ILI NDOA YAKO IDUMU FANYA YAFUATAYO

KUMTEGEMEA MUNGU KWA WANANDOA NI JAMBO JEMA SANA NA NDOA SAHIHI YA KIMUNGU NI YA MKE 1 KWA MME 1

Wanandoa fulani wazee walinipa siri ya kudumu kwa ndoa yao mpaka leo, waliniambia mambo makuu 5:

1. Wanamtanguliza Mungu katika mambo yao yote.

2. Kila mmoja amemsoma mwenzake na anajua anachopenda na asichopenda. Wakasema mwanzoni ilikua ngumu kwa sababu  mmoja ndo aliamua kujitoa kwa ajili ya mwenzake, lakini baada ya muda wote wakajikuta wanaelewana.
3. Mume akisema labda ana njaa au amechoka, mke a

tajishughulisha haraka sana kuhakikisha mumewe amekula au amepata anachohitaji kwa wakati ule. Vivyo hivyo, akisema ana njaa au amechoka mume atajishughulisha mpaka ahakikishe mke amekula na kupumzika. Wakasema hii haina kutegeana, wala kulalamika.

4. Mmojawapo akitoa wazo mwenzake halipingi moja kwa moja, hata kama hilo wazo sio zuri, anamsikiliza mwanzo mpaka mwisho, alafu anamwambia unaonaje tukiliboresha namna hii na hii? wanakubaliana na kutekeleza.

5. Mmojawapo akimletea mwenzake zawadi, hata kama hakuipenda anaipokea kwa furaha na shukrani, anachoangalia ni thamani ya ule upendo, sio thamani ya zawadi.

KAMA WATOTO WA MUNGU MLIOOKOKA NI MUHIMU KUWA NA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA NDOA YENU NA FAMILIA YENU PIA

{MUNGU AKUBARIKI SANA NA KAMA HUJAMPA YESU MAISHA YAKO KUMBUKA NDUGU WAKATI WA WOKOVU NI SASA NA WAKATI WA KUTENGENEZA MAISHA YA UZIMA WA MILELE NI SASA HIVYO CHUKUA HATUA}

Comments