![]() |
| Na Mwl Peter Mabula Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi |
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe Ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU wa Mbinguni.
◼️Usitoe sadaka kwa majini Wala usitoe sadaka Yako kwa waabudu shetani.
Walawi 17:7 "Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi."
◼️Katika Sheria ya Neno la MUNGU hii ni Sheria ya milele ndivyo Biblia inavyosema hapo juu, yaani Mwanadamu mwenye akili timamu kamwe huruhusiwi kutoa Sadaka zako kwa majini Wala kwa Waabudu shetani.
Maana yake kumbe wako watu hutoa sadaka kumbe wanatoa kwa majini ndio maana Neno la MUNGU wa Mbinguni linakataza kufanya ujinga huo wa kutoa Sadaka kwa majini, hivyo sehemu yeyote inayojihusisha na majini tambua kabisa ukipeleka Sadaka zako huko mbele za MUNGU utakuwa unatoa sadaka kwa majini na sio MUNGU.
➡️Majini ni Nguvu za giza hivyo usitoe sadaka zako kwa kwa Nguvu za giza, huko utaambulia vifungo vya kiroho tu na mateso yanayotokana na shetani, toa Sadaka zako kwa MUNGU wa Mbinguni ambalo huko utaambulia ulinzi wa MUNGU na baraka.
Kumb 32:17 "Walitoa sadaka kwa pepo, si MUNGU, Kwa miungu wasiyoijua, Kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu, Ambayo baba zenu hawakuiogopa."
◼️Mawakala wa shetani ni watu wote waliomkataa YESU KRISTO kuwa Mwokozi wao, hao wako upande wa shetani ndio maana tunawaita mawakala wa shetani.
Yohana 3:36 "Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya MUNGU inamkalia."
◼️Mawakala wa shetani huabudu Miungu huko kwenye Ibada zao huwa kunatolewa sadaka ambazo ni machukizo kwa MUNGU maana hawamwabudu yeye.
Kumbu 8:19" Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka."
✓✓Ndugu, Sadaka zako toa katika MUNGU wa Mbinguni kule anakoabudiwa katika KRISTO na katika Roho na kweli.
Kumbu 12:11-12 "wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA. Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi, na wana wenu, na binti zenu, na watumishi wenu wanawaume na wanawake, na Mlawi aliyemo malangoni mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu."
➡️Sadaka kwa majini kiroho itakufanya uwe umefanya uasherati na hayo majini, ni hatari sana.
Walawi 17:7 "Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi."
➡️Sadaka kwa majini itakufanya uingie Agano la kishetani litakalokitesa.
◼️Ndugu, zingatia Neno la MUNGU linaposema "Usitoe sadaka kwa majini "
➡️Unaweza ukatoa sadaka kwa shetani kupitia Watumishi wake na kwa njia hiyo unakuwa umekabidhi kizazi chako kwa shetani.
Zaburi 106:37 "Naam, walitoa wana wao na binti zao Kuwa dhabihu kwa mashetani."
◼️Ndugu, toa Sadaka zako kwa Watumishi wa kweli wa Bwana YESU KRISTO.
✓✓Kumbuka Mwanadamu ameumba katika hali ambayo hawezi kuepuka kutoa Sadaka maana sadaka ni Ibada hivyo Ukiona Mtu hawezi kutoa Sadaka kwa MUNGU wa Mbinguni ujue Mtu huyo hutoa kwa shetani kupitia kwenda kwa waganga, kubet, kulipia gesti ili azini n.k
◼️Hivyo ni heri sana ndugu ukaamua kuwa wa KRISTO na Sadaka zako za hiari toa kwa MUNGU kupitia Watumishi wake ambao rohoni mwako utashuhudiwa ni Watumishi waaminifu katika KRISTO YESU Mwokozi.
◼️Ndugu ongozwa na ROHO MTAKATIFU katika utoaji wa baadhi ya sadaka kama unataka ufanikiwe katika Maisha Yako.
Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."
Asante kwa kujifunza Neno la MUNGU siku ya leo, Kabla sijamaliza nakuomba Wewe ambaye hujaokoka nakusihi sana amua Leo kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako na Jina lako litaandikwa katika kitabu Cha uzima Mbinguni, katika maeneo Yako tafuta Kanisa safi la kiroho linalohubiri Wokovu wa KRISTO YESU nenda kamweleze Mchungaji atakuongoza Sala ya Toba utaokoka Kisha baada ya hapo fuata mafundisho ya Neno la MUNGU hapo Kanisani.
MUNGU wa Mbinguni akubariki sana.
By Mwl Peter Mabula
Mtenda kazi katika Shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi.
+255714252292 ( kwa Ushauri, maombezi, pamoja na Whatsapp)
Ubarikiwe

Comments