BWANA YESU HUWA HAWI KWENYE SANAMU HATA SIKU MOJA.


Na Peter M Mabula.Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.


BWANA YESU KRISTO atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la MUNGU. 
Leo nina ujumbe mzuri na mtamu sana na ujumbe huu unakuhitaji tu wewe kubadilika kuanzia ufahamu wako hadi matendo yako.
BWANA YESU hajawahi kukaa katika sanamu  wala picha iwayo yoyote, hilo ndio jambo muhimu la kwanza nataka tujue.

BWANA anasema katika Isaya 42:8 kwamba ''Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. ''

BWANA hajawahi kukaa katika sanamu na wala hawezi na hajawahi kuwapa sanamu sifa zake na kwa andiko hilo tu inatosha kabisa kwamba wanaoomba sanamu au kuzisujudia sanamu au picha ambazo wao husema ni za YESU hao wanakuwa wametekwa fahamu zao na shetani.
Matendo  17:29 ''Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa MUNGU, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.'' 
 
Tangu Mwanzo wa Biblia hadi Mwisho sanamu inakatazwa kwa vyovyote kuhusika na kanisa la MUNGU. YESU wetu hakaagi kwenye picha.
kama wewe yesu wako yuko kwenye picha au sanamu nakupa pole sana maana huyo sio YESU ila ni sanamu yako tu isiyo na  faida hata moja.
BWANA YESU anakaaga katika mioyo yetu wateule wake na sio kwenye picha wala sanamu ndivyo maandiko yasemwavyo.
Waefeso 3:17-19 ''  KRISTO akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina;na kuujua upendo wake KRISTO, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa MUNGU.''

-Andiko linasema ''KRISTO akae mioyoni mwenu'' sasa huyu Kristo anayekaa katika sanamu ni yupi huyo? 
Kristo wa kwenye picha kubwa ambazo watu hubandika vyumbani mwao na kuzisujudia ni wa wapi?
Ndugu zangu naomba utambue kwamba YESU KRISTO hakaagi katika picha bali moyoni. Na BWANA YESU atakuja moyoni mwako siku ukiamua kumpokea kama BWANA na MWOKOZI wako.

1 Thesalonike 1:9-10 ''Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia MUNGU mkaziacha sanamu, ili kumtumikia MUNGU aliye hai, wa kweli; na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja. '' 
 
Mtu hawi mtakatifu kwa sababu anajitangaza kwamba yeye ni mtakatifu, bali mtu anakuwa mtakatifu kwa kupokea Wokovu wa KRISTO na kisha anajitenga na maovu ya dunia.
Kuna watu wametekwa na sanamu kiasi kwamba huziabudu.
Kuna watu hata hawajawahi kumuomba MUNGU bali huziomba sanamu na kulia mbele za sanamu wakihitaji msaada.
Kuabudu wanadamu ni kuabudu sana.
Kuabudu sanamu ni kuabudu chochote kilicho nje na utatu wa MUNGU.

1 Kor 10:14-15 ''Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu. Nasema kama na watu wenye akili; lifikirini ninyi ninenalo. '' 
 
shetani amewaziba masikio maelfu ya watu kiasi kwamba wanaona ni jambo dogo kusujudia mawe, miti au sanamu.
MUNGU ametuumba wanadamu ili tumwabudu.
MUNGU hajawahi kuwa kwenye jiwe wala hajawahi kuwa kwenye sanamu iwayo yoyoe hivyo kama kuna mtu anamwabudu MUNGU kupitia jiwe au sanamu huyo anakosea sana maana sanamu yake hiyo ni machukizo kwa MUNGU.

1 Yohana 5:21 ''Watoto wadogo, jilindeni nafsi zenu na sanamu. ''
 
Ni makosa makubwa kutumainia sanamu.
Mzee mmoja aliwapiga hadi kuwafukuza watoto wake na mke wake kwa sababu tu waliihamisha chumbani sanamu ambayo yule mzee alikuwa anaibabudu akisemahuyo ni mariamu mama wa Mungu.
Ndugu zangu hada kumwabudu mariam ni makosa makubwa sana mbele za MUNGU.
Walioanzisha kuabudu wanadamu akiwemo Mariam Biblia inasema hivi juu yao; '' Kwa maana waliibadili kweli ya MUNGU kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.-Warumi 1:25''
Kumwabudu Mariam ni kuabudu shetani.
Kumuomba Mariamu lolote ni kuonyesha tu kwamba wewe umepishana na kusudi la MUNGU juu ya uzima wa milele.
Mwanadamu yeyote akitaka ROHO MTAKATIFU aingie ndani yake ni lazima kwanza mwanadamu huyo aachanae na sanamu zote.
Ukitaka MUNGU awe anasema na wewe hakikisha unajitenga na sanamu.
Zaburi 115:3-8 '' Lakini MUNGU wetu yuko mbinguni, Alitakalo lote amelitenda.  Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu,  Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake.  Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia. '' 
 
Ukitaka MUNGU akutumie hakikisha unaikimbia ibada ya sanamu.
Ukitaka ukubaliwe na mbingu hakikisha huabudu sanamu.
Waisraeli wakati wakitoka Misri MUNGU aliwaagiza kuzivunja kila sanamu za wanadamu katika Eneo ambalo waisraeli walipita.
Sanamu zile kwenye ambazo kwa jina jingine zinaitwa ashera zilitakiwa kuvunjwa maana ni machukizo kwa MUNGU.

 Kumbu 7:5 '' Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.''

Ndugu yangu najua unaupenda uzima wa milele.
Ninachopenda kukuambia ni kwamba hakuna mwabudu sanamu hata mmoja atakeingia uzima wa milele.
BWANA YESU anasema;  ''Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa MUNGU wake, naye atakuwa mwanangu. Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.- Ufunuo 21:7-8 ''

Haijalishi unaiabudu sanamu unayodhani wewe ni ya Yesu au Mariamu lakini ukweli ni kwamba waabudu sanamu wote makazi yao ni katika ziwa la moto na sio mbinguni.
Ndugu najua kwa baadhi ya watu ni ngumu kuziacha sanamu lakini kama unaupenda uzima wa milele nakusihi ndugu achana na sanamu na anza kumwabudu MUNGU BABA katika Roho na kweli.
 
Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments