Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe rafiki.
Karibu Tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Leo tunaangalia umuhimu wa Msamaha kwa Mkristo.
Kwanza kabisa napenda kusema Neno hili "Muogope na kumuheshimu sana Mtu aliyekukosea Kisha akakuomba Msamaha"
Kwanini nasema umuogope Mtu huyo?
Ni kwa sababu Usipomsamehe na yeye amekuomba Msamaha kesi zake za rohoni zilizotokana na makosa yake kwako zinafutika na kuhamia kwako, yaani yeye anaokuwa amesamehewa na Wewe unakuwa na dhambi ya kurokusamehe, Kuna vifungo vya giza huambatana na watu wasiosamehe.
Hivyo Mtu akikuomba Msamaha akiwa amemaanisha Msamehe haraka sana isibaki tabu kwako
Luka 17:3-4 " Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe."
◼️ Ni Muhimu kujua kwamba Mtu yeyote anapotenda dhambi yeyote huwa anamkosea MUNGU lakini tabia mojawapo ya MUNGU ni kuwasamehe kabisa wanaotubu katika KRISTO YESU.
Isaya 55:7 "Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa."
◼️Kwa namna hiyo hiyo kama sisi tunaitwa Watoto wa MUNGU basi ni lazima tuwe na tabia ya kusamehe wanaotukosea.
◼️Kusamehe ni maelekezo ya MUNGU ya kudumu hivyo unayekataa kuwasamehe Wanadamu waliokukosea unakuwa unapingana na MUNGU wa Mbinguni.
➡️Kwa sababu Wanadamu wengi ni wabinafsi wasiotaka kusamehewa Neno la MUNGU limewawekea kipimo kwamba ili MUNGU awasamehe wanapotubu basi na wao lazima wawe wamewasamehe waliowakosea.
Mathayo 6:14-15 " Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na BABA yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala BABA yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu."
◼️Mtu asiyewasamehe watu hawezi kusamehewa na MUNGU na Mtu ambaye hatasamehewa na MUNGU hawezi kwenda Uzima wa Milele.
◼️Kanisa la YESU KRISTO linatakiwa liambatane na kusameheana.
◼️Mtu aliyeokoka aliyekua kiroho huwa ni mtu wa kusamehe na kuachilia waliomkosea.
◼️Mkristo safi anayejitambua huambatana na kusamehe waliomkosea.
◼️Mtu aliyekomaa kiroho ni lazima pia awe mtu wa kuwasamehe wenzake.
◼️Viongozi wa Kanisa wanaojitambua ni lazima wawe ni watu wa kusameheana na kusahau pale wanapokosewa.
◼️Mchungaji mzuri wa kondoo huwasamehe kondoo wake wanaomkosea, huwakaribisha zizini na kuwajali.
◼️Msamaha ni jambo muhimu sana kwa watu wa MUNGU.
Waefeso 4:32 " tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na MUNGU katika KRISTO alivyowasamehe ninyi."
✔️✔️Na unapowasamehe wanadamu waliokukosea inakubidi ujichunguze kama kweli umesamehe au bado hujasamehe.
➡️Kusamehe ni Nini?
◼️Kumsamehe Mtu aliyekukosea ni kumfutia rohoni deni la kosa.
◼️Msamaha ni kuhurumia kisha unaachilia.
◼️Msamaha ni pendo la upendo.
◼️Msamaha ni upendo usiohesabu mabaya Bali huyafuta.
◼️Kusamehe ni Kanuni ya kawaida kabisa ya kimaisha kwa watu wa MUNGU waliokolewa na Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
Marko 11:25-26 " Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na BABA yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi hamsamehe, wala BABA yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]"
➡️Msamaha wa kweli huleta toba ya kweli.
◼️Msamaha huwatoa moyoni wale uliokuwa umewabeba moyoni.
◼️Msamaha ni mlango wa kukaribisha baraka za MUNGU katika Maisha yako.
◼️ Msamaha na ni mlango wa kumfukuza shetani ili asitumie kutokusamehe kwako kama fimbo ya kukuchapa maana mbele za MUNGU utakuwa na hatia ya kutokusamehe.
2 Wakorintho 2:10-11 " Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za KRISTO, Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake."
➡️Usikupokuwa mtu wa kusamehe ujue kuna baadhi ya baraka za MUNGU hutazipata.
◼️Hakikisha unakuwa mtu wa kusamehe, kuachilia na kusahau.
◼️Maana mojawapo ya Neno kusamehe ni mtu kuondoa uchungu ulioingizwa moyoni na yeye mwenyewe baada ya kuchukizwa
◼️Mkristo yeyote anatakiwa kuwa mtu wa kuwasamehe wengine na kujitenga na dhambi.
➡️Kusamehe sio kuvumilia bali ni kumfutia mtu hatia na kumwachilia.
◾Kwanini tusamehe?
◼️Ni kwa sababu tunaposamehe ni kwa faida yetu wenyewe.
Wakolosai 3:13-14 " mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama BWANA alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu."
◼️Ni kwa sababu MUNGU ametuagiza kuwa watu wa msamaha kwa wanadamu wenzetu wanaotukosea.
◼️Kama vile ambavyo sisi tunapomkosea MUNGU huwa tunaomba msamaha na yeye anatusamehe, basi inatupasa na sisi tuwe watu wa kusameheana.
◼️Mtu anayemwendea YESU KRISTO na akatubu toba ya kweli hupokea msamaha pale pale, MUNGU kama muumbaji hutusamehe sisi tunapotubu hivyo hata sisi inatupasa kuwasamehe ndugu zetu, marafiki zetu, wapendwa wetu na watu wote wanaotukosea.
◼️Msamaha ni Kanuni inayotakiwa kuwa Kanuni yako Mteule wa MUNGU.
Mathayo 18:21-22 " Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
YESU akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini."
◼️Ndugu hakikisha unakuwa mtu wa msamaha na kuachilia.
Asante kwa kujifunza Neno la siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka au uliokoka ukarudi nyuma, nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments