MUNGU NDIYE ANAYEJUA NJIA YA KUKUPITSHA KUELEKEA MAFANIKIO YAKO. (sehemu ya pili)

na Mwl Nickson Mabena


Kutoka 13:17-18a.

...Hebu tuendelee na somo letu;

asilimia kubwa sana ya watu, wanataka kufikia mafanikio ila wanashindwa kujua kwamba zipo njia za kupitia kufikia mafanikio;

safari zote Yesu ndiye aujuaye mwisho wake, yeye ndiye anayejua ni njia ipi akupitishe ili akufikishe alipokusudia ufike.

Ukichagua njia ya kupita mwenyewe, mwisho wako utakuwa mbaya sana hata kama sasa unaona mafanikio.
Kwa sababu hiyo kuna watu wengi sana, wanatamani watoke kwenye ndoa zao, wanajuta hata kwa nini walioa/waliolewa, kwa sababu walijichagulia njia waliyoiona wao kuwa ni sahihi katika kumpata mke/mume.

HEBU TUANGALIE MIFANO KADHAA KATIKA BIBLIA;

Esta; Binti huyu kabla hajawa malkia, alilelewa na Mjomba wake baada ya wazazi wake wote kufariki, alikuwa ni yatima!
najua kpoteza wazazi wote inauma sana, lakini ndiyo ilikuwa njia ya Mungu kumuadaa ili awe malikia, kama vile haitoshi. Mjomba ake Esta ajulikanaye kwa jina la Mordekai alichukuliwa mateka (Esta 2:5,6)

kwa hiyo Esta alikubali kwanza kukaa utumwani, maisha ya kitmwa hayakuwa mazuri, ila ilibidi akubaliane nayo kwani MUNGU ALIKUWA ANAMUANDAA ili awe malkia,
sijui kingetokea nini endapo angegoma kukaa na mjommba wake utumwani; nafikiri asingekuwa malikia, kwa hiyo kukubali kwake kukaa utumwani, huku akiwa mjane kulimfanya awe Malikia.

Ndugu yangu, wapo watu wengi wanatamani kuishi maisha ya kimalikia lakini kamwe hawataki kupitia UYATIMA, UTUMWA, au changamoto ambazo Mungu anataka wapitie; na kwa sababu hiyo hujichagulia njia zao na mwisho wao huwa mbaya sana.
isiwe hivyo kwako, watu wanaweza kukuona usiyefaa sasa, ila Mungu anakuangalia kivingine kabisa.

Daudi; Kabla hajawa mfalme, alikuwa mchunga kondoo... kabla hajawa mfalme ilibidi akutane na Goliathi kwanza,

Usitamani kuwa mfalme kama hutaki kuchunga kondoo, au kupambana na Goliathi wa maisha yako.

Ndugu, Mungu anaangalia mwisho wako......

Comments