MAOMBI YA KUNG'OA MIPAKA YA ADUI ZAKO KISHA WEWE KUMWEKEA ADUI MIPAKA.

Na Mtumishi Peter Mabula.
Bwana YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze kisha tuombe maombi ya vita.
Leo nataka tuombe tuking'oa mipaka yote ambayo adui zetu wametuwekea, Kisha tuweke mipaka sisi ili adui asivamie kwetu.

Iko mipaka ya MUNGU ambayo ni mipaka mizuri na ya ushindi kwetu lakini mawakala wa shetani nao huweka mipaka yao ili kutuzuia.

Ayubu 38:11 '' Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?''

Siku moja katika siku za karibuni ilikuwa ni zamu yangu kuomba ili kumaliza ibada ya mkesha. 
Katika maombi hayo nikasikia sauti ikisema hakikisheni mnang'oa mipaka yote ya adui.
Baadae baada ya kuomba juu ya kung'oa mipaka ya adui nikapata ufunuo mwingine ambao ulikuwa unasema kwamba tumwekee adui mipaka, ili baada ya kung'oa mipaka ya adui basi tuweke mipaka sisi ili adui asiingie ndani ya mipaka yetu.

Namshukuru sana Bwana YESU maana baadae nilipata maandiko mengi yanayofundisha juu ya kung'oa mipaka ya adui na jinsi ya kumwekea adui mipaka.
Kuna watu kwenye vitu fulani maishani mwao huwekewa mipaka na adui zao ili wasivuke mipaka hiyo.
Mipaka ni vikwazo ambavyo maadui zako wanaviweka ili kukuzuia.
Mipaka ni laana za kipepo ambazo zimewekwa ili kukuzuia.
Mipaka ni mipango ya adui zako ya kuhakikisha hufanikiwi kiasi unachokitaka.
Mipaka ni kizuizi katika jambo lako lolote.
Ngoja nikupe maandiko machache ili yakusaidie kujua na kuomba.

1 Thesalonike 2:18 ''wa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.''

Katika andiko hilo Biblia inaonyesha wazi kwamba shetani wakati mwingine anaweza kuwazuia wateule wa MUNGU katika mipango yao, Mtume Paulo alipanga kwenda kuhubiri katika mji fulani lakini mara mbili zote shetani alimzuia, maana yake shetani alimwekea mpaka mtumishi wa MUNGU ili asifanikiwe kuvuka kwenda kwenye kazi yake ya injili. Kizuizi kama hicho kinaweza kuwa katika maisha ya kila mtu, mipango yako ya mwaka huu inaweza kuzuiliwa na kama hutajua jinsi ya kung'oa mipaka hiyo ya adui hakika mwaka utaisha wewe ukiwa hivyo hivyo.

Isaya 42:22 '' Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.''

Kuna siri nzito sana katika andiko hilo la Isaya 42:22.
Kuna watu wameibiwa ufahamu , kuna watu wametekwa na mawakala wa shetani.
Kuna watu wamenaswa katika mitego ya shetani.
Kuna watu ndoa zao, kazi zao, masomo yao, familia zao au uchumba wao umenaswa katika mitego ya shetani.
Kuna watu wako katika mashimo maana yake wako katika kifungo cha shetani.
Kuna watu wamefichwa katika magereza ya magonjwa.
Kuna ndoa ziko gereza la mateso.
Kuna biashara za watu ziko katika gereza la kufilisika.

Ayubu 33:11 ''Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza.''

Hata maadui zako wanaweza kukupeleleza na kukuwekea mipaka.
Mkatale ni mti uliotumika kuwafunga watu ili wasitoroke.
Kuna watu shetani amewawekea mipaka ili wasifanikiwe kufikia malengo yao.
Leo tunang'oa mipaka yote ya kipepo kwa jina la YESU KRISTO.
Somo hili nilitaka liwe masomo mawili lakini siku hizi nafasi ninayo chache ya kuandika masomo ndio maana nataka hapa hapa somo lote likamilike.

Ayubu 14:4-5 '' Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;''

Mipaka ipo.
MUNGU anaweza kukuwekea mipaka mizuri lakini kama adui zako nao wanaweza kukuwekea mipaka ili usivuke nje ya mipango yao. mipango yao ni kuhakikisha hufanikiwi.

Ayubu 21:15 ''Sauti za utisho zi masikioni mwake; Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;''

Kuna watu wametekwa nyara.
Kuna watu ufahamu wao umetekwa, kuna watu uhusiano wao umetekwa na mtekaji amewawekea mipaka ili wasifanikiwe.
Sifa mojawapo ya mipaka ni kwamba yule aliyewekewa mipaka hawezi kuivuka mipaka hiyo hadi apate msaada wa kung'olewa mipaka hiyo. Nguvu pekee inayoweza kung'oa mipaka ya adui zako ni Damu ya YESU KRISTO na jina la YESU KRISTO.

Isaya 5:13 '' Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.''

Mateka huwa hawezi kuvuka mipaka ya watekaji.
ikiondolewa mipaka tu kwa aliyetekwa hakika anakuwa huru.
Kung'oa mipaka ni ushindi mkubwa sana.
Sijui ni jambo gani kila ukijaribu kulipata vinaibuka vikwazo.
Inawezekana kabisa una mchumba wako na mnapanga kila mwaka kwamba mtaoana lakini haijawezekana huu mwaka wa 3, hamjatenda dhambi na mnadumu katika utakatifu lakini kila kitu kinagoma. ndugu mnatakiwa kung'oa mipaka yote ambayo wachawi au waganga au watu wabaya wote wamewawekea, hakikisheni mnaiondoa mipaka hiyo kisha nyie ndio muweke mipaka kwa adui zenu, kuhakikisha hakuna adui anayeweza kuingilia mipango na baraka zenu zenu.
Inawezekana kabisa kuna ukuta mkubwa sana wa kuwatenganisha wanandoa, ndoa hiyo kila siku iko vitani, adui wamewawekea mipaka hivyo hakikisheni mnang'oa mipaka hiyo na nyie wekeni mipaka kwao ili kila adui akitaka kuingia katika baraka yako aharibikiwe yeye kwa jina la YESU KRISTO.

Maombi haya naomba yamsaidie muombaji mchanga ili yawe kianzio cha kuomba katika kulifikia hitaji lake halisi.
Kila mtu ana hitaji lake  hivyo ni muhimu sana kuombea hitaji lako, wewe ndio unajua unakozuiliwa hivyo pambana kwa jina la YESU KRISTO.
Utakatifu ni jambo la lazima kwa muombaji hivyo hakikisha unatubu na kuacha dhambi kisha omba maombi haya ya vita na BWANA atakushindia.

Maombi ya Kung'oa mipaka ya adui zako.

ROHO wa MUNGU pokea sifa milele.
Ninakushukuru BWANA kwa uzima na ulinzi wako kwako.
Nakushukuru ROHO MTAKATIFU maana umetaka nilijue jambo hili na ili niombe na kushinda.
Kwa jina la YESU KRISTO niko kinyume na kila adui zangu kwenye ulimwengu wa roho, niko kinyume na walionilaani, niko kinyume na wanaoniroga na niko kinyume na roho zote za kishetani, niko kinyume kwa jina la YESU KRISTO. Ninaharibu kila mpango wa shetani na ninaangamiza kwa damu ya YESU KRISRO kila mpango wa wachawi.
Kila mipaka ambayo nimewekewa na wachawi ili nisioe/ nisiolewe, ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekewa katika masomo yangu ili nisifaulu,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekewa ndoa yangu isiwe na maelewano wala masikilizano,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekewa ili akaunti yangu ikae bila pesa siku zote, ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekewa na wachawi ili nisikue kiroho,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekea ili mimi niwe mtu wa dhambi siku zote,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niyowekewa ili niwe wa kufukuzwa kazi kila siku,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekea ili kila siku niwe wa kufeli,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekewa ili nisizae,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekewa ili nisipate mchumba,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niyoyowekewa ilikila siku nikosane na ndugu zangu,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila mipaka niliyowekewa ili kila mara niwe  mchafu,ninang'oa mipaka hiyo kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Katika jina la YESU KRISTO ninatanganza ushindi sasa baada ya miaka yote ya shetani na mawakala wake kuong'olewa.
Asante BWANA YESU kwa kunishindia.
Nakushukuru MUNGU BABA maana katika wewe uko ushindi na uzima.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea.
Amen Amen.


 Baada ya kung'oa mipaka yote ambayo adui waliweka kwako, hakikisha unawawekea adui zako hao mipaka ili asitokee adui wa kuingia katika mipaka yako.

 Maombi ya kuwawekea mipaka adui zako.

Katika jina la YESU KRISTO ninawawekea mipaka adui zangu wote ili wasiingilie wokovu wangu, mipango yangu  na maisha yangu.
Neno la MUNGU linasema katika Zakaria 2:5 kwamba 
'' asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.''
Damu ya YESU ikawe sasa ukuta wa moto ili kuwazuia adui zangu kuingia mipango yangu ya mwaka huu.
Damu ya YESU ikawe sasa ukuta wa moto ili kuwazuia wachawi wote kuingia afya yangu na familia yangu.
Damu ya YESU ikawe sasa ukuta wa moto ili kuzuia kila kila roho ya shetani kuingia maisha yangu.
Naweka mipaka katika mipango yangu ili adui yeyote asiivuruge wala kuiharibu mipango yangu, ninaweka mipaka kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ninaweka mipaka ya damu ya YESU katika ufahamu wangu ili adui asivamie ufahamu wangu, ninaweka mipaka kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
ninaweka mipaka kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Biashara yangu naiwekea mipaka ya damu ya YESU ili wanaoiba pesa kichawi wasiibe tena, ninaweka mipaka kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Ninaweka mipaka ya damu ya YESU katika ndoa yangu na familia yangu, sitaki adui waingilie ndoa yangui na familia yangu, ninaweka mipaka kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Nakushuru BWANA maana mipaka niliyoiweka katika mipango yangu, ndoa yangu, uchumba wangu na kila jambo langu hakuna adui atakayeiingilia,   ninaweka mipaka kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Asante MUNGU BABA kwa kunipa ushindi.
Ni katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi.
Amen Amen.

 
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili


Comments