MAOMBI YA KUMUOMBA MUNGU ILI AFANYE JAMBO JIPYA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU na kisha tuombe maombi ya ushindi sana.
Leo tunamuomba MUNGU afanye jambo jipya katika maisha yetu.
Kama magonjwa yalitutawala leo MUNGU BABA anafanya jambo jipya kwa kuleta uponya wake.
Isaya 43:19 ''Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.''

 MUNGU wetu anaenda kufanya jambo jipya, Hata baraka ambazo tuliziona haziwezekani kwetu leo kwa maombi yetu kupitia jina la YESU KRISTO tunaenda kufanikiwa.
Kwanini MUNGU afanye jambo jipya?
Ni kwa sababu '' hakuna neno lisilowezekana kwa MUNGU.-Luka 1:37''

Kwanini JEHOVAJ MUNGU wetu atende jambo jipya?
Yeye MUNGU anakuuliza wewe akisema;
 ''Tazama, mimi ni BWANA, MUNGU wa wote wenye mwili; je! Kuna neno gumu lo lote nisiloliweza? -Yeremia 32:27 ''
Kwa sababu MUNGU wetu anaweza yote basi hakika kwa maombi yako ya imnai na utakatifu kupitia jina la YESU KRISTO anaenda kufanya jambo jipya kwako ambalo ulidhani haliwezekani.

 Kwanini MUNGU afanye jambo jipya?
Ni kwa sababu yeye yuko juu ya vyote na juu ya wote.
Biblia inamthibitisha MUNGU wetu kwamba;
''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.-Zaburi 83:18''
Kama aliponya magonjwa yote;Mathayo 9:35 ''Naye YESU alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri habari njema ya ufalme, NA KUPONYA MAGONJWA YOTE  na udhaifu wa kila aina.''
Sio kwamba aliponya magonjwa fulani tu bali magonjwa yote.
Unateswa na kaugonjwa gani hata usipone?
Ukimwamini BWANA YESU na ukampokea na kuanza kuishi maisha matakatifu hakika uponya utakuwa mali yako hata kama ulidhani hutapona.
Kama aliponya magonjwa yote atashindwa nini kutengeneza jambo jipya kwako?
Mimi Peter Mabula juzi Nilikuwa namuombea rafiki yangu mmoja kwa simu kutokea Kilimanjaro ndipo niliposikia sauti ya ROHO MTAKATIFU ikisema kwamba niombe  juu ya MUNGU kutenda jambo jipya kisha akanipa ujumbe huu ili nikufundishe wewe na uombe maombi ya ushindi ukiliendea hitaji lako.
Siku hiyo kwa simu kwa muda wa masaa mawili kamili niliombea watu wengi na wengine katika hao walinishuhudia usiku ule ule kile ambacho MUNGU ametenda katika mahitaji yao waliyonishirikisha.
Hakika MUNGU alifanya jambo jipya katika afya zao na katika mahitaji mengine.
Ni kweli mama yangu umeteseka sana na magonjwa lakini jambo jipya atakalolifanya BWANA YESU kwako ni kukupa uponyaji.
Hayo magonjwa uliyoyaona tangu miaka mingi hutayaona tena yakiwa katika mwili wako. Mwamini tu BWANA YESU na Neno lake na hakikisha huigizi kwa MUNGU bali umeamua kabisa kuishi maisha matakatifu katika BWANA YESU.
Ni kweli umekuwa tasa muda mrefu sana sana JEHOVAH mwenye nguvu anaenda kukubariki uzao.
Ulidhani tumbo lako halitatoa mtoto na hadi mumeo akawa anakujeruhi kwa maneno yake, lakini wakati huu BWANA anaenda kutenda jambo jipya kwa kuwabariki uzao uliobarikiwa.
 Ni kweli familia yenu imekuwa na matatizo mengi sana lakini kwa maombi yako ya leo kupitia damu ya YESU KRISTO na jina la YESU KRISTO, MUNGU BABA anaenda kufanya jambo jipya kwa kuwapa ushindi, furaha na amani.
Inawezekana kabisa kila mwaka katika ukoo wenu mnazika, hadi  wakati huu mmeanza kufikiri ni zamu ya nani kufa mwaka huu. Habari njema ni kwamba BWANA YESU kupitia maombi yako anaenda kufanya jambo jipya la kuondoa vifo visivyo mpango wa MUNGU. Mtatimiza miaka ya ahadi kwa jina la YESU KRISTO.
Kufa tutakufa wote lakini sio kufa kwa mpango wa shetani na mawakala wake, leo omba utashinda hakika kwa jina la YESU KRISTO.
Kama aliumba mbingu  na dunia kama inavyosema Biblia;
 Mwanzo 1:1 '' Hapo mwanzo MUNGU aliziumba mbingu na nchi.'
Je atashindwa nini kukuponya hako ka ugonjwa kanakokusumbua? Leo omba hakika utashinda.
Unaweza pia kuomba maombi ya kufunga kabisa ukiomba maombi ya ufunuo huu wa kumwambia MUNGU atende jambo jipya, hakika utashinda.
Kama wachumba wanakuacha kila ukipata, hakika wakati huu utapata mchumba na utafunga ndoa kanisani, omba tu na dumisha utakatifu.
Kama watu wote wanajua kwamba wewe haiwezekani kuolewa, hakika wakati huu utaolewa na utazaa watoto wa kiume na wa kike kwa utukufu wa MUNGU.
Kama watu wanadhani hutapata kazi hakika kupitia ufunuo huu dai kazi yako kwa MUNGU na utapata kazi hiyo, mkumbuke tu MUNGU kupitia kazi hiyo atakayokubariki.
Wanaopanga ufukuzwe kazi, watafukuzwa wao baada ya kuomba maombi haya ya ufunuo huu wa kumwambia MUNGU afanye jambo jipya katika kazi yako.
MUNGU BABA anasema leo kwamba;
''Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.   -Yeremia 29:12''
 BWANA wa majeshi leo anaenda kufanya jambo jipya kupitia maombi yako katika KRISTO YESU.
Mambo haya matatu yazingatie.
3-Utakatifu tu ndilo jambo muhimu kwako kuanzia leo.
 2-Wokovu wa KRISTO tu ndilo jambo special utakalotakiwa kulishika siku zote.
3-Kuomba kwa imani katika KRISTO leo kutafanya jambo jipya kwako.
Kama wachawi hawajawahi kukukimbia leo watakimbia wote kwa jina la YESU KRISTO.
Ni kweli mama umeteseka miaka mingi katika ndoa yako, lakini BWANA YESU anaenda kutenda jambo jipya la kukupa furaha ya kudumu.
 Ni kweli ndugu yangu umeteseka sana na magonjwa  lakini leo BWANA YESU anaenda kufanya jambo jipya .
Kama kwa miaka mingi watu walikuona wahivi hivi, leo hutakuwa wa hivi hivi bali utakuwa mbarikiwa.
MUNGU akubariki sana  na mchango wa kuchapisha vitabu bado nakusanya, ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari nakuomba usiache kunitumia katika namba yangu ya 0714252292, jina PETER MABULA, namba hiyo iko mwishoni mwa kila somo langu na katika Blog yangu ya Maisha ya ushindi, utaona masomo yangu 520 ambayo yote yana namba hiyo chini kabisa mwa somo.
MUNGU wa mbinguni akubariki sana na leo sitakuandikia maombi ya kukuongoza  maana nimejulishwa kwamba kuna watu watashindwa kuliombea hitaji lao halisi linalotakiwa kufanyiwa jambo jipya ila naamini kwa maelekezo ya somo hili utakuwa umeshajua ni katika jambo gani kwako unahitaji MUNGU afanye  jambo jipya la kukupa ushindi wewe. Kwa sababu MUNGU atakutendea kupitia maombi yako ambayo utayaomba kwa kufuata maelekezo ya somo hili, naomba usiache kunipa ushuhuda wa kile atakachokutendea BWANA YESU baada ya kujibiwa. Na mimi nawaombea wote watakaoomba kupitoa ufunuo huu ambao ROHO wa MUNGU ametupa mimi na wewe.
Unaweza kunishuhudia kile MUNGU alichokutendea kupitia.
Email: Mabula1986@gmail.com.
Facebook inbox: Peter M Mabula.
au kwa namba yangu ambayo ni 0714252292.
MUNGU yule ambaye mbingu ni zake akubariki sana sana.
Amen Amen.
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili


Comments