JITENGE NA IBADA YA SANAMU





FARAO MFANO MZURI YA WATU WALIOKUWA WANAABUDU SANAMU KWA MUJIBU WA BIBILIA
mpendwa msomaji wa maisha ya ushindi nakukaribisha katika mafundisho haya ya kuhusu kujitenga na ibada ya sanamu, Katika 1Yohana :21 Biblia inasema ''Watoto wadogo jilindeni nafsi zenu na sanamu''. hivyo ni machukizo mbele za MUNGU sisi watoto wake tuliompa BWANA YESU maisha yetu kujihusisha na sanamu na ndio maana MUNGU aliwaambia waisraeli alipokuwa anawatoa misri akiwapeleka kaanani kwamba  ''Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki,juu ya milima mirefu, na juu ya vilima na kila chini ya kila mti wenye majani mabichi. Ujiangalie usije ukanaswa ukawafuata....'Kumbukumbu la torati 12:2,30a,31.Ndugu Bibilia inakataza kuabudu sanamu na nakuomba usihusike na sanamu kwa vyovyote vile kwani ni dhambi kama zilivyo dhambi zingine.Na waabudu sanamu Biblia inasema hivi juu yao Warumi 1:25 {Kwa maana waliibadili kweli ya MUNGU kuwa uongo wakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya MUUMBA anayehimidiwa milele.Amina}. Ndugu hakuna haja ya kuabudu sanamu wala kuhusika na waganga wa kienyeji wala waaguzi au wapunga pepo na kila aina ya unajimu kwani na uchawi kwani MUNGU anasikia maombi yako popote ulipo na   Biblia inatuambia katika Zaburi 115:3-8 kuwa ''Lakini MUNGU wetu yuko mbinguni, alitakalo lote amelitenda .Sanamu zao ni fedha na dhahabu kazi ya mikono ya wanadamu. Zina vinywa lakini hazisemi, zina macho lakini hazioni zina masikio lakini hazisikii harufu, zina mikono lakini hazishiki , miguu lakini haziendi wala hazitoi sauti kwa koo zake. Wazifanyao watafanana nazo.na kila mmoja anayezitumainia''. ndugu ambaye hujaokoka kumbuka wakati wa wokovu ni sasa na achana na kuabudu sanamu na Biblia inatuambia kuwa ''..... ikimbieni ibada ya sanamu.Sivyo lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani wala si kwa MUNGU nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani.Hwamuwezi kunywea kikombe cha BWANA na cha mashetani 1 Korintho 10:14b na 20. MUNGU BABA akubariki sana ila kumbuka MUNGU hahitaji kuhusishwa na chochote bali yeye anajibu maombi bila hata kupitia sanamu na kumbuka jinsi alivyosikia maombi ya Nabii Yona akiwa ndani ya tumbo la samaki baharini lakini aliomba na MUNGU alisikia na akamwamuru samaki amtapike Yona.Mwisho kumbuka ndugu Biblia inasema kuwa siku ya hukumu waabudu sanamu wataenda jehanamu  ''Waabudu sanamu sehemu yako ni katika ziwa la moto'' Ufunuo 21:8b. MUNGU akubariki sana na kama hujampa BWANA YESU maisha yako awe BWANA na MWOKOZI wako fanya hivyo leo .
WENGINE HUABUDU WANYAMA AU SANAMU ZA WANYAMA HII NI DHAMBI MBELE ZA MUNGU
sanamu kubwa kuliko zote iliyopata kutengenezwa iliyopo Rio de janeiro nchini Brazil

Comments