TUKIO ALILOLIFANYA BWANA YESU LAFANYIKA KPC.


Mchungaji Elly  Wakati wa Ibada.

Mchungaji Elly Botto ni mtumishi wa MUNGU ambaye MUNGU amekuwa anamtumia sana katika maombi ya kuwafungua watu waliofungwa na nguvu za giza na wanaoteswa na kila laana na kila hila za shetani. Mtumishi  huyu ambaye ndie Mchungaji kiongozi wa Pentecostal Asemblies of God(P.AG) Kawe Dar es salaam , kanisa ambalo ni maarufu kwa jina la Kawe Pentecostal Church(K.P.C)  leo pia ROHO wa MUNGU amempa ufunuo wa ajabu ambao kupitia ufunuo huo ROHO MTAKATIFU na nguvu zake alidhihilika katika kanisa.
Rev. Botto alikuwa anafundisha somo liitwalo NGUVU KATIKA  UMOJA, Katika ujumbe huo alianza na andiko  la Kumbu 32:30 linalosema '' Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa?''   Kisha akaendelea na maandiko mengine lakini alipokaribia kumaliza kufundisha alimwagiza mmoja wa mashemasi akachote maji kwenye bomba nje ya kanisa kisha akasoma maandiko ya Yohana 13:14-15  yanayosema '' Basi ikiwa mimi, niliye BWANA na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. '' Baada ya kufafanua andiko hilo Mchungaji Botto akasema ''Tunataka tufanye tendo la Imani alilolifanya BWANA YESU''
Baada ya neno hilo kanisa lilianza kumwabudu MUNGU na huku tendo la imani la kutawadhana miguu iliendelea ambapo kuna baadhi walipokea nguvu za ROHO MTAKATIFU na kuna ambayo walifunguliwa na kuwekwa huru.
Hizi hapa habari picha katika ibada ya leo. Pia Kama utahitaji maombezi kwa njia ya simu bure kabisa unaweza ukampigia mchungaji Elly Botto kwa namba 0719640642 au  0752965812

Schola Mabula katika uwepo wa nguvu za MUNGU akimuonya miguu Lidia Yohana.

Mzee Kiongozi wa Kanisa la KPC akimuosha Miguu Tobietha Karistus.

Wakati wa maombi ya utulivu.

Askofu Joel Nondi kutoka Kondoa Dodoma alikuwepo kanisani kwenye ibada hiyo ya maajabu lakini hapa akimuosha miguu Bibnti Esta Joseph
Baada ya kuosha miguu nguvu ya MUNGU ilishuka

Wakati wa Neno.

Mama Mchungaji akimuosha miguu Binti huyu.

Maombi.

Mchungaji Elly Botto akumuosha miguu dada Veronicah

Kuna wengine walishindwa kukaa katika kiti baada ya nguvu ya MUNGU kudhihilika.

Katika uwepo wa ajabu wa nguvu za MUNGU.

Issa Danda akioshwa miguu na Mchungaji Botto.

Daudi Lubeleje akioshwa miguu na mchungaji Elly Botto.




Mama mchungaji akimuosha miguu Mzee kiongozi wa kanisa.



REV. Elly Boto akiombea.
Mkao wa kupokea baraka.


Nguvu ya MUNGU ya ajabu iliposhuka kwa muimbaji huyu wa nyimbo za injili Teddy Lukindo.

Godfrey Kessy Katika huduma.

Comments