AMPHIBIANISM KATIKA KANISA

Picha ya Mfano
Bwana Yesu asifiwe sana?

Natumahi umekuwa na siku njema na umebarikiwa.
Mimi nimebarikiwa sana na siku yangu.
wacha nikujulishe jambo moja mpendwa.

Ushaapata kujua kuwa kuna wakristo ambao ni kama wanyama wanaoishi ndani ya maji na nyakati zingine wawezawapata nchi kavu (amphibians) kama vile chura,Kobe,kiboko,mamba nk?

Wanyama hawa huwezi kubainisha maisha yao ni ndani ya maji au ni nchi kavu.
Wakristo pia wapo ambao utashindwa kuelewa wameokoka au hawajaokoka kwa tabia zao mbaya na hata wengine wanatumika madhabahuni.

Wengine wamechangia hata kuwafanya wengine kutoenda kanisani maana wanasema kama wokovu in ule wa fulani hata kanisani siendi.
An amphibian christian ni mkristo yule ambaye leo ameokoka na kesho analewa huku akijitetea kuwa mchungaji wao aliwaambia waonje kidogo.

-An amphibian christian in mkristo asiye na msimamo wa kumtetea Yesu.Wakati umepata shida wamwendea Yesu na shida ikiondoka kanisani hurudi tena.

-Amphibian christian ni mtu yule alitumiaye jina la Yesu kwa kujificha anapotenda dhambi.

-Amphibian Pastor in mchungaji ambaye badala awaunganishe wadada na wandugu kwa ndoa zao anamtaka dada kwanza alale naye ndio afunganishe ndoa yao.

-Amphibian Christian in wewe unayeenda kanisani huku umejifunga hirizi viunoni na madawa ya kiganga kwani haamini kuwa Yesu ni zaidi ya hirizi ya hirizi.

-Amphibian Pastor ni mchungaji aliyeitwa na Mungu na baada ya mwito wake akaingiwa na tamaa na kujiunga na Illuminati ili aongezee upako wa shetani. 

-Amphibian christian ni wewe msengenyaji/mwenye wivu/kiburi huku unasema umeokoka na kutoa ushuhuda mrefu na mtamu sana.

-Amphibian Christian in wewe ambaye wasema umeokoka na kisha kwa facebook unachangia posts za ngono na mambo ya dunia huku ukizichukia za kumtukuza Mungu.

-Amphibian christian ni wewe unayeusomea ujumbe huu kwa guest house na kuniona mpumbavu.

-Amphibian christian in wewe uliyepanga kwenda date na huku watwambia Mungu anazidi kukutendea makuu tangu uokoke.

Amphibian Christian in machukizo mbele za Mungu maana vitendo vyake huiamsha hasira ya Bwana Mungu.
Geoffrey Mwanza.
Tahadhari mpendwa,Mungu hapendezwi na amphibian Christians.Anza kutubu na kuiacha dhambi hii na Mungu atakusamehe na utafanywa chombo kipya.
Ubarikiwe sana.
By Mchungaji Geoffrey Mwanza. 

Tupigie simu kwa ushauri zaidi:
THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES
Geoffreymwanza@yahoo.com
+254724 656 653

Comments