![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni sana tujifunze Neno la MUNGU.
◼️Leo tunaangalia kwa sehemu namna Bora ya kutunza Muujiza wako.
➡️Mfano Adamu alipewa Muujiza unaoitwa "Bustani ya Edeni" ili akae, ni Bustani ya MUNGU yenye vitu vizuri sana, Adamu hakuigharamikia Bustani hiyo kwa lolote ila MUNGU aliyempa Muujiza huo alimwambia Adamu ailime na kuitunza.
Mwanzo 2:15 "BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza."
◼️Hata Wewe MUNGU akikupa Muujiza ujue anataka Muujiza huo uutunze, usipoutunza Muujiza huo hautadumu hata kama aliyekupa ni MUNGU Mwenyewe.
◾Muujiza ni Nini?
◼️Muujiza ni jambo ambalo MUNGU wa Mbinguni amekutendea ambalo halitokani na maarifa Yako, uwezo wako au kitu kingine nje na MUNGU wa Mbinguni.
MUNGU ni mtenda Miujiza wetu na anapenda kutenda Miujiza.
Kutoka 34:10 "Akasema, Tazama, nafanya agano; mbele ya watu wangu wote nitatenda miujiza, ya namna isiyotendeka katika dunia yote, wala katika taifa lo lote; na watu wote ambao unakaa kati yao wataona kazi ya BWANA, kwa maana ni neno la kutisha nikutendalo."
◼️Muujiza ni mambo yaliyoshindikana kwa njia zingine zote ila Bwana YESU KRISTO Kwa sababu ni mweza yote akakutendea kwa uweza wake.
Zaburi 86:10 "Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, Wewe ndiwe mfanya miujiza, Ndiwe MUNGU peke yako."
◼️Miujiza ya MUNGU ipo mingi sana katika Maisha yetu, hata kuwa hai ni Muujiza wa MUNGU kwetu.
Mfano hai Mimi Peter Mabula naweza kusema hivi MUNGU ameniongezea kitu cha ajabu sana,
MUNGU ameniongezea cha thamani sana, MUNGU ameniongezea uhai .
➡️Je na wewe umeongezewa na MUNGU kitu hiki cha ajabu sana ambacho ni uhai?
◼️Kama ni kweli hakikisha unamtukuza YAHWEH MUNGU Muumbaji.
◼️Mtukuze yeye MUNGU na endelea kunyenyekea sana kwake huku ukimtumikia Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
◼️Miujiza ya MUNGU ipo mingi;
Kufunga Ndoa Takatifu ni Muujiza wa MUNGU, kuzaa katika Ndoa Yako ni Muujiza wa MUNGU.
Wako watu walifunga na kuomba kwa ajili ya mambo mbalimbali katika Maisha yao na Bwana YESU KRISTO akawatendea, Ndugu ni Muhimu pia kujua namna ya kuuutunza Muujiza wako.
➡️Kuna Miujiza huwa inakuja lakini haidumu kwa sababu ya makosa ya waliotendewa Miujiza hiyo.
Wengine hawajaelewa, ngoja nitoe mifano kwa ufupi.
➡️Unaweza ukapata muujiza wa MUNGU wa kununua gari, lakini ukikaa vibaya shetani anaweza akaitumia gari hiyo hiyo kukuletea ajali mbaya.
➡️Kama hujaelewa bado, ngoja nikupe mfano mwingine.
Unaweza ukapata muujiza wa kupata uzao na uzao huo huo ukaja kukuangamiza.
➡️Unaweza ukapata Mume/Mke kwa muujiza wa MUNGU Kabisa lakini ni huo huo muujiza wako unakuja kukufilisi na kukukimbia na kukuachia maumivu mabaya.
Sasa naamini sana umejua umuhimu wa kuutunza muujiza wako ambao MUNGU Baba amekupa.
◼️Mambo ya kufanya ili kutunza Muujiza wako.
1. Kuuombea muujiza wako.
Mathayo 7:8 "kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.'
◼️Uombee ulinzi Muujiza wako, Mfano umeomba upate kazi ukapata endelea kunyenyekea kwa Bwana YESU huku ukiomba ulinzi kazi Yako.
◼️Unaweza ukaomba upate Mchumba na ukapata lakini uchumba huo ukaishia njiani kwa sababu ya dhambi au kukosekana Maombi ya ulinzi.
Miujiza ya MUNGU hutunzwa.
2. Kuuweka muujiza wako kama ushuhuda aliokupa MUNGU.
Zaburi 71:17-19 " Ee MUNGU, umenifundisha tokea ujana wangu; Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo. Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee MUNGU, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako. Na haki yako, Ee MUNGU, Imefika juu sana. Wewe uliyefanya mambo makuu; Ee MUNGU, ni nani aliye kama Wewe?
◼️Yaani hakikisha siku zote anaonekana MUNGU kwamba ndiye amekupa Baraka hiyo, na mtukuze yeye hata mbele ya watu wote.
Isaya 12:5 "Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote."
3. Kwa kutoa sadaka ya shukrani huku ukimrudishia MUNGU sifa, utukufu na heshima zote.
Zaburi 116:17-18 " Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la BWANA; Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote."
◼️Kumbuka Mtu anayetoa Sadaka ya Shukrani kitendo hicho ni kumtukuza MUNGU hivyo anaweza kupata ongezeko.
Zaburi 50:23 "Atoaye dhabihu za kushukuru, Ndiye anayenitukuza. Naye autengenezaye mwenendo wake, Nitamwonyesha wokovu wa MUNGU."
4. Kuishi maisha matakatifu huku ukiwa na muujiza wako.
Ndugu tunza muujiza aliokupa MUNGU Baba.
◼️Usipoutunza muujiza aliokupa MUNGU hakika shetani anaweza kuutumia muujiza wako huo kukuonea na kukutesa.
Jitahidi kutunza muujiza wako.
◼️◼️Utunze muujiza kwa kuomba ulinzi, kumtukuza MUNGU kwa matoleo ya shukrani na kwa kumpa MUNGU heshima zote zinazotokana na muujiza huo n.k
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments