JE NABII ISSA(AS) NDIYE YESU KRISTO? (2)

Mtume Peter Rashid Abubakar
Mtume Peter Rashid Abubakar aendelea kufafanua somo la JE NABII ISSA(AS) NDIYE YESU KRISTO? Kipengele cha pili hebu endelea msomaji wangu. Na kama hukusoma sehemu ya kwanza FUNGUA HAPA


2. KUUMBWA KWA ISSA.
ISSA-Tusomapo habari za Issa ndani ya Quran, tunaelezwa kuwa Issa kaumbwa kama alivyoumbwa Adamu. Bila shaka hali ya Issa kwa mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adamu: alimuumba kwa udongo kisha akamwambia KUWA basi akawa(AL-IMRAN 3:59). Hivyo kwa mujibu wa aya hii, Issa kaumbwa kama alivyoumbwa Adamu,yaani kwa udongo. Na kwa maana hiyo kama vile Adamu alivyotenda dhambi na ndivyo na Issa alivyo.
YESU-Hapo mwanzo kulikuwapo Neno,naye Neno alikuwako Mungu,Naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu,vyote vilifanyika kwa huyo,Wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.(Yohana 1:1-4). Na sasa Baba, unitukuze mimi pamoja nawe,kwa utukufu ulee niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako(Yohana 17:5). Maandiko haya yanathibitisha kuwa Yesu hakuumbwa,bali ndiye aliumba kila kitu yaani ndiye muumbaji,kwasababu pasipo yeye hakikufanyika chochote. Vile vile Biblia inatueleza kuwa alikuwapo kabla ya ulimwengu kuwapo. Hivyo Yesu hakuumbwa. Maana yake ni kwamba hata huyo Issa ambaye waislam wanamjua ndani ya Quran,aliumbwa na huyo Yesu kristo. Kwa hiyo kwa ushahidi huu ya kuumbwa kwa Issa na Yesu ni wawili tofauti(THINAIN MUTAFARIKAN).


 3. JE MANABII WALIWATABIRI?
ISSA-Tunaposoma kitabu cha Quran,hatuoni andiko lolote linalomzungumzia kutabiriwa kwa Issa,hivyo huyu Issa yeye hakutabiriwa na Nabii yeyote kama akina Musa,Daudi, n.k.
YESU-Ndani ya Biblia kuna tabiri 63 za manabii,wakitabiri habari habari za Yesu Kristo. Hebu tuangalie tabiri chache katika hizo. Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama Bikra atachukua mimba atazaa mtoto mwanaume naye atamwita jina lake Imanuel: Isaya 7:14,Isaya 9:6-7. Huu ni utabiri ambao unamhusu Bwana Yesu hii ni kuthibitisha kuwa yeye alitabiriwa na manabii,hivyo basi watu wale,mayahudi walijua kwamba atakuja mtawala atakayeitwa Masihi. Vile vile ifuatayo inadhihirisha kuwavYesu alitabiriwa.
UTABIRI WA AGANO LA KALE.
Mwanzo 49:10....Atakuwa uzao wa Yuda... Zaburi 2:7...Atakuwa Mwana wa Mungu.... Zaburi 72:10-15...Watu wakuu watamsujudia..... Yeremia 31:15...Watoto watauawa.
AGANO JIPYA.
Waebrania 7:14..maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda... Luka 1:32-35, Mathayo 2:16-18.
Hizi ni baadhi tu za tabiri ambazo zilitabiriwa na manabii. Kwa ushahidi huu, Issa hawezi kuwa ndiye Yesu kwasababu Issa hakutabiriwa(THINAIN MUNTAFARIKAN).


 4. NASABA (Wazazi wao).
Watu wengi wanaposema kuwa Issa ndiye Yesu husema kwamba kwa kuwa mama yake Yesu alikuwa akiitwa Mariamu na Mama yake Issa alikuwa akiitwa Mariam. Hivyo kwa kigezo hicho Issa ndiye Yesu. Hiyo hoja haina nguvu kwani akina Mariamu wako wengi. Tatizo si kufanana majina, tatizo ni Mariamu yupi aliyemzaa Yesu na Mariamu yupi aliyemzaa Issa?. Kwa mujibu wa kitabu cha Quran Mariamu aliyemzaa Issa ni dada yake na Haruni!! Quran inasema Suratul Mariam 19:28. Ewe dada yake Haruni,Baba yako hakuwa mtu mbaya wala mama yako hakuwa hasharati!!. Hivyo kwa mujibu wa maandiko hayo Mariam ni dada yake na Haruni ambaye ni ndugu yake na Musa!!. Sasa kwa mujibu wa Biblia tunakuta kwamba dada yake Haruni alikuwa akiitwa Miriamu. Kutoka 15:20. Na miriam nabii mke ndugu yake Haruni akatwaa tari mkononi mwake. Miriam alikuwa ukoo wa Lawi na kaka zake,na Bwana yesu alikuwa ukoo wa Yuda.
YESU-Mama yake aliitwa Mariamu ambaye alikuwa katika ukoo wa Yuda kama maandiko yalivyotabiri kuwa atatoka katika ukoo huo. Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda. Waebrania 7:14. Kwa ushahidi huu Issa na Yesu ni wawili tofauti kabisaa kwa kiarabu (THINAIN MUNTAFARIKAN).

MUNGU akubariki sana.





Mtume Peter Abubakar akihubiri katika moja ya makanisa nje ya Tanzania.
N.B.  Mtume Peter Rashid ni msomi na mtaalamu kabisa wa dini maana amewahi kuwa shehe na kusomea kila elimu ya dini ya kiislamu ila BWANA YESU akamukoa na sasa anatumika katika viwango vya juu sana, yaani kama unasumbuliwa na nguvu za giza kimbilia kanisani kwake mbezi  mwisho jijini Dar es salaam, mimi binafsi huwa ananibariki sana maana kama unasumbuliwa na mapepo yeye anayajua yote majina yao hivyo hata hasumbuki sana maana utasikia tu kwamba '' jini jabali toka kwa jina la YESU KRISTO, wewe shamsa toka kwa jina la YESU KRISTO'' na  mgonjwa anapona. Anakukaribisha sana kanisani kwake mbezi mwisho jijini Dar es salaam.

Comments