MUELEZE YESU SHIDA YAKO BILA KUPINDISHA MANENO.


BY SNP KING G MWANGASA
Yohana-5:14-15
14 Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.

Na Pastor G Mwangasa Ufufuo na uzima Moshi,
Swala siyo una shida gani? Bali je! upo tayari kuponywa na Bwana Yesu.Ili upate upendeleo wa ki MUNGU ni lazima uwaachilie watu wote waliowahi kuujeru na kuumiza Moyo wako na uanze ku,Usafisha moyo wako na kuutakasa kwa Damu ya thamani ya Yesu Kristo.
Thamani ya maisha ya mwanadamu awaye yote yule ipo mikononi mwa Yesu na wala sio mikononi mwa wanadamu.Ukiwashikilia wanadamu ndani ya moyo wako hauwezi kufika mbali kabisa.
Warumi->6:22-23
Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Kuna makosa ambayo mtu aweza kuyafanya pasipo kufahamu kwamba anafungua mlango wa mashetani kwenye maisha yake pamoja na kizazi chake.

Na mashetani hao wakiingia ndani ya mtu wanageuka na kuvaa sura ya walinzi wa kiroho, Maana yake wanaanza kukulinda ndani ya balaa,mikosi,laana,hasara kwenye biashara nk.
Yule mtu alikuwa amepooza maana yake ameganda sehemu moja na kwenye maish ya mtu kuna,Mgando wa kiroho ambao unayafanya maisha ya mtu kutokupiga hatua ya namna yeyote,Yamkini umeshaanza kuuona mgando wa namna hiyo kwenye maish yako,Jambo moja la kufahamu ni kwamba yawezekana ulitenda dhambi au wazazi wako,Ukawaruhusu mashetani kuingia ndani yako na kuanza kukutesa.
Bali ashukuriwe Mungu kwa maana yeye yupo tayari kuichukua aibu yako,na akikusamehe hawezi kukumbuka kabisa.
Isaya->43:26
26 Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Mahali popote ulipo.Shirikiana na nyumba ya ufufuo na uzima moshi kumuomba,Mungu msamaha kwa dhambi zote walizotenda wazazi wako au wewe mwenyewe na endelea kubatilisha agano lolote la kishetani lililowahi kufanyika kwenye maisha yako,anza kusimamisha agano jipya la damu ya mwanakondoo kwenye maisha yako.


Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments