ILIKUWA NI JUMAPILI YA UKOMBOZI NA KUFUNGULIWA KPC KAWE.

BWANA YESU yuko kazini kuwaponya na kuwaweka huru wote ambao wako tayari kuwekwa huru.
Jumapili ya jana ilikuwa ni jumapili ya ukombozi na kufunguliwa katika ibada kuu ya kanisa la Kawe Pentecostal Church. (KPC). 

Akifundisha somo lililoambatana na uponyaji Mchungaji Elly Boto alisema kwamba KAZI YA KUPONYA NI KAZI YA BWANA YESU hivyo yeyote atakayetaka kupona atapona, yeyote atakayetaka kufunguliwa atafunguliwa na yeyote atakayetaka uzima wa BWANA ataupata. 

Ilikuwa ni ibada ya ajabu sana ambapo kaka mmoja jina lake Yusufu alifunguliwa kutoka kwenye nguvu za giza ambazo zimemtesa tangu akiwa mtoto na kujikuta akifanya uchawi wa hali ya juu sana akishirikiana na Babu yake  huko tangu, alisema kwamba amewahi kushiriki uchawi wa hali ya juu lakini BWANA YESU amemhurumia na sasa yuko huru mbali na hirizi , mbali na majini, mbali na mizimu yuko huru kwa BWANA YESU. Hizi ni baadhi ya picha katika ibada hiyo pia kama unahitaji maombezi na ushauri ni bure kabisa pia namba
0719640642 au 0752965812. pia unaweza kumpigia mzee kiongozi wa kanisa hilo kwa namba 0657361222. ni bure kabisa 





wakati wa kumwabudu  MUNGU


ni saa ya uponyaji na kufunguliwa

Yesu aliponya na kuokoa

Yusufu akiombewa

ni uzima kwa jina la YESU KRISTO.

DADA HUYU AKIFUNGULIWA

Mchungaji Elly Boto akimwombea dada huyu. ambaye alikuwa anasumbuliwa na nguvu za giza.





BWANA nikumbuke na kuniponya






Comments