwafufua tena!” Aliniambia niendelee kutembea pamoja nae na tulikwenda mahali fulani penye mlango na mlango ulikuwa umetengenezwa kwa dhahabu halisi.Nilianza kukimbia huku na huku kwenye mtaa uliofanywa kwa dhahabu na nikawa ninachukua vumbi la dhahabu na kujipaka kwenye mwili wangu. Na Yesu aliniambia nirudi na akaniambia kuna mitaa ya dhahabu mbinguni. “ Hii yote ni urithi kwa watu wangu,” Bwana akasema. “ Lakini kwenye kanisa langu kuna wezi wengi ambao wananiibia fungu la kumi na sadaka! Waambie watu wangu hakuna mwizi atakayeingia kwenye ufalme wa Mungu!” Inabidi turekebishe maisha yetu kwa ajili ya Bwana.Kisha tuliona meza ndefu sana kwa ajili ya watu mamilioni ikiwa na chakula cha kutosha na vinywaji. Kulikuwa na mataji mengi na glasi kwa ajili ya watu kunywea. Bwana akasema, “Yote haya yameandaliwa kwa ajili ya watu wangu!” Meza hii iliandaliwa kwa ajili ya harusi ya Mwana kondoo. Kuna dada mmoja katika Kristo ambaye pia alipelekwa mbinguni na kasha aliona malaika wakienda na kurudi wakiwa wanatayarisha chakula cha Harusi hii! Nikamuambia Bwana, “ Kwa nini dada huyu aliona malaika wakitayarisha vitu hivi, lakini mimi sioni matayarisho yoyote yanayofanyika? Bwana akajibu, “Ni kwa sababu matayarisho yote yamekamilika!” Kuna mataji kwa wote wanaofanya kazi na ni watii kwa Bwana. Kisha nikamuuliza, “ Bwana utakuja lini basi,kama maandalizi yote yamekamilika?Itachukua muda gani mpaka utakaporudi? Nionyeshe muda, Ni muda gani umebaki katika saa ya mbinguni?” Watu wengine wamekuwa na maono ya muda, wakionyesha kuwa itakuwa ni usiku muda ambao Bwana Yesu atarudi. Niliuliza, “ Ni lini saa itagota katika mshale wa saa sita usiku?Je ni dakika moja imebakia? dakika tano?” Bwana Yesu akausoma uso wangu kwa muda kidogo, kasha akajibu, “Ricardo,mbinguni hakuna muda tena!” Kisha nikaitikia, “Vizuri bwana , kama hakuna muda tena, kwa nini bado haujarudi?” Yesu akanyanyua mkono wake na kuchukua kidole gumba chake na vidole vyake vingine na kunionyesha alama inayoonyesha kitu fulani kidogo sana na akasema,“Muda wote uliobakia ni Neema ya Mungu kwa wale waliorudi nyuma warejee tena na kutubu na kuifanya kazi ya kwanza.” Na Bwana wa Majeshi hajarudi kwa sababu ametupa sisi sote muda kidogo sana wa kutubu na Muda huo unaitwa, “ Muda wa neema/rehema ya Baba” Yesu anarudi muda wowote, ni lazima tuanze kumtafuta kwa moyo wetu wote na tufunge na kuomba na tuzifanye kazi za kwanza. Nimemaliza kila kitu. Yesu alirudia, “ Tuko kwenye muda wa Neema ya Mungu!” Kisha malaika alitokea upande wetu wa kuume akisema kwa sauti, “Muda umewadia!! muda umekwisha. Maandalizi yote yamekamilika! Yesu anampokea bibi harusi wake( kanisa)!” Bwana Yesu anarudi na kila ishara iliyoko kwenye maandiko inatimia! Sinema zinaonyesha kitu fulani cha kutisha kinakuja. Wanasayansi wanatambua kitu fulani kikubwa kitatokea, hawajui ni kitu gani hicho!Hatahivyo, Sisi kanisa tunatambua kwamba Yesu anarudi hivi karibuni! Malaika walipomaliza kusema, kasha mamilioni ya malaika walianza kuruka na kushangilia kwamba bibi harusi(kanisa) linarudi mbinguni. Nikaendelea kumuuliza, “ Kitu gani kinaendelea?” Lakini hakuna aliyeonekana 8 kujali, wote walikuwa wakishangilia kwa habari njema. Nilijumuika na malaika na kuanza kulisifu jina la Yesu pia! Wakati huo nilipoinua mikono yangu nilihisi mtu fulani ameninyanyua kuondoka mbinguni na kunirudisha chini kwa spidi ya ajabu. Hivi sasa, malaika wanashangilia kwamba Bwana Harusi anarudi. Nilirudi duniani na niliachwa pale madhabahuni kanisani ambapo nitakuwa ninaomba kila siku. Muda ni mfupi sana!! Kama hutaki kuniamini mimi, basi usiamini. Lakini anakuja na itakuwa ni ujio wa milele. Watu wa Mungu hawaamini katika unyakuo. Tafadhali amka, Kwa jina la Mungu amka katika ukweli!! (Ricardo analia). Bwana Yesu alikuwa karibu yangu, na aliniambia, “Ricardo, hivi ndivyo ambavyo unyakuo utakuwa kama utatokea hivi sasa!” niliweza kuona dunia yote na Roho mtakatifu mzuri ambaye anatupa amani na furaha ya kuishi katika dunia.Kisha nikaona kama mvuke ukiingia kanisani na ukanizunguka na nikamuuliza Bwana, “Hii ni nini?” Akasema, “Hiki ndicho nakiita Unyakuo.”Kisha nikaona watu wakivunja milango ya kanisa, wakitaka kuja ndani, na kupayuka, “Watoto wangu wako wapi? Wote wametwaliwa!” Watoto wote katika ulimwengu wametwaliwa kwa sababu Mungu hata waacha nyuma. Mtu wa kwanza kuingia katika kanisa alikuwa ni Mwalimu wa kwaya, akapayuka, “ Kanisa liko wapi! nimeachwa nyuma! Nimebaki! Nimebakia!” Baada ya mwalimu wa kwaya, niliona wachungaji wengine, waumini wa wakiume na wa kike,na waangalizi wa kanisa wote wanalia, “Nimeachwa nyuma!” Wazazi wengi na wanandoa wengi waliwatafuta wale wawapendao na watu wale walioko kanisani wakawajibu, “Muwapendao hawako mahali hapa! Bwana amewachukua,” Watu hawa walianza kulia, “Yaani kumbe ni kweli, Yesu amekja na kuchukua bibi harusi!”. Watu walikuwa wakilia na kuomboleza wakitamani kama tu wangemuamini Yesu Kristo. Kila mtu asiyemuamini Yesu kama Masihi amepotea! Nikaona watu wengi na wachungaji wakilia na watu walianza kuwadai wachungaji, "Kwa nini wewe hukuhubiri ukweli, kwa nini hukufundisha utakatifu na kunionya mimi kuhusu yote haya? Ni kwa sababu yako nimeachwa nyuma! "Wengi wataachwa nyuma kwa sababu hawaishi maisha matakatifu. Tunahitaji kuhubiri utakatifu wa kweli na kuwafundisha watu toba ya kweli! Niliona jinsi watu walivyopiga wachungaji na kuwakatakata na kuondoa nywele zao. Wachungaji walilia na kuomba watu wasiwadhuru. Watu hawakuacha kwa sababu walikuwa sasa na mapepo. Kuna makanisa kabisa ambayo yataachwa nyuma. Nilimuona kaka mmoja alikuwa anajaribu kuyakwarua macho yake mwenyewe kwa sababu ya huzuni kuu. Na watu walipigiza vichwa vyao sakafuni na kwenye kuta kwa sababu hawakutambua kuwa Yesu alikuwa ndiye jibu pekee. Kwa sababu watu walitaka kuendelea katika dhambi na uovu na kuishi maisha vile walivyotaka. Watu walijikata wenyewe na kupigiza vichwa vyao mpaka kiasi cha kuona fuvu zao zikiweka ufa na walianguka chini. Damu ilitiririka bure ndani ya kanisa kwa watu ambao walikuwa wakijijeruhi wenyewe. Kisha nikaona kijana akipiga kelele kwa Mungu, "Tafadhali Bwana, nichukue!" Alikuwa amechelewa mno. Yesu alikuwa tayari amekwishakuja na kulipokea kanisa lake. Hapo nilianguka chini kwa sababu niliona mambo mengi zaidi ya kutisha. Yesu akaniambia, "Katika dhiki kuu, kutakuwa na matatizo makubwa haijawahi kutokea kabla." Kisha nikauliza, "Kwa nini watu wanaruka nyuma baada ya kuumizana vibaya wao wenyewe?" Bwana Yesu akajibu, "Kwa sababu kwa wakati huu, watu watatamani kifo, lakini hawatakipata. Kifo kitakuwa kimetoweka katika uso wa dunia. Nilimwuliza Bwana, "Kwa nini wachungaji wote hawa na watu wameachwa nyuma?" Na Bwana akasema, "Kwa sababu ninajua mioyo yao. "Mungu anatujua sisi .. Anajua yote ya mioyo yetu. Nilianguka chini, karibu kuzimia. Yesu alisema, "nimetaka kukuonyesha 9 hili ili kwamba uonye kanisa langu na kuwapa matumaini. Waambie kwamba kama watu watatubu sasa, mimi nitawasamehe wakati bado kuna muda. Nitafanya jambo kubwa katika dunia. " Tafadhali,fungua macho yako. Kanisa la kiinjili nchini Chile linaongezeka. "Waambie watu wangu kama wataomba msamaha, nitawasamehe." kisha nikaona maono mengine na nikaona moto umefunika mbingu nzima. Yesu akasema, "Je, umeweza kuona? Huo moto uliona juu ya nchi/dunia, ni moto juu ya nchi ya Chile. Kwa sababu Chile itakuwa kwa ajili ya Kristo! Mungu ataibadili Chile! " kisha nikaona moto unataka kuja juu ya Chile na Yesu akasema," Macho ya Baba yangu yako juu ya Chile. "Mara moto utakapokaa juu ya Chile, nchi nyingine zitaona na kujua kuwa Mungu yuko mahali hapo. Kanisa lote duniani litafurahi kwa sababu Uwepo wa Mungu unatembea Chile. Bwana alinichukua katika maono mpaka mahali paitwapo "Paseo Humada" Akanionyesha watu waliokuwa vilema na walio na matatizo. Kisha nikaona waamini wa kweli wakiomba juu ya viwete wasio na miguu na wakitiisha viungo kukua. Viungo vilitii na kukua mbele ya macho yao. Watu wasio na mikono waliiota mikono kwa upya mara moja. Wakati huu, Bwana ataonesha miujiza ya uumbaji. Katika makanisa watu ataponywa. Katika siku hii, wafu watafufuliwa na Mungu akutumia wewe ndani ya Chile kufanya miujiza hiyo kama mitume wa zamani walivyofanya katika Biblia. Huo ni ufunuo mzima ambao Mungu alinipa (Ricardo Cid). Yeye anakuja hivi karibuni. Maranatha! Amina! Ndugu aliyefasiri ufunuo wa Ricardo Cid wa Masaa 8 Mbinguni ni Peter Kahale ni kijana aliyeokoka na anampenda Yesu na mwenye shauku ya kuhubiri injili ya Yesu Kristo.

Comments