MAMBO 4 AMBAYO MUNGU ALITAKA UYAJUE KATIKA MWAKA 2013



1.WEWE NI MWENYE DHAMBI:''Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa MUNGU'' Warumi 3:23. 



2.DHAMBI ZAKO ZIMEKUTENGA NA MUNGU; ''Lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone'' Isaya 59:2. 



3.MUNGU AMEKULETEA NJIA YA WOKOVU;''Kwa maana KRISTO naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili ya wasio haki, ili atulete kwa MUNGU'' 1Petro 3:18. 



4.WOKOVU WA MUNGU NI BURE KWA AJILI YAKO; ''Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele'' Yohana 3:16. 


MUNGU AKUBARIKI SANA NDUGU ULIYEFANIKIWA KATIKA KILE AMBACHO MUNGU ALITAKA UKIJUE 2013 YAANI KUMPOKEA BWANA YESU KAMA BWANA NA MWOKOZI WAKO NA KWA YULE AMBAYE BADO HUJATIMIZA KUSUDI LA MUNGU KWAKO LA MWAKA 2013, BADO HUJACHELEWA ,CHUKUA HATUA. YA KUMPOKEA YESU LEO NA MUNGU ATAKUBARIKI SANA.


Ni mimi ndugu yako katika BWANA YESU,


Peter Michael Mabula.


Maisha ya Ushindi Ministry.

Comments