NILITAKA KUJIUA WAKATI WA CHRISTMAS ILA YESU AKANIPONYA UKIMWI WAKATI HUO WA CHRISTMAS.

 Na Mchungaji Eliya Chiguru.


Shalom wana wa Mungu. Namshukuru Mungu kunifikisha christmas ya leo. Ninalo jambo la kusema kuhusu siku hii ya christmas ,hasa nikukumbuka mwaka 1993.nilipojaribu kujiua bila mafanikio.


Kisa ni hiki,nilikuwa msabato mzuri tangu utoto ila sikuwa najua nini maana ya kuacha dhambi nk,nilicho kuwa nafahamu ni kutokula samaki wasiokuwa na magamba na kuishika sabato na kukariri maandiko juu ya sabato tu.
Nilikuwa mwasherati mzuri tu, na ikizingatiwa nilizaliwa ziwani na nyumbani kwetu tulikuwa wavuvi wa samaki hivyo uvuvi huo tuliutumia kuwapata wasichana na wamama. 


Mwisho wa siku,hawara zangu wote kumbe walikuwa wameshaathirika na ukimwi na walikufa wote. Nami nikaanza kuugua majipu,kuharisha na homa zisizo na mpangilio. Mwaka 1993 baada ya kuwa nimekata tamaa ya maisha nilifanikiwa kwenda kwa mamaangu mdogo kule wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza hapo ndipo nilipoamua kujiua kwa kununua krorokuin za miatano. Niliandika barua ya kwanini nimeamua kujiua,nikaiweka hapo juu ya meza. Muda huo huo ghafla nilitoka nje baada ya kuhisi kuharisha ,niliporudi ndani nikakuta vidonge vyangu vya kunifanya nife havipo, kumbe baba mdogo, mme wa mama mdogo alikuwa ameshtukia mchezo huo nilipotoka nje tu akaingia chumbani na kuvichukua vile vidonge na huo ndo ukawa ndo mwanzo wa mimi kuokoka,maana wakati nalia kwa uchungu kupotea kwa vidonge, ndipo aliingia chumbani kwangu na kunishauri niende kwa walokole ili waniombee nami nitapona.

Wakati ananipa ushauri huo, yeye ni mzee wa kanisa wa AIC,ila familia tulikuwa tunaenda kwa waganga pamoja na kuabudu kwetu sabato na AIC zetu. Ndipo niliamua kuandika barua kwa Mchungaji mmoja wa kanisa la kiroho aliyekuwa hapo na walikuwa kanisani tena ilikuwa ijumaa jioni. Walikuja na kuniombea na jumapili yake ilikuwa christmas nikaamua kuokoka na kuponywa magonjwa yangu yote tangu wakati huo. Mchungaji aliyeniombea enzi hizo akiwa ni Mchungaji Donatu Chrisant na ndie babaangu wa kiroho, kwa sasa yuko Arusha na ni member wa group hili,lakini pia mamaangu mdogo yumo humu ni watumishi wakubwa tu,wanawezathib
itisha haya nisemayo. Hivyo Christmas huwa ninakumbuka tukio la kutaka kujiua na pia kuponywa magonjwa yangu yote. Zaburi 103:3-5. Ushauri wangu kwako ndugu yangu ,labda na wewe ni mmoja wapo kama Mimi,au unapitia changamoto fulani fulani,usikate tamaa,huyu YESU aliyezaliwa leo,mpe nafasi uone upendo wake kwako,hakika hatakuacha uendelee kuteseka na jambo baya lolote lile. 


Nimeamua kuuweka huu ushuhuda wangu mwenyewe mimi Mchungaji Eliya Chiguru ili utiwe nguvu na ujue MUNGU yupo kukusaidia kama alivyonisaidia mimi.
Kupitia kuponywa kwangu,MUNGU aliweka huduma ya uponyaji na kuwafungua watu,sema tuko vijijini hatuvumi ila wamo.
Kuna kichaa mmoja alifunguliwa hapa nzega,na mlemavu wa mkono pia na kina mama kupata watoto
Barikiwa sana na nakutakia christmas njema katika jina la YESU KRISTO Mwana wa MUNGU aliye hai. Amen.
By Mchungaji Eliya Chiguru.
0763531588
0784531588.



N.B
Mchungaji Eliya Chiguru sasa ni Mchungaji na Ameshafungua Makanisa mengi na MUNGU akimtumia sana kwenye Huduma yake.
Hakika YESU anaponya magonjwa yote haijalishi ni Ukimwi au nini. Ukiamini hakika unapona.
Mathayo 9:35 inasema kwamba YESU aliponya magonjwa Yote.
Ubarikiwe.
Nakuomba share kwa marafiki zako mbalimbali.

Comments