UFANYE NINI KATIKA KUUKULIA WOKOVU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
Bwana YESU atukuzwe Mteule wa MUNGU.
Karibu tujifunze somo hili ambalo
Siku moja nitachapisha kitabu kidogo cha jinsi ya kuukulia wokovu.
Kitabu hicho nitakigawa bure kwa kila mtu anayeokoka au aliyeokoka karibuni ili kimsaidie kujitambua na kujielewa kuhusu yeye katika Wokovu wa KRISTO ulio wa thamani sana.

Dondoo za somo litakalopatikana katika kitabu hicho ni hizi hapa na naamini hata leo utajifunza kitu cha thamani sana.
Kwa maamuzi yako ya kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi, ukatubu, ukamkiri YESU na kuahidi mbele ya watumishi wa MUNGU kwamba sasa utaambatana na YESU, hakika UMEOKOKA.

Warumi 10:9-11 "Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika."


Sasa wewe ni kiumbe kipya.

2 Wakorintho 5:17 "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya."


Ulizaliwa kwa Mara ya kwanza na wazazi wako wa kimwili lakini kupitia Wokovu wa KRISTO ulioupokea sasa umezaliwa Mara ya pili na MUNGU Baba.
Umezaliwa kwa Neno la MUNGU ili uishi maisha matakatifu yanayoagizwa na MUNGU kupitia Neno lake Biblia takatifu.
Waefeso 2:10 "Maana tu kazi yake(MUNGU), tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo."


Baada ya hapo sasa unatakiwa ujitambue kwamba wewe ni nani.
Je wewe ni nani?
Biblia ina majibu.
1 Petro 2:9-12 "Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya MUNGU, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la MUNGU; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. Mwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze MUNGU siku ya kujiliwa."

 
1. Wewe sasa ni uzao mteule maana umezaliwa Mara ya pili na MUNGU mwenyewe, hakikisha unaishi kama uzao mteule.
Kumbuka Neno linasema, Yohana 3:3 "YESU akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa MUNGU."


2. Wewe sasa unatokea ukuhani wa kifalme.
Fanya kazi ya MUNGU katika injili ya KRISTO.
1 Wakorintho 15:58 "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA."


3. Wewe sana ni raia wa taifa takatifu linalojumuisha wateule wa KRISTO wote duniani wanaoishi maisha matakatifu.
1 Petro 1:14-23 " Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu; bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita Baba(MUNGU), yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya KRISTO. Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini MUNGU, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa MUNGU. Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikilia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la MUNGU lenye uzima, lidumulo hata milele."


4. Wewe sasa ni mtu wa miliki ya MUNGU.
Warumi 8:1 "Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika KRISTO YESU.''
Enenda kwa ROHO MTAKATIFU tu maana ndio kanuni ya watu wa miliki ya MUNGU.
Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa Mungu, hao ndio wana wa MUNGU."


5. Wewe kabla hujaokoka ulikuwa gizani lakini  sasa uko nuruni mwa MUNGU.
Usiishi katika Giza tena Bali ishi sasa maisha yako yote katika nuru ya MUNGU ambayo ni KRISTO.
Unataka kujua ulitokaje gizani?
Biblia inakujibu.
Yohana 3:16-21 Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee(YESU), ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana MUNGU hakumtuma Mwana(YESU) ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye(YESU) hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu. Maana kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasije yakakemewa. Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika MUNGU."


Walio gizani ni wale ambao hawajaamua kuokolewa na Bwana YESU KRISTO.
Walio gizani ni watenda dhambi wote.
Wewe sasa hutakiwi kuishi katika Giza maana dhambi ni Giza.
Uko nuruni sasa maana ulikubali kuipokea nuru ya MUNGU ambayo ni YESU KRISTO.


Isaya 60:1 "Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia."


Jambo la muhimu kujua lingine ni Hakikisha umehamishwa mwili wako kutoka gizani.
Hakikisha nafsi yako imehamishwa kutoka gizani .
Na hakikisha roho yako imehamishwa kutoka gizani.


Wakolosai 1:12-14 " mkimshukuru Baba(MUNGU), aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake(YESU); ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;"


Kazi ya kukuokoa ni ya Bwana YESU lakini kazi ya kukombolewa ni juhudi yako kwa YESU.
Ndio maana unahitaji kuwa mtu wa maombi.
Unahitaji kuwa mtoaji wa zaka na sadaka.
Unahitaji kuwa mtu wa kufunga na kuomba wakati mwingine.
Unahitaji kumtii sana ROHO MTAKATIFU.

Umeokolewa kwa Neema hivyo usiitumie vibaya Neema ya MUNGU aliyokupa.

Waefeso 2:8-9 "Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu."


Hakikisha umewekwa huru kwa maombi na utakatifu.

Yohana 8:36 "Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli."


Fanya kazi ya MUNGU na timiza kusudi la MUNGU la kuokolewa kwako.

Wakolosai 1:10 "mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana(YESU), mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya MUNGU;"


MUNGU akubariki kwa kujifunza somo hili muhimu na pia Ukipenda kunisapoti kwa sadaka yako ya hiari katika huduma yangu karibu sana na pia kitabu changu cha MAOMBI YA KINA kinapatikana, tuwasiliane nitakujulisha jinsi ya kukipata.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
0786719090
mabula1986@gmail.com
Nakuomba share kwa marafiki zako ujumbe huu.

Comments