MAANA 10 ZA NENO "KUOKOKA


Na Mtumishi Geoffrey Mwanza.
1. Kuokoka ni kuvunja urafiki wako na shetani na kuanza urafiki mpya na wa uhai na Yesu Kristo.

2. Kuokoka ni hamisho ya kiroho ndani ya moyo wa mtu kutoka kwa wafu hadi kwa walio hai.

3. Kuokoka ni kujichagulia uzima wa milele na kukataa nguvu za Jehanamu.

4. Kuokoka ni kujiandaa kwa ujio wa Bwana Yesu na kisha kutawala pamoja naye.

5. Kuokoka ni kujikatia tiketi ya kwenda mbinguni na kuiacha njia ya kuzimu.

6. Kuokoka ni kumwaibisha shetani nakumwinua Bwana Yesu.

7. Kuokoka ni kujitwalia uhuru wako na kumnyima shetani kuitawala himaya yako.

8. Kuokoka ni mwanzo wa kuabudu Mungu na kama hujakoka na unaenda Kanisani ujue bado hujaanza kuabudu pia bado haujajua kuabudu Mungu wa mbinguni.

9. Kuokoka ni kujichagulia mema na kuyakataa maovu.

10. Kuokoka ni kuwa hai na kama hujaokoka umekufa.

Ubarikiwe sana na kama hujaokoka uokoke sasa hivi kwani hauna tofauti na maiti.
By Mchungaji Geoffrey Mwanza. 

Tupigie simu kwa ushauri zaidi:
THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES
Geoffreymwanza@yahoo.com
+254724 656 653

Comments