UFAHAMU WA KIMUNGU

Na Mwinjilisti John Chinyuli

Wakati ufahamu wa dunia unasema mpende akupendaye asiye kupenda achana nae,ufahamu wa Kimungu unasema wapendeni adui zenu waombeni wanao wauzi, ooh haleluya,"Mathayo 5:14"


-wakati ufahamu wa kidunia unasema haki sawa ufahamu wa Kimungu unasema mwanaume n kiongozi wa familia(kichwa) ampende mke wake na kumuheshimu nao wataishi kwa amani "1 Koritho 11:3"

 
-wakati ufahamu wa dunia unasema jino kwa jino ufahamu wa Kimungu unasema tuushinde ubaya kwa wema,yaaani mpaka rahaa,"Rumi 12:21"


-wakati ufahamu wa kidunia unasema hakuna kuokoka duniani,wala hakuna watakatifu duniani ufahamu wa Kimungu unasema watakatifu walio duniani ndio Mungu mwenyewe anao pendenzwa nao kwahiyo kumbe wapo na hili linawezekana tu baada ya kuokoka,kama hujaokoka take action "Zaburi 16:3"


-wakati ufahamu wa kidunia ukisema kuokoka ni umaskini,utembee kinyonge,uvae malapulapu ufahamu wa Kimungu unasema sisi ni matajiri wa Rohoni tena na mwilini,Yesu mwenyewe alichukua umaskini wetu ili sisi tuwe matajiri oooh haleluyah "Wakolosai 4:19"
-wakati ufahamu wa dunia unasema kuchezea ujana ndio mtu anakula maisha na raha za ajana yaan et kula bata ufahamu wa Kimungu unasema furaha yetu ni kuishi maisha ya haki tutakula raha za hapa na za ule ulimwenge ujao yaan" Zaburi 37:29"


-wakati ufahamu wa dunia unaogopa wachawi na waganga na kuwaona ndio msaada wao na hata kwenda kuwasujudia ufahamu wa Kimungu unasema ametupa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge "Luka 10:19"


Ndani ya ufahamu wa Kimungu ndipo ipo hekima,ushindi,amani,maarifa ,tena unapatanisha maadui,hatukukokoka ili tuwe wajinga au tupotee bali tumeokoka ili tuwe na UFAHAMU WA KIMUNGU oooh haleluya,blessed be u...! tamani kuishi maisha yanaongonzwa na ufahamu wa Kimungu

 

                 MUNGU akubariki sana.
 
                 By Mwinjilisti John Chinyuli 
                 0767 592989/0712 592989

Comments