MFAHAMU KEKE: MUIMBAJI KUTOKA AFRIKA KUSINI ALIYETIA FORA KATIKA TAMASHA LA PASAKA



Mwanzilishi na mchungaji wa SHERKINAH GLORY WORSHIP TABERNACLE nchini Afrika Kusini, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Black Pearl Media, Mshindi wa tuzo mbalimbali za muziki wa Injili ambaye ametoa CD na DVD zilizofikia mauzo ya platnum na kusambaa kote Afrika, Muigizaji wa ukumbini na Mchezaji anayejulikana kama Keke, Kekeletso Phoofolo, Jumapili ya pasaka mwaka huu  aliungana na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka Tanzania, Kenya, Zambia na Uingereza katika kumsifu Mungu katika Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka jijini Dar es Salaam likiandaliwa na Msama Promotions chini ya Mkurugenzi wake ndugu Alex Msama.

Kekeletso Phoofolo (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Tamasha la Pasaka.

Miongoni mwa wanamuziki waliotumbuiza katika tamasha hilo ni pamoja na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Sara K kutoka Kenya, Glorious Worship Team, John Lisu, Mwanamuziki kutoka UK na Rose Muhando.

Katika Tamasha hilo mgeni rasmi alikua ni Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania mh.Bernad Membe ambaye alimuwakilisha rais Jakaya Kikwete kutokana na kutoweza kuhudhuria kwa kuwa nje ya nchi kwa shughuli za kiserikali.
Keke akisalimiana na Mhe. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania

Utukufu ni kwa Bwana aliyeubariki ulimwengu na kumpa kipawa mtu huyu na nafasi ya kuonyesha kipawa chake hicho kisicho na kifani katika nchi ya walio hai. Sio tu kipaji kilicho katika mzunguko wa damu na katika mishipa yake, lakini pia nguvu ya Mungu kupitia muziki wake ambayo inamtofautisha yeye na wasanii wengine.

Tumbuizo lilikuwa zuri ni wimbo baada ya wimbo baada ya wimbo

Wakati Afrika Kusini ... ilikuwa imechoka na Tunes zilizozoeleka katika muziki wa injili, Keke aliwasili na kuleta dhana tofauti kwa kuuleta muziki wa Injili kwa vijana kwa jinsi inayowafaa. Kubadilika kwake juu ya jukwaa humfanya kila mmoja kustaajabu na kuvutiwa na muziki wa Injili.

Keke, ambaye jina lake halisi ni Kekeletso Phoofolo , alizaliwa na kukulia Pimvill , Soweto. Akiwa na umri wa zaidi ya miaka 30 mwimbaji ambaye akiwahi kuwa na bidii ya kuwa katika jeshi lakini muziki alichukua nafasi na kumfanya kuanza kazi yake na Zoe Gospel Music mwaka 1994 kama “backing vocalist” na baadae kukamilisha kwenye "Shell Road to Fame " Sun City mwala 1997 kama mkongwe.



Back Vocalists wakimsindikiza Keke katika Tamasha la Pasaka
Keke kamwe hakuwa akijizuia mwenyewe; mwaka 1998 aliingia katika Kwaito na kundi la watu walioitwa Kom - Kom . Kisha alipata fursa ya kwenda kwenye ziara na Benjamin Dube 1999 kabla ya kujiunga na " Joyous Celebration 5" mwaka 2000-2001 kama mojawapo wa waimbaji viongozi wa kwaya. Kuongoza kwake katika wimbo 'Jo Ke Mohlolo - Hlolo' kulimpa nafasi ya kufanya kazi na kundi wanaume la Redeemed. 
Katika kuhudumu kwake na kutafuta kibali  Keke amefanya kazi na wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Bheki Mseleku, Winston Mankunku na Umoja . Hii ilisababisha simu kutoka kwa Malkia wa Swaziland kuongoza na kusimamia "live" recording ya Redemption Choir mwaka 2001-2004 na kumpatia nafasi zaidi za kufanya “projects” katika nchi za jirani.
Mpiga drums nambari moja wa Keke akiwa anahudu kwa kipawa chake

Mwaka 2006 aliamua kuimba kama solo ambayo ilifanya vizuri. Mafanikio ya albamu yake ya kwanza iitwayoRestoration’ (Matengenezo) iliandaa njia kwa ajili ya albamu yake ya pili 'Revival (Uamsho)' ambayo ilikuwa 'Live' DVD iliyorekodiwa "Vaal University of Technology” (Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Vaal).
Kwenye UAMSHO, Keke ambaye ni mume wa mke mmoja na baba wa watoto watatu anasema 'Sote tuna nafasi ya kuwa na tunachotaka, na tunachohitaji kufufua akili zetu. Hisia lazima zishughulikiwe kwa sababu tuna uhuru wetu na Afrika ina zaidi ya inavyohitaji. Tuje nje ya mawazo ya kimaskini. Huu si wakati wa kuangalia nyuma kwa sababu kama tukifanya hivyo, hatutaweza kuiona kesho.” DVD hiyo ina ya nyimbo nzuri kama vile Sefapano, ‘I’m in Love’, ‘I need Your Touch’ na ‘Testimony’ to mention few of the best in his live album.

Baadhi ya umati wa watu waliohudhuria Tamasha la Pasaka
Album zilizorekodiwa “live” ambazo Keke amefanya katika huduma yake ya Muziki wa Injili ni Revival, Living Testimony, Holy of Hollies na Spirit Unlimited.
 
 

Comments