Gospel Hip Hop wamwita Msama


1
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama,


WAIMBAJI wa miondoko ya muziki wa Injili wa kufokafoka ‘Gospel Hip Hop’ wametoa wito kwa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, kuelekeza nguvu zake katika miondoko hiyo.
Kwa mujibu wa mwimbaji wa nyimbo hizo, Faraja Kampambe ‘Hurukweli’, Msama ni mfano wa kuigwa katika muziki wa Injili ambao unafikisha ujumbe wa Neno la Mungu kwa Jamii.
Hurukweli alisema, Msama anatakiwa kugeukia miondoko hiyo ili kupata ladha tofauti ya ufikishaji wa huduma ya Neno la Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje.
Aidha, Hurukweli alisema wakati akimuomba Msama aelekeze nguvu kwenye miondoko hiyo, hivi sasa amekamilisha albamu ya nyimbo nane alizorekodi katika Studio ya K Production ya Tabata na Pantu iliyoko Sinza jijini Dar es Salaam.
Hurukweli anaitaja albamu hiyo kuwa ni ‘Kila Mwenye Pumzi’, ikiwa na nyimbo kama ‘Saa ya Wokovu’, ‘Upendo wa Yesu’, ‘Nitarap Tu’, ‘Sauti Hii’, ‘My Life’, ‘Let it Go’ na ‘Zinduka’.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Comments