WAKATI WAKO WA KUOKOKA NA MATESO YA KUZIMU NI SASA.


Bwana Yesu asifiwe.

Katika Luka16:24-25 imeandikwa:
"Akalia,akasema,Ee baba Ibrahimu,nihurumie,umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini,auburudishe ulimi wangu;kwa sababu ninateswa katika moto huu.Ibrahimu akasema,Mwanangu,kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako,na Lazaro vivyo alipata mabaya;na
sasa yeye yupo hapa anafarijiwa,na wewe unaumizwa.


Alleluyah..................

Kabalama Masatu.

Hii habari ukiwa makini kuisoma basi nina uhakika utaogopa kwa wakati huu kudharau habari njema za injili ya neno la Mungu linalohubiriwa ulimwenguni kote kwa maelfu na maelfu.

Ndugu yangu mpendwa huu ndiyo wakati wa kufanya maamuzi sahihi ili ujiweke katika mazingira mazuri.

Hebu fikiri juu ya tabu aliyoipata Lazaro kipindi alipokuwa hai hapa duniani na ufikiri juu ya anasa alizokuwa anazifanya huyu tajiri.


Tunaona wazi mwisho wa maisha yao baada ya kufa.
Sina njia nyingine mbadala nitakayokueleza ili ikuokoe na mateso ya kuzimu isipokuwa ni wewe kumkubali Yesu na kuokoka.
Hebu fikiri huko kuzimu huyu tajiri anatamani angalau apate hata tone la maji.Ooooh,hakika ni mateso.


Kuzimu ni vilio,kuzimu kunatisha,kuzimu hafai mwanadamu kwenda ila kwa ugumu wa mioyo yetu tunajikuta tunaishia kuzimu.
Fanya maandalizi ya maisha yako ya baadaye baada ya kufa ungali bado uko hai.Hatima ya maisha yako baada ya kufa iko mikononi mwako,mateso ya kuzimu husaidiwi na mtu yeyote yule.Yanakukabili wewe mwenyewe maana ndiyo mshahara wa yale uliyoyatenda ukiwa duniani(ni pesheni).
Hakuna nafasi ya kutengeneza kwa waliyokwisha kufa.
Nafasi ni sasa,usiiache neema hii ndugu yangu usije ukalia na kusema nilihubiriwa kuanzia kanisani mpaka mitandaoni lakini niliwaona wapuuzi.

 
Ooooh,ndugu njoo kwa Yesu akuokoe na mateso ya kuzimu.
  NJOOO. NJOOO. NJOOO,
YESU ANAKUITA.



MUNGU akubariki 
By Kabalama Masatu.
Mawasiliano ni:
0753-305957;
0789-628226;
0717-624035.

Comments