JINSI MAINZI MAFU YANAVYOVUNDISHA MARHAMU YA MUUZA MARASHI!.

Na Mwl Nickson Mabena

"Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima". MHUBIRI 10:1
Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu, habari ya Uzima wako. Natumai unaendelea vizuri katika Maisha ya Kila Siku!.
Leo, nataka tujifunze ujumbe huu, Ambao ROHO WA BWANA ameniongoza kuuleta kwako,
Inawezekana Kichwa cha somo hili ni Kigumu sana kwako, lakini Ukisoma hadi Mwisho utanielewa!
Ukitaka kuelewa vizuri andiko hilo, lazima upate tafsiri ya Neno Moja baada ya Lingine!.
Mainzi Mafu, hawa ni Nzi wanaonuka kwa sababu ya Kufa, Kwa Kiswahili kingine, naweza kusema ni Nzi waliooza!.
Marhamu, haya ni Mafuta ya thamani, na yenye harufu nzuri tena ya Kuvutia, kwa kiswahili cha sasa ningeyaita LOSHENI au Pafyumu (Marashi)!.
Mafuta haya, yalitumika nyakati za Biblia,
Ngoja nikuonyeshe kipindi cha Yesu,
Yohana 12
1 Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwepo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu.
2 Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye.
3 Basi Mariamu akatwaa ratli ya MARHAMU ya nardo safi yenye THAMANI NYINGI, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya Marhamu.
Ukisoma vizuri kwenye hayo Maandiko hapo juu,
Utaona, Mariamu alichukua Marhamu yenye thamani nyingi,
Alimpaka Yesu miguu, na nyumba nzima ikajaa harufu nzuri, ya Marhamu!.
Yuda akataka iuzwe, maana aliona kitu cha thamani 'Kinachezewa'.
Muuza Marashi, ni Mtu anayefanya biashara ya Kuuza Mafuta Mazuri, kutoakana na andiko hilo, naweza nikasema ni Muuza MARHAMU!.
Sasa tuje kwenye Somo, Mhubiri anatufundisha kwamba, Hao Nzi wanaonuka, Wanaweza Kuyavundisha Mafuta Mazuri, Japo Mafuta hayo yanapendwa sana, na yanawavutia wengi, hata Yuda anatamani yauzwe!.
Anamaanisha hivi, Nzi akitumbukia kwenye hayo Mafuta, pamoja na Uzuri uliopo ndani ya hayo Mafuta, Mafuta yatavunda tu!,
Harufu nzuri, Inaweza kupotezwa na uvundo wa MAINZI!
Kadhalika, Upumbavu haba (Upumbavu kidogo), ni Mzito Kuliko hekima na heshima!.
Maana yake ni hii, Mtu ukiwa na heshima kubwa, hekima kubwa, jina kubwa, huduma kubwa, au Mazuri yoyote yale, UKIFANYA Upumbavu haba (yaani kidogo) tu, HUO UPUMBAVU, NDIO UTAONEKANA KULIKO MAZURI YOTE ULIYOTENDA!!.
Mfano, Kiongozi, anaweza akafanya Mazuri Mengi, lakini siku akiharibu kidogo tu, Mazuri yote yanachafuliwa na UPUMBAVU HABA!.
Hata wewe Kanisani kwako, au kwa ndugu zako, Tenda Mazuri meengi, hata hayaonekani, lakini Ukifanya Baya Dogo tu, Lazima lionekane Kuliko Mazuri yako!!.
Ndio, maana kwenye taarifa za habari au humu kwenye Mitandao ya Kijamii,
Hukuti Habari za Kwamba, Mchungaji flani, amehubiri Watu kadhaa wameokoka au wameponywa Magonjwa,
Hukuti habari inasema Mtumishi flani amewaombea Watu watu wakajazwa na Roho Mtakatifu!.
Lakini, Utaona na Kusoma, kwamba Mchungaji amefumaniwa, mara Mchungaji Amewalawiti watoto,
Mara mtume akutwa kwa Mganga wa Kienyeji n.k!.
(Haijalishi walikua wanahubiri kwa kiwango gani)
Upumbavu haba, unavundisha Marhamu yote!.
Jua kwamba, Watu wanaweza wasitafute Kuiona MARHAMU yako, ili wakusifie, wapate Msaada, lakini wakatafuta UPUMBAVU haba ili kuivundisha MARHAMU yako.
Wakati wanamshitaki Yesu, pamoja na mazuri Mengi sana, aliyoyafanya bado walitafuta Baya kwake, ili Mazuri yake Yachafuke,
"Pilato akawaambia, Basi nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulubiwe. Akasema, kwani? Ni ubaya alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, wakisema, Na asulubiwe. Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lo lote, bali ghasia inamzidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe". MATHAYO 27:22-24
Lakini hawakuona, Pilato akagoma kutoa hukumu!.
Sasa hivi tunakuamini, na kukusikiliza, kwa sababu hatujalisikia Baya lako lolote,
Mfano, Ikatokea Umepewa/umempa Mtu mimba, na asiye Mme/Mke wako,
Na tukasikia, habari zikavuma,
Hatuta kusikiliza tena, wala kukuamini, kama wewe usivyowaamini ambao umesikia habari zao mbaya!!.
HICHO KITU CHA KIMUNGU ULICHONACHO, NDIO MARHAMU YAKO, ANGALIA MAINZI MAFU YASIVUNDISHE MARHAMU YAKO!!.
Shetani anatafuta sana, akukoseshe, ili Aivundishe Marhamu yako!,
Maombi yangu kwa Mungu, asikuweze, na asikupate!.
Naamini Umenielewa, Mungu akubariki Sana!.
TUMFILISI SHETANI 2016!
........Amen, amen........
By Mwalm Nick.
0712265856 (WhatsApp#)

Comments