ULIMI NI HATARI SANA

 

Na Mwl Peter Mabula, Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO 


Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote. 


Siku chache zilizopita ROHO MTAKATIFU aliniambia kwamba nifute maneno yote mabaya niliyotamkiwa na watu haijarishi ni watumishi wa MUNGU au mtu yeyote lakini kama aliwahi kuninenea jambo baya ina maana jambo hilo bado lipo linanifuatilia hivyo nifute maneno yote mabaya niliyowahi kutamkiwa  nikafanya hivyo katika maombi.


Na  kwa sasa ni utaratibu wangu kufuta maneno yote mabaya ninayonenewa.


Ndugu, ufunuo huu husika nao pia na wewe, futa kila neno baya ulilonenewa na mtu yeyote hata kama ni wazazi, futa kwa jina la YESU KRISTO.


Neno la MUNGU linasema '' Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.-Ayubu 5:21''


Hapo tunajifunza kwamba kumbe kuna mapigo ya ulimi lakini pia kumbe yupo MUNGU atakayetushindia. 


Lakini MUNGU atatushindia tu kama tuko upande wake.


Ashukuriwe Bwana YESU KRISTO aliyekuja kutupa uzima kisha uzima tele, yaani alikuja kutupa uzima sana na kisha uzima wa milele.(Yohana10:10b)


Mtumishi wa MUNGU anasema ''Adui zangu

wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake likapotea?-Zaburi 41:5''


Hata wewe ndugu inawezekana wapo watu wengi wanaokuzika huku ukiwa hai.


Inawezekana wapo watu wanaokunenea mabaya ya kukua kila siku.


Inawezekana wapo watu  wanaokuendea kwa waganga ili tu ufe au usifanikiwe.


Inawezekana wapo watu wanaotamani ufe ili washangilie kisa tu wewe ni mtumishi wa MUNGU.


Inawezekana Wapo watu  wanaotamani ufe ili wachukue nafasi yako kazini maana wewe ni mkuu wao wa kazi. 


Hizo zote ni nguvu za kaburi, mkimbilie Bwana YESU KRISTO  leo ili uwe salama. 


umeijua siri hii mkimbilie Bwana YESU  KRISTO  leo na utakaa salama.


''Amemeza mauti hata milele; na BWANA


MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.-Isaya 25:8''


Ni ahadi nzuri sana ya MUNGU kwako.

Hata kama wachawi waliwaza mauti

 kazini kwako au kwenye afya yako

lakini ukienenda katika Bwana YESU utakaa


salama, maana  mfano kama watakunenea mabaya kwa miezi 7 lakini una uwezo wa kuyafuta maneno yao kwa dakika 1 tu kwa maombi kupitia jina kuu la YESU KRISTO.

Ndugu omba na MUNGU akubariki sana. 

By Peter Mabula. 

Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi. 

+255714252292

Ubarikiwe

Comments