HIVI GIZA NA NURU VINA SHIRIKA GANI?

Na  Mwinjilisti Jofrey Sanga

Sikuyajua kama ndivyo yalivyo mpaka roho aliponionyesha, shetani anavyojua kujigeuza kama malaika yule wa nuru, sasa kajigeuza na amekuwa rangi nyingi, kajiingiza kwa siri kanisani, watu wa MUNGU wao bila kujua wameanza kumwabudu.
 1 Yohana 3:8 unasema hivi azitendaye dhambi ni wa shetani maana shetani alizitenda tokea mwanzo. Tunao watu wengi makanisani, kutenda dhambi kwao sio tishio, hivi watu hawa wanapokutana pamoja kuabudu wanamwabudu nani?

Kutoa pesa kwao sio tatizo, hata fungu la kumi sio tatizo kwao wanatoa tuu, hawajatubu dhambi wanaendelea kusali, hivi watu hawa wanamwabudu nani? wengine ni viongozi wa dini, na wengine ni washirika wao, na hata gari la kanisa wao ndio walionunua na kanisa pia walijenga wao lakini wamezikumbatia dhambi na wanazitenda huku wakiendelea kuabudu, Mchungaji ukitaka kukosana nao awaambie watubu dhambi, na wachungaji nao wamekumbatiana na washirika wao katika dhambi, swali je? wanamwabudu nani hawa?


Hata wahubiri nao ndio balaa tena sana, ni washirika kumbe ni wake zao, wamewakuta watu wamesimama, wao wanawaangusha ili wawaibie, wanahubiri ujumbe wa kutoa wanasahau toba ya msamaha na kweli, je watu hawa wakikutana pamoja kuabudu wanamwabudu nani?
Mimi nashangaa na Makanisa mengine ya ajabu, eti Wokovu wa Yesu wao wanaukataa, kulewa pombe kwao sio ajabu hata wachungaji wao wanaibariki, ukiwambia wewe umeokoka wanasema iyo sio imani yao, wakati mwingine katika ibada zao wanamtaja YESU lakini katika matendo yao wanamkataa, hivi watu hawa katika ibada zao wanamwabudu nani?
Giza na Nuru zina shirika gani? hebu kuweni giza katika Nuru ambaye ni YESU KRISTO ili tumwabudu MUNGU katika roho na pia kweli, YESU ni kweli na uzima tena ndio njia ya kutufikisha Mbinguni, MUNGU ataka tumwabudu katika roho na pia kweli.
EWE shetani pepo uliye mchafu, NAKUAMURU KWA JINA LAKE YESU TOKA NDANI YA KANISA LAKE MUNGU NENDA KUZIMU UKACHOMWE MOTO KATIKA JINA LA YESU, TUMEGUNDUA HILA NA NJAMA ZAKO, UNATAKA TUKUABUDU WEWE NI KAMA NANI? NAKWAMBIA HIVI TUNAYE MUNGU BABA WETU YEHOVA, MUNGU ALIYE HAI, SIFA UTUKUFU NI WAKE HATA MILELE NA MILELE. AMINA 

 
JAMANI HEBU TUMWABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI ACHA MAIGIZO, MUNGU ATAKA SOTE TUMWABUDU KATIKA ROHO NA KWELI.
ZIDI KUBARIKIWA MTU WA MUNGU

By  Mwinjilisti Jofrey Sanga

Comments