TB JOSHUA WA NIGERIA ATUA DAR ES SALAAM


H1
Mtume TB Joshua wa kanisa la Church of All Nations nchini Nigeria  ametua jijini Dar es salaam leo  tayari kwa kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli siku ya Alhamisi.

Mara tu baada ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, TB Joshua alikwenda Ikulu moja kwa moja kumsalimia Rais Jakaya Mrisho  Kikwete  kumsabahi na kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani, huku akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha. TB Joshua amepongeza Rais Kikwete pia kwa kupata Dkt Magufuli kama mrithi wake, akimtaja Rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.
Alipowasili alipokelewa  na Rais Mteule John Magufuli kisha pia alimtembelea Mheshimiwa Edward Lowasa.
Hizi hapa habari Picha katika matukio ya ujio wa Mtumishi wa MUNGU TB Joshua.



Rais Kikwete akisalimiana na TB Joshua

TB Joshua akiwa na Mheshimiwa Lowasa

TB Joshua akiwa na Rais Mteule John Magufuli pamoja na familia ya Mwesimiwa Rais Mteule

Mapema akiwasili alipopokelewa na Rais Mteule Mheshimiwa John Magufuli.

TB Joshua akisalimiana na Mheshimiwa Lowasa.






Comments