USITOE MIMBA

Na Mwl Nickson Mabena

Siku Moja nilihudhuria Ibada kwenye kanisa flani Kubwa Jijini Dar es salaam, Roho Mtakatifu akasema na Mchungaji kwamba kuna Binti ametoa Mimba, Mchungaji akatangaza ili kama yupo amuongoze Sala ya Toba,
Nilichoshangaa, Walitoka Mabinti Wengi sana, Wengine wakawa wanasita sita kutoka,
Kwa Idadi ile ya watu zaidi ya 20, nikastaajabu, Kumbe Mchezo wa Kutoa Mimba ni Mchezo unaofanywa na Mabinti wengi sana.
Yaani Unarukaruka kwenye Uzinzi na uasherati wako Unaringia KUTOA MIMBA... Haa!.
Kutoa Mimba ni Dhambi ya KUUA,
Unaua Kiumbe kisicho na Hatia, alafu bado unajifariji Kwa Sababu unahudhuria Kanisani, na Kwaya Unaimba, tena ni Kiongozi wa Sifa!.
Nawaza hapa, Watoaji Mimba wengi kwenye Makanisa Makubwa, hasa ya Mitume na manabii, Ambayo hayakemei DHAMBI, Wamejificha humo!.
Eti Unatoa Mimba ili tukuone Bado Binti, tukuone Bado hujazaa.. Sasa tukishakuona hivyo ndio inakuaje!?.
NAKUSHAURI: TUBU LEO, MGEUKIE YESU MWOKOZI, OKOKA...
DUNIA HAINA PA KUKUPELEKA,
YESU ANA PA KUKUPELEKA...

USIZINI, USIUE, USITOE MIMBA!.

 Siku moja usiku nilipogiwa simu na Mama Mmoja ambaye ni Ndugu yangu, baada ya kusalimiana,
alinambia kuna jambo anataka aniulize, nikamwambia sawa,
Akanambia, ana rafiki yake amechumbiwa na kijana Mmoja, walikua wameshatambulishana kwa wazazi, sasa katika kuendelea na Maisha ya kila siku, Yule Binti akapewa Mimba na kijana mwingine tofauti na yule aliyemchumbia,
Binti hataki Mchumba wake ajue kama ni Mjamzito, Maana akijua anaweza akaghairi kumuoa, Kwa hiyo Binti akawaza AITOE ile Mimba, lakini bado yupo njia panda, hajui njia ipi ni salama, kati ya Kumeza Vidonge, au Opereshini, kwa hiyo akataka ushauri kwa huyu Mama aliyenipigia Simu,
Yule Mama akasema "mimi sijui , lakini nina ndugu yangu, amesoma Sayansi, ngoja ntamuuliza", ndugu yake mwenyewe ndio Mimi!.
Mimi nikamjibu kwenye Simu, Nikamwambia, Mwambie asitoe Hiyo Mimba, hicho kiumbe hakina hatia, Kama Kufa, yeye ndiye anastahili Kufa, Maana Biblia inasema Mshahara wa Dhambi ni Mauti, yeye amefanya Dhambi, Mtoto hana hatia, kwa nini amuue!?.
Nikasema, hakuna Njia salama hata moja kati ya hizo, zote ni Dhambi!!!.
Nikuuliza, na Wewe.. 👇👇👇 👉Unatoa Mimba ili UOLEWE!?,
Ndio Maana huolewi sasa, Maana hakuna sababu ya Kuolewa kwako!.
Mungu akupe Mme wa nini!?,
Tatizo lingine nimeliona.... 👇👇👇 👉Mabinti Wengi Vyuoni, wakipata Changamoto za Uchumi, hukimbilia Kulala na Wanaume ili wapate Pesa, Wakipata Mimba, wanakimbilia Kutoa, wengine wanasema Eti Mimba ya BAHATI MBAYA...
Kuna Mimba ya Bahati Mbaya kweli!?, ina maana na Usomi wako wote, hujui matokeo ya Kujamiiana!?.

Unawaona Siku chache wamevaa MADELA (Magauni ya wajawazito), alafu baada ya Wiki chache anarudi kwenye vimini vyake, sasa unajiuliza, ina maana ameshajifungua!?,
kumbe ameshatoa!!.
Mungu akusaidie Unayeusoma Ujumbe huu, Usifanye Mgumu Moyo wako,
Yawezekana Unakuhusu Moja kwa Moja, hakuna haja ya Kukomaa, Bali Kutubu!.

Usifanye Uuaji wa Namna hiyo, ni dhambi kubwa sana, Mama yako angekutoa kipindi hicho, leo hii Usingekuwepo!!.
Yesu yupo kwa Ajili yako, yupo tayari kukuokoa, yupo tayari kukufanya Mtoto wake, yupo tayari kukufanya Kiumbe Kipya!!.
USIZINI, USIUE, USITOE MIMBA!.
Huu ni Ujumbe wangu kwa Mabinti....
Mwalm Nick.
(0712265856 WhatsApp#)

Comments