NIMEPONA MARA 2 KWA NJIA YA KUSIKILIZA NENO LA MUNGU RADIONI


Shalom watu wa MUNGU na ni jambo la kumshukuru MUNGU baba yetu wa mbinguni kwa neema yake ya uzima maana amependa tuwe hai ndio maana tuko hai. katika maisha yangu nimekutana na mambo mengi sana na kama kuna mtu ana shuhuda ambazo JEHOVAH MUNGU ametenda kwake basi na mimi ni mmoja katika hao na hata hivyo naamini kila mtu ana ushuhuda maana hata kuwa hai tu ni ushuhuda tosha na pia hongera sana wewe unaetoa ushuhuda maana kwa kufanya hivyo unamwaibisha shetani na wapambe wake na unamtukuza MUNGU aliyekutendea muujiza huo. Katika maisha yangu ya kabla ya kuokoka na baada ya kuokoka kuna matukio mawili ambayo MUNGU alinitendea muujiza kwa njia ya radio yaani kusikiliza radio na leo napenda kukushirikisha, Mwaka 2003 nikiwa nasoma  Biharamulo sec school nikiwa form two kuna siku moja  sikumbuki ilikua siku gani lakini ilikua mwezi wa 10, shule yetu ilikua ni ya boarding hivyo tulikua haturuhusiwi kutoka ,   nilitoroka shuleni asubuhi na kwenda kutembea madukani maana maduka yako mbali na shule na huko madukani nilinunua biscuits pakti 1 ya Tsh 200 na wakati wa kurudi nilirudi huku nakula njiani na kwa sababu ya kutoroka nililazimika kuzunguka njia ya mbali porini ili nisionwe na walimu  na katika kuzunguka huko nilijikuta naumwa tumbo  ghafla baada tu ya kumaliza kula ile pakti ya biskuti  na maumivu niliyoyapata siku hiyo sijawahi kuumwa tumbo kama siku hiyo maana nilishidwa hadi kutembea na tumboni kulikua kama kuna wembe unakataa hivyo kulazimika kukaa eneo hilo hilo kwa masaa 7 kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni  kwa muda huo wote nlikua tu nalia na kutapika sana ikafika kipindi nikanza hadi kutapika damu ilipofika saa 10 nilitembea huku nimeinama hadi barabarani na rafiki yangu mmoja Paschal Venance ambaye sasa ni mwalimu akaniona pale barabarani na kunibeba hadi bwenini na nilipofika nilitulia tu kitandani maana hata kuongea vizuri sikuweza na wanafunzi wenzangu walinizunguka na kushangaa kwa hali niliyokua nayo niliogopa kwenda hospital maana niliogopa walimu hasa second master aliyekua mkali sana na nililala ili nitoe taarifa kesho yake ndipo niende hospital maana siku hiyo nilikua nimetafutwa sana na mwl mmoja nikajipumzisha huku nasikiliza kituo cha RADIO FREE AFRICA cha Mwanza na ilipofika saa 12 jioni kilianza kipindi cha mahubiri na alikua ana hubiri Mwl Chritopher Mwakasege nilisikiliza kwa muda kama dk 45 akaanza kuombea  na alipotamka kuwa kama kuna mtu anaumwa majumbani ashike sehemu anayoumwa na mkono mmoja ashike radio nilifanya hivyo na aliombea kama dk moja tu lakini alipoanza tu kuomba nilisikia tumbo likiunguruma na alipomaliza kuombea alisema umepona na unawzeza kusimama na kujigeuza geuza na kujiangalia sehemu uliyokua unaumwa nilisimama na kushangaa nimepona maana nguvu zangu zilirudi zote na tangu muda huo nikapona nilimshukuru MUNGU sana kwa maombezi yale ya radio ambayo yalisababisha kupona muda huohuo na hadi leo naami ni kuwa ile biskuti ilikua na sumu ila MUNGU akanihurumia tu na kuniponya kupitia maombezi ya radio na tukio la pili ambalo lilitokea kwa njia ya kusikiliza radio ni mwaka 2011 nikiwa zanzibar nilikua nakabiliwa na wakati mgumu sana kwa kila kitu kuanzia kazini , nyumbani na kwa ndugu pia na siku hiyo nilikua nimefunga  maombi ya siku mbili na kwa muda huo wote wa maombi nilikua naomba na kichoka nasoma BIBLIA na nikichoka pia kusoma Biblia naimba tenzi za rohoni au nyimbo tu zozote za injili na pia kichoka nasikiliza RADIO WAPO FM na ilipofika saa 4 usiku nilichoka na kulala na ilipofika saa 7 nilijikuta nashtuka na kuanza kusikiliza Radio na kulikua na mcungaji mmoja anaitwa Michael Peter Nguru alikua anafundisha Radio Wapo somo fulani na niliendelea kusikiliza na katika hali ya kushangaza yule mchungaji wa radioni alinitaja jina akisema ''KUNA NDUGU MMOJA UKO ZANZIBAR JINA LAKO PETER MICHAEL MABULA  NA UNANISIKILIZA MUDA HUU SAA 8 NA DK 13 NINA NENO KWAKO KUTOKA KWA BWANA, BWANA ANASEMA SONGA MBELE  NA AMEGEUZA UTEKA WOTE WA ADUI NA KUANZIA SASA UTAKUA MSHINDI'' Nilishtuka sana na kujaa hofu nyingi sana kusikia jina langu na la baba na babu likitanjwa radioni tena saa 8 usiku lakini baada ya muda nilikua na amani na kufurahi sana na nikashangaa sana kwamba MUNGU anaweza kutumia njia yeyote usiyodhani ili kukufikishia ujumbe wake na kweli niliona majibu mazuri sana. Na kwa matukio haya mawili ya radio namtukuza MUNGU sana lile la RADIO FREE AFRICA mwaka 2002 na hili jingine la WAPO FM la 2011. MUNGU awabariki sana

Comments