MKE WA ADDO NOVEMBER AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE


Addo Novemba ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania na ni Rais wa Chama Cha Muziki wa Injili Tanzania na pia ni mwanasheri. Hivi karibu mke wake kwa neema ya Mungu ameweza kujifungua mtoto wa kike, na hivi ndivyo alivyoaandika Addo katika FB akaunti yake

"Tunamshukuru sana Mungu kwa ajili ya Mke wangu kipenzi Deborah Gwimile Mwasongwe kwa kujifungua mtoto KIKE muda wa saa saba na dakika 25 usiku huu, Mama na Mtoto ni wazima wa afya! MUNGU YESU ATUKUZWE SANA! NALOLI NALOLI! ahsanteni wanamaombi duniani kote! Ahsante ROHO MTAKATIFU! GLORY GLORY GLORY!"
Rumafrica For All Nations inakupongeza sana Addo na mke wako kwa kupata zawadi hii ya mtoto, kwani kuna watu wengi wanatafuta watoto na hawapati, lakini wewe Mungu amaekujalia. Tunawatakia malezi mema na Mungu azidi kuwapa afya njema na kubariki kazi ya mikono yenu....Asanteni

Comments