MAHUBIRI SAHIHI NI YALE AMBAYO KRISTO NI SEHEMU YA MAHUBIRI HAYO.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la uzima.
Siku moja nilipata ufunuo kwa sauti ukiniambia ''Usiishi kwa sababu tu unaishi bali ishi kwa sababu YESU KRISTO anaishi ndani yako''
Niliuandika ufunuo huo na kuutunza sana moyoni mwangu, nilitaka tu kuishi kwa sababu YESU KRISTO anaishi ndani yangu, niliamua kumhubiri KRISTO anayeokoa. Tangu hapo najitahidi katika kila somo langu basi aonekane YESU anayeokoa na hili somo la leo ni nla 540 kuliandika tangu November 2012.
Siku nyingine Tena nikapata ufunuo kwa sauti ukisema ''Mahubiri sahihi ni yale ambayo YESU KRISTO ni sehemu ya mahubiri hayo kwa lengo la kuwaokoa wanadamu''

Baada ya ufunuo huo nilijaribu kuchunguza kama mitume katika Biblia walikuwa wanafanya hivyo? 
Nikagundua kwamba ndio kazi ya Mitume waliyokuwa wanaifanya, nikagundua kwamba ROHO MTAKATIFU aliyewafunulia Mitume basi ndio huyo amenifunulia na mimi maana mitume kazi yao ilikuwa moja tu kuhubiri injili ya wokovu wa KRISTO anayeokoa. Ukisoma Agano jipya lote lina habari kuu moja yaani Wokovu wa KRISTO unaleta Msamaha wa dhambi kwa kila anayemwamwini YESU na kumpokea kama Mwokozi wake.
Hakuna mtu anayeishi duniani bila imani ila tatizo tu ni kwamba imani ya kweli ni moja tu yaani Wokovu wa KRISTO YESU.
Warumi 10:17 ''Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la KRISTO.''

Hiyo ndio imani pekee moja tu ya uzima wa milele ambayo chanzo chake ni lazima ulisikie Neno la KRISTO.
Watumishi Waaminifu Wa BWANA YESU Ambao ROHO MTAKATIFU Amewapa Neno Lake Ili Wafundishe Ni Wengi. Kuna Watumishi Walipewa Kufundisha Imani Kama Kenneth Haggin.
 Kuna Waliopewa Kulisha Kondoo Kama Mwl Mwakasege. 
Kuna Waliopewa Neno La Siku Za Mwisho. 
Kuna Waliopewa Kufundisha Utakatifu Kama Askofu Kakobe. Kuna Waliopewa Kufundisha Madhara Ya Dhambi, Kuna Waliopewa Kuonya, Kuna Waliopewa Kukaripia, Kuna Waliopewa Kukemea. Zote Ni Huduma Njema. Sio Kwamba Aliyepewa Huduma Moja Hawezi Kufundisha Nyingine, Hapana, Anaweza Kufundisha Ila Kuna Wanaofiti Zaidi Kwa Sababu Wapo Kwenye Eneo Lao Walilopewa Na ROHO MTAKATIFU. 
 Mfano Ujumbe Wa Mwl Mwakasege Ukinipa Niufundishe Mimi Ambaye Ni Mwinjilisti kwa mfano Itanipa Shida Na Watu Wanaweza Wasinielewe Vizuri Kama Mwl Mwakasege Ambapo Ujumbe Wake utapenya Ndani Kabisa Ya Moyo kabisa kwa sababu anayeufundisha yuko katika eneo lake na nafasi yake aliyopewa na ROHO MTAKATIFU. Hata Wewe Uliyeokoka Una Huduma Ambayo Utatakiwa Uifanye Na Ukiifanya Wewe Itakuwa Nzuri Zaidi Kuliko Mimi Nikiifanya.
Kuna wengine humtumikia KRISTO kupitia uimbaji, nikiiga mimi sitafanya vizuri kama waimbaji wenyewe ambao ndio waliokabidhiwa huduma hiyo.
Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.
 
 Mithali 12:1 {Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa, Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama}.

 Barikiwa sana wewe unayependa mafundisho ya neno la MUNGU.
Ubarikiwe sana wewe ambaye unalifanyia kazi neno la MUNGU kila iitwapo leo.
 Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.
Ubarikiwe sana wewe unayechota maarifa ya kiMUNGU kupitia Neno lake maana adui hatakuweza kamwe.

Wakolosai 3:16-17 '' Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana YESU, mkimshukuru MUNGU Baba kwa yeye.''

Ndugu kama umepata vitu vingi lakini hujaokoka basi wewe umepungukiwa jambo moja yaani umepungukiwa Neno a KRISTO.
Ukiwa na Neno la KRISTO utafanya kazi ya MUNGU kwa usahihi.
Ukiwa na Neno la KRISTO utumishi wako hautalaumiwa.
Mtumishi Wa MUNGU Hatakiwi Kuwa Mlopokaji bali msema kweli ya MUNGU.
Ni muhimu sana kila mhubiri asimame katika zamu yake ya kuhubiri injili ya KRISTO inayookoa.
 Mahubiri Ni Maneno Ya Watu Yanayoambatana Na Neno La MUNGU Na Kulitii Neno La MUNGU. 
Ukiona Mahubiri Yanalipinga Neno La MUNGU(Biblia) Hayo Sio Mahubiri Sahihi.
Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.
 Ukiona Mahubiri Yanailekebisha Biblia Hayo Sio Mahubiri Sahihi.
 Ukiona Mahubiri Yanaifafanua Biblia Kinyume Na Inavyotaka Yenyewe Hayo Sio Mahubiri Sahihi.
Na Mahubiri Yasiyo Na Kipengele Cha Toba Hayo Nayo Yanatakiwa Yalekebishwe. 
Mahubiri Humshuhudia MUNGU Na Kazi Zake Na Kuainisha Mpango Wake. 
Mahubiri Sahihi Ni Yale Yaliyo Kwa jinsi Ya KRISTO YESU Na Mtu Wa Kwanza Kuhubiriwa Na Mahubiri Anatakiwa Awe Ni Mhubiri Mwenyewe.
Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.

Warumi 10:13-17 '' kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, BWANA, ni nani aliyeziamini habari zetu? Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la KRISTO.''

 Injili ya KRISTO ni lazima uhubiriwe kama anavyotaka MUNGU na sio wanadamu.
Injili ni msema kweli na lengo la injili ni kusema ukweli ili mwanadmu auache ubaya wake.
Hata kama ni kanisani ni lazima ukweli wa KRISTO usemwe na si vinginevyo.
Ni Heri Kuwa Na Washirika Wachache Wanaoenda Uzima Wa Milele Kuliko Kuwa Na Washirika Wengi Wanaokwenda Jehanamu.
 Heri uwe na waumini wachache ambao wanaishi maisha matakatifu kuliko kuwa na waumini wengi ambao wamejaa dhambi kuanzia kichwani mpaka miguuni. Injili itatukanwa kwa sababu ya hao wengi wasio na hofu ya MUNGU.
Mfano mmoja ni huu; Uganga wa kienyeji ni kazi ya shetani ambayo aliileta ili watu wategemee tunguli badala ya MUNGU aliyewaumba. na ndio maana wote hutumia mizimu na majini ambao ni watoto wa
shetani. Leo kuna baadhi ya wakristo huenda kwa waganga. Kuna ndugu nilimuonya kuhusu kwenda kwa waganga hata hakunielewa maana alisema kwamba hajawahi kusikia kiongozi wake wa dini  akikataza kwenda kwa waganga. Ndugu yangu ambaye na wewe uko katika kundi kama la ndugu huyu nakuombea  MUNGU akupe ufahamu leo ili umjue YESU ni nani na umpe maisha yako.


Zaburi 34:14-16 ''Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie. Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao. Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani. ''

Ndugu lipokee Neno la MUNGU na kubali kubadilishwa na Neno la MUNGU.
Naomba ujue kwamba Tumemkimbilia BWANA YESU Ili Tusiaibike Milele, Hilo ndilo jambo la Kwanza. Jambo La  Pili Ni kwamba  Tumemkimbilia BWANA YESU Ili Tusionewe Na Shetani Na Mawakala Wake. 
Mtu hawi mtakatifu kwa sababu anajitangaza kwamba yeye ni mtakatifu, bali mtu anakuwa mtakatifu kwa kupokea Wokovu wa KRISTO na kisha anajitenga na maovu ya dunia.

1 Yohana 2:15-17 ''Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba(MUNGU) hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele.''

 Neno la Mungu ndilo kweli inayodumu milele. 
Neno la Mungu ndilo linalompa mtu uhakika wa jambo ambao hauwezi kuyumbishwa na kitu chochote.
Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.  Pesa Ni Jawabu La Mambo Yote Lakini Sio Uzima Wa Milele.
Huwezi kupata uzima wa milele kwa kutumia pesa.
Kubali tu kufundishwa na Neno la MUNGU ili utimie kiroho kama ulikitii Neno hilo la wokovu wa uzima.
 "Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote" (Wakolosai 3:16]

  Kuna tatizo moja ninaloliona katika wateule wa MUNGU.
Dalili Moja Wapo Ya Siku Za Mwisho Ni "Watu Kujipenda Wenyewe". Wateule Wengi Leo Wanajipenda Wenyewe Hata Hawataki Kuwashuhudia Wengine Injili Ya BWANA YESU Ili Wapate Uzima Kama Walioupata Wao Hao Wateule. Ndugu Usijipende Mwenyewe Hata Ukasahau Kuwaonya Wengine Ili Watoke Kwenye Hiyo Barabara Ya Jehanamu Waliopo, Na Waje Uzimani Kwa BWANA YESU Baada Kutubu Na Kuokoka Kupitia Neno Lako.
 Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.
 Jambo Muhimu Kwa Kila Mwanadamu Ni Kukataa Kile Akataacho MUNGU Na Kufanya Kile Atakacho MUNGU.
 Ukiliweka neno la MUNGU moyoni mwako kwa kulitafakari, unaweza ukaishi bila kutenda dhambi, kwa kuwa neno hilo litakuwa nuru na taa miguuni pako 
Zaburi 119:105 ''Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.''

Ni heri Neno la KRISTO likawa ndani yako na ukalitii.
Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.
BWANA YESU anasema kwamba Mbingu zitapita na vitu vyote vinapita lakini maneno yake hayatapia kamwe.
 Mathayo 24:35'' Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.''

 Ni heri ndugu ukalihuburi neno la KRISTO la wokovu maana hilo halitapita kamwe.
Ni heri ndugu ukaliishi Neno la MUNGU maana hilo halitapita kamwe.
Neno la MUNGU ni lazima litimie na si vinginevyo. Ukilisusia wewe wengine wanalishika na wanaenda uzima wa milele.
Ukilidharau wewe wengine tunaliheshimu ndio maana tumeandaliwa taji ya uzima mbinguni.
BWANA YESU anaendelea kusema kwamba ''Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.-Marko 13:31'' 

 Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.
 Hii dunia tunapita tu ndio maana tunatakiwa sana  tumpe YESU maisha yetu ili tuwe na uhakika wa maisha yajayo.
Luka 21:33 ''Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.''

 Kama wewe ni mhubiri ni heri ukamhubiri KRISTO anayeokoa na si vinginevyo.
 Utajulikana pote kwa namna unavojitoa kwa MUNGU na si kwa namna unavyojisifia.
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments