UKITAKA KUFANIKIWA MAISHANI, FANYA HIVI!

Na Mtumishi Vicent Mwengo.

1. ZUNGUMZA KWA UMAKINI: 
Kinywa chako kinaweza kufanya ukafanikiwa au ukajiharibia, mtu anaweza akawa anakuheshimu ila utakapozungumza pumba tu, atakushusha thamani yote.

2. JENGA UAMINIFU: 
Ukiaminiwa na walimu, wanafunzi wenzako, majirani na hata bosi wako ni rahisi wewe kuweza kufanikiwa maana utakuwa na mtu wa kwanza kwao kukufikiria pale wanapotaka kushirikisha watu mambo yao. kama huaminiki itakuwa ngumu sana

3. ONESHA HESHIMA KWA WATU WOTE: 
Bila kujali mtu huyu ni tajiri au maskini, mkubwa au mdogo, heshimu kila mtu maana hujui kesho yako itakuwaje

4. KUWA MVUMILIVU:
 Uvumilivu unahitajika katika kila kitu, pengine ni kazi au masomo, haijalishi umefeli cha muhimu ni kuvumilia hadi mwisho utashinda. onesho uvumilivu hata kazini kwako.

5. ACHA UOGA: 
Tabia hii ya uoga hufanya watu wengi kushindwa, maana anapotaka kufanya kitu uoga unamshika anaacha. Uoga wake ndio mchawi wa maendeleo yako! ushinde uoga

6. WEKA AKIBA; 
Hata kama ni mwanafunzi hela unayopewa na mzazi au mkopo, jitahidi utunze kiasi, na wewe kama ni mfanyakazi usitumie mshahara wako wote, kumbuka akiba haiozi heshimu hata sh 100.

7. KUWA NA FIKIRA MPYA:
 Fikira mpya zitakufanya uweze kupata pesa, zitakufanya upate mbinu za kufaulu mitihani, na zitakufanya uwe mbunifu kazini hata kushawishi bosi akupandishe cheo.

8. VAA VIZURI UPENDEZE; 
Katika dunia hii nafasi nyingi hupatikana kutokana na muonekano wako ulivyo, ukishindwa kuwa na muonekano wa ushawishi wengi watashindwa kukuamini

9. TUMIA PESA KWA AKILI: 
Ndio pesa inatafutwa itumiwe lakini kabla hujatumia pesa hovyo angalia majukumu uliyonayo, kama una mke na watoto huwezi kujilinganisha na mtu aliye single. Na wewe ulie single, angalia matumizi yenye akili na sio starehe zisizo msingi
MUNGU AWABARIKI.
By Vicent Mwengo.

Comments