BWANA YESU NISAIDIE, UNAFIKI USIONEKANE KWANGU!

Na Lucy Marandu

Luka 6:40

Nitawezaje kuwa na ujasiri wa kukemea/kuonya ikiwa nami ninayafanya yaleyale wayafanyayo wale niwaonyao??
1kor 11:1

"Basi mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe hulionii?? Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? MNAFIKI WEWE, itoe kwanza ile boriti ktk jicho lk mwenyewe ndipo utakapoona VEMA kukiona kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako" Luka 6:41-42

Ahaaaaa kumbe imetumepaswa kujiangalia kwenye kioo kwanza kabla ya kutoka njee?(kuwaendea wengine) kwa kuwafundisha na kuwaonya??

Kumbe ni baada ya kujiona sisi kuwa wasafi ndipo tunaweza kuona VEMA kibanzi kilicho ktk jicho la wenzetuu??

Wale watumishi wa Mungu wanaowahubiri wengine na kuwaambia eti msinifuate mimi bali mfuate maneno niwaambiao, kumbe ni watumishi wa Shetani?? Ha ha haaa....
Akawaambia;-
"Je, aliye Kipofu aweza kumuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili??"
Luka 6:39

Mungu atusaidie sana, tusije tukawa miongoni mwa viongozi vipofu, na hatimaye kuwadumbukiza wateule wa Mungu shimoni bure!

Mungu na Atusaidie sana sana!

Ameen!
By Lucy Marandu.

Comments