USING'ANG'ANIE DINI UKASAHAU WOKOVU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu sana tujifunze Neno la MUNGU.
Dini ni njia ya kumwabudu Mungu lakini pia sio dini zote humwabudu Mungu YEHOVA/YAHWEH
Kila dini wana Mungu wao isipokuwa Wakristo na wayahudi tu ndio wanaabudu MUNGU mmoja aliyeumba mbingu na dunia na wanadamu wote, dini zingine zinaabudu akina mungu wao.


Yohana 4:20-23 '' Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. YESU akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba(MUNGU) katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba(MUNGU) katika roho na kweli. Kwa maana Baba(MUNGU) awatafuta watu kama hao wamwabudu.''
 
Lakini pia katika Ukristo kuna waliojiingiza kwa siri ili kuwapoteza yamkini hata walio wateule.
Ndio maana Biblia inatushauri kuzijaribu kila roho tuone kama zinatokana na MUNGU.


1 Yohana 4:1 "Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na MUNGU; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani."


Hao waliojiingiza kwa siri katika Ukiristo na kuwapotosha watu Biblia inasema wana jina la kuwa hai lakini wamekufa yaani wana jina safi la ukristo lakini hawamtii KRISTO na kwa njia hiyo hawana nafasi katika ufalme wake.

Ufunuo 3:1 '' ... Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa  ''
 
Kwanini Dini na dhehebu haviwezi kumpeleka mtu mbinguni?
Kuna dini zinafundisha kutimiza matakwa ya dini hizo na sio matakwa ya MUNGU.
Kuna madhehebu hufundisha waamini wao kutimiza matakwa ya dhehebu na sio matakwa ya MUNGU.

Bwana YESU alisema kwamba sio wote wamwitao Bwana Bwana watakaoingia katika uzima wake wa milele, Bali ni wale tu wanaotimiza matakwa ya MUNGU.

 Mathayo 7:21 '' Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.''

Mapenzi/Matakwa ya MUNGU ni yapi?

1. Kuishi Maisha ya wokovu matakatifu na haki.
 2 Kor 4:2 'lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la MUNGU na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za MUNGU.''

2. Kuacha dhambi na mabaya yote.
 Wakolosai 3:9 ''Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;''

3. Kuliishi Neno la MUNGU la injili ya KRISTO.
 Zaburi 119:11 ''Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.''

4. Kumwabudu MUNGU Baba katika roho na kweli.
 Yohana 4:24 ''MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.''

5. Kuenenda kwa ROHO MTAKATIFU na kulitimiza kusudi la MUNGU.
  Warumi 8:14 ''Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.''

Kama dini haimwabudu JEHOVAH hakika dini hiyo ni dini jina tu.
Kama dini haiwafundishi waamini kuokoka kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi na kuishi maisha matakatifu yanayoagizwa na Biblia hakika hiyo dini au dhehebu ni dini jina tu lakini imekufa hata kama ina wamilioni ya waumini.
Waliompokea YESU kama Mwokozi tangu zamani waliokoka.
Matendo 16:30-31 '' .....   yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.'' 
 
Kama dhehebu linakataa Wokovu na kumcha MUNGU katika Wokovu wa KRISTO hakika hiyo dini/Dhehebu ni machukizo kwa MUNGU.
Warumi 10:13 '' kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana(YESU) ataokoka.'' 

Ndugu zangu kwenda mbinguni kunahitaji;

1. Kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi.
Warumi 10:9-10 ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka.Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.'' 
 
2. Kuishi maisha matakatifu baada ya kumpokea YESU kama Mwokozi.
1 Petro 1:15 ''bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; ''
 
3. Kwenenda kwa ROHO MTAKATIFU katika KRISTO.
Kumbuka ROHO MTAKATIFU haipatikani nje na KRISTO.

 Warumi 8:9 '' Lakini ikiwa ROHO wa MUNGU anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na ROHO wa KRISTO, huyo si wake.''

4. Kumwabudu MUNGU katika kweli yake.
Zaburi 29:1-2 ''Mpeni BWANA, enyi wana wa Mungu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu; Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu. '' 
 
5. Kuliishi Neno la MUNGU na kulitii, kumbuka KRISTO ni Neno juu ya Neno la MUNGU.
 2 Kor 8:21 ''tukitangulia kufikiri yaliyo mema, si mbele za BWANA tu, ila na mbele ya wanadamu.''

Utauwa/utakatifu/ucha MUNGU, haki na nguvu za ROHO MTAKATIFU ndio mavazi ya mteule wa MUNGU ili afike mbinguni.
Dini yeyote inayokataa Wokovu wa KRISTO huko usiende. 
Najua yako baadhi ya madhehebu mengi wanaomtukuza shetani kupitia mafundisho yao yanayopotosha watu 100% na kuna  madhehebu niliyoyashuhudia katika maeneo ambayo nimewahi kufika na kuona.
Wengi wana maroho na sio ROHO MTAKATIFU, na maroho hayo huwasaidia tu kwenye ubishi ili kutimiza matakwa ya dini na dhehebu na sio matakwa ya MUNGU.

Waebrania 4:12 ''Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.'' 

Kanisa Lazima Liwe Kanisa La Biblia. Kama Kanisa Lenu Sio La Biblia Ila Ni La Vijitabu Tu Fulani Hilo Sio Kanisa Ni Taasisi Za Watu Waongo. Na Kama Kanisa Lenu Limeibadilisha Biblia Hata Herufi Moja Hilo Sio Kanisa Bali Danguro La Shetani.
Ufunuo 22:18-20 ''Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki(Biblia), Mtu ye yote akiyaongeza, MUNGU atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
 Na mtu ye yote akiondoa lo lote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, MUNGU atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki. Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana YESU. ''

  Nimeambiwa Kuna Mtu Mmoja Siku Hizi Hamwabudu MUNGU Katika Roho Na Kweli, Nusu Nasadiki Na Nusu Sisadiki.
 Lakini Je Kwanini Kuliacha Tumaini La Uzima? 
Kwanini Kumwabudu BWANA Kwa Midomo Tu Huku Matendo Ziro?. 
Bwana YESU Yuaja Na Atamlipa Kila Mtu Kama Matendo Yake Yalivyo.
Ufunuo 22:12-13 ''Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. ''

 Uwezo Mzuri Wa Kufikiri Huzaa Uwezo Mzuri Wa Kutendea Kazi Ulichofikiri. 
Kama Ukifikiri Uzuri Wa Uzima Wa Milele Hakika Utamfuata Bwana YESU Ili Akuokoe.
 Unaweza Kuwa Kanisani Lakini Wewe Bado Ni Mateka Wa shetani Kwa Sababu Unaendeleza Dhambi. Unaweza Kuwa Kanisani Lakini Bado Ni Mateka Wa shetani Kwa Sababu Dhambi Uliyoifanya Siri, Hutaki Kuitubia. 
Unaweza Kuwa Kanisani Lakini Wewe Bado Ni Mateka Wa shetani Kwa Sababu Hujamweleza Mchungaji Hali Yako Ya Zamani Ambayo Hujaiachilia 100% Ili Akuombee Na Kukushauri. Ndugu Jifungue Leo Kutoka Katika Vifungo Vya Giza.
 MUNGU akubariki na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments