JE UNAFAHAMU WEWE NI MFALME NA KUHANI?

Na Emmanuel Kamalamo.

Unaweza usielewe mapema jambo hili ,lakini utaelewa baada ya kusoma kile Roho Mtakatifu anataka usome na uelewe.
Soma na mimi kitabu cha Ufunuo 1:5-6 mandiko yanasema hivi,"....Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, na kutufanya kuwa wafalme na makuhani kwa Mungu"
Kwa hiyo kama umeokoka tambua "UMEOSHWA KWA DAMU YA YESU" na kama umeoshwa kwa damu ya Yesu si kuondolewa dhambi tu la asha! bali unapewa na nafasi ya wewe kuwa "MFALME NA KUHANI" kwa kuthibitishwa kwa damu ya Yesu.
Unapokuwa "MFALME" unakuwa na mamlaka na kutoa neno la mwisho juu ya mambo yote kama mfalme.
Na unapokuwa "KUHANI" maana yake unakuwa na nafasi ya kwenda kwenda mbele za Mungu kwa njia ya maombi kwa ajili yako mwenyewe na kwa ajilu ya watu wengine.

Wewe una vyeo vikubwa sana katika utawala wa Mungu katika nafasi ya..."UFALME NA UKUHANI"...katika ulimwengu wa roho. Ukitumia "UFALME" na "UKUHANI" uliopewa na Mungu kwa njia ya damu ya Yesu, katika ulimwengu wa roho shetani/mapepo/wachawi/majini hawawezi kuwa na neno la kusema wala kupinga juu ya kile ambacho ametamka wewe mwana wa Mungu.
NA WEWE WAWEZA KUWA MFALME NA KUHANI UKIMPOKEA YESU KRISTO MOYONI MWAKO.
Ni kujiunga katika uzao mteule wa ukuhani wa kifalme(watu waliookoka na kuzaliwa mara ya pili) taifa takatifu watu wa milki ya Mungu upate kuzitangaza fadhiri zake yeye anayekuita utoke gizani uingie katika nuru yake ya ajabu.
SEMA SALA HII KWA IMANI.
Mungu Baba, mimi ni mwenye dhambi, ninatubu naomba unisamehe dhambi zangu zote. Nioshe kwa damu ya Yesu Kristo, na ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na uliandike kwenye kitabu cha uzima. Ingia moyoni mwangu kwa uwezo wa Roho Mtakatifu wako, asante kwa kunisamehee na kuniokoa. Amen.
MUNGU AKUBARIKI
ekamalamo@gmail.com

Comments