JE UNAONA NINI NDUGU?

Na Mtumishi Peter Mabula


BWANA YESU atukuzwe.
karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Je unaona nini?

Yeremia 1:11-12 ''Tena neno la BWANA likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi. Ndipo BWANA akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize. ''

Yeremia wa leo ni wewe, je unaona nini?
Mwaka huu unaona nini?
Kwenye huduma yako unaona nini?
Kwenye ugonjwa ulionao unaona nini? Unaona kupona au unaona kufa?





Zaburi 103:3-5 '' Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema, Aushibisha mema uzee wako, Ujana wako ukarejezwa kama tai; Kwenye masomo yako unaona nini? Unaona kufaulu au kufeli?Kwenye ndoa yako yenye mgogoro unaona nini? Unaona laka au unaona ushindi?

MUNGU anapanga mambo mengi mazuri juu yako, je unayaona hayo mema ambayo BWANA anataka kukupa?
ukiyajua yaliyo mema  kutoka kwa MUNGU na ukaomba kwake ili kuyapata hayo hakika utapokea. tatizo ni watu wengi kuona matatizo badala ya ushindi.
kama moyo wako unaona mataktizo tu na unayakiri hayo kila siku hakika matatizo hayo yatakuwa sehemu ya maisha yako.
kama unasema kila siku mimi ni wa hivihivi hakika utakuwa wa hivyo hivyo.



Nabii Yeremia alipoulizwa anaona nini alisema anaona ufito wa Mlozi.
Ufito ni fimbo na fimbo kwenye lugha ya rohoni ni Neno la MUNGU, Ndio maana jibu la MUNGU likaja kwa Yeremia kusema ameona vyema maana ameona Neno na Neno hilo kwa sababu ni la MUNGU basi MUNGU huliangalia Neno lake ili alitimize.

Je wewe ndugu yangu unaona nini katika maisha yako?
Wakati Mwingine MUNGU hawezi kukubariki kitu usichokiona, hivyo unatakiwa uone.
Biblia inaweza kukufanya uone vyema.
Kuenenda na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU huko ndiko kuona jambo sahihi.

Ninachoweza kukushauri ni kwamba;
Ukitaka BWANA YESU atende kwako basi na wewe tenda ya kwake. Ya BWANA YESU ambayo unatakiwa kuyatenda ni kumtumikia, kumkiri popote uliko, kuishi maisha matakatifu na kulitii Neno lake siku zote.


Inawezekana uko katika maumivu makubwa, inawezekana kabisa unaumwa na unajua tu kwamba utakufa wiki hii lakini naomba nikueleze kwamba MUNGU BABA hajashindwa kukuponya na ukiamua kuomba kwake hakika utapona.
ukiendelea kukiri kifo hakika utakufa.
Ayubu alikuwa katika wakati mgumu kuliko wewe lakini hakukiri mabaya bali alimwamini MUNGU na alijua kwamba Mtetezi wake YESU KRISTO yuko hai na atamtetea tu.
chukulia wewe unaumwa na hata tumaini limeondoka lakini ukimkumbuka MUNGU kwamba ana nguvu zote unapata tumaini kwamba ukimuomba atakusikia na kukuponya. Kisha unaomba na baada ya muda mfupi unapona hakika utamtukuza MUNGU.
Ayubu alikuwa katika kilele cha maumivu ya kuumwa na kuteseka lakini alisema neno hilo kabla ya kupona '' Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona MUNGU; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu.-Ayubu 19:25-27'' 

Ayubu alikuwa anaumwa lakini alikiri ushindi wa MUNGU na aliamini kwamba atapona.
Wewe mtu wa MUNGU unatakiwa uwe na tabia ya kumwamini BWANA hata kama uko katika mazingira magumu.
MUNGU anasikia maombi maana kama aliweza kusikia maombi ya Nabii Yona akiwa ndani ya tumbo la nyangumi katikati ya bahari, je atashindwa kusikia maombi yako?
Ndugu omba kwa utulivu.
usikubali tatizo lolote likuondoe katika kumwamini na kumtegemea BWANA YESU.
Je baada ya kusoma ujumbe huu unaona nini?
Je umeanza kuona uzma?
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments