NUKUU MUHIMU KUTOKA KWA WATUMISHI WA MUNGU.

Mwinjilist Reinhard Bonnke
BWANA YESU asifiwe.
Kuanzia leo nitakuwa nakuletea Nukuu kutoka kwa watumishi mbalimbali wa MUNGU walizosema kwenye mahubiri yao au kwenye mahojiano kwa lengo la kutufundisha, kuinua imani zetu na kutufanya tujue jambo la kutenda ili kumpendeza MUNGU wa mbinguni. kwa leo nakuletea maneno ya watumishi hawa wa MUNGU aliye hai.

1. Usipoteze uhakika wa wokovu wako kwa kukaa kwenye mafundisho ya kanisa ambalo linakataa neno la MUNGU na Nguvu ya MUNGU- By Mwinjilisti REINHARD BONNKE.

2.  ROHO MTAKATIFU hana mashaka wala haandiki mashaka, Ahadi za BWANA ni ''ndio na Amina'' wala sio'' la au labda''- By MARTIN LUTHER.

3.Uhusiano wako na MUNGU ni muhimu kuliko huduma yako, linda uhusiano wako na MUNGU.By Mwl. CHRISTOPHER MWAKASEGE.

4. Ndoto ni ujumbe wa mambo yaliyopita au yajayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana, ni lugha ya kiroho- By Mtume na Nabii JOSEPHAT MWINGIRA

5. Mahubiri sahihi ni yale tu ambayo YESU KRISTO ni sehemu ya mahubiri hayo kwa lengo la kuokoa roho za watu, ndivyo walivyohubiri Mitume  wote kwenye Biblia Takatifu-By PETER M  MABULA.

6. Kama tunataka kumwona MUNGU akitenda kazi, ni lazima  tuwe mbali na woga, kuruhusu kutawaliwa na woga ni kumfanya MUNGU kuwa na uwezo mdogo kuliko yale yanayotuogopesha- By Askofu ZACHARIA KAKOBE.

7.Kuna watu wanadai pesa ndio kila kitu katika maisha yetu ya duniani, Lakini sio kweli kwa sababu pesa inaweza kununua kitanda lakini sio usingizi, Pesa inaweza kununua dawa lakini sio afya. Tumtegemee MUNGU kwa kila jambo tunalolihitaji-By Mchungaji Mama GETRUDA RWAKATARE.

8. MUNGU anabaki kuwa MUNGU hata kama hajajibu sawasawa na jinsi ulivyomuomba, kumbuka hiyo wala usije ukasahau hata siku moja-By Mwl. CHRISTOPHER MWAKASEGE.

 Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .

Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma ujumbe huu



Comments