JE SIKU SAHIHI YA KUABUDU NI SIKU GANI?



Neno la MUNGU ndilo lenye ukweli wote.
ndugu nimesoma lakini napenda utambue kuwa katika BIBLIA MUNGU amefanya maagano makuu mawili na wanadamu la kwanza MUNGU alifanya agano na wana wa Israel kupitia Musa KUTOKA 24:4-8 {...........  Musa akatwaa nusu ya ile damu ..... kisha akakitwaa KITABU cha agano akakisoma masikioni mwa watu .......Musa AKAITWAA ILE DAMU AKAWANYUNYUZIA WATU AKASEMA HII NDIO DAMU YA AGANO ALILOFANYA BWANA PAMOJA NANYI KATIKA MAMBO HAYA YOTE} tunaposema agano maana yake ni mapatano kwa hiyo mmoja kati ya walioweka agano akilivunja kuna kuwa na maamuzi mengine, hawa wana wa Israel walivunja agano WAAMUZI 2:11,20 [Wana wa israel walifanya yaliyokuwa maovu machoni mwa BWANA nao wakawatumikia mabaali] katika mstari wa 20 MUNGU mwenyewe anatangaza kuvunjika kwa agano {Basi hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israel naye akasema kwa kuwa taifa hili wamelihalifu agano langu nililowaamuru baba zao wala hawakuisikiliza sauti yangu} kumbuka katika agano hili la MUNGU na wana wa Israel MUNGU aliwapa Amri 613 na Amri 10 za msingi ili waenende na kuishi kwa hizo lakini wakavunja na baada ya hapo MUNGU kupitia  manabii akasema atafanya agano jingine au agano jipya tusome katika YEREMIA 31:31-33 {Angalia siku zinakuja asema BWANA nitakapofanya AGANO JIPYA na nyumba ya Israel na nyumba ya yuda si kwa mfano wa agano lile nililofanya na baba zao  katika siku ile nilipowashika mkono ili kuwatoa katika nchi ya misri  AMBALO AGANO LANGU HILO WALILIFUNJA ingawa nalikuwa mme kwao asema BWANA .....................} Pia  MUNGU akasema kupitia EZEKIELI 36:26-27 {Nami nitawapa ninyi moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani yenu  nami nitatoa roho ya jiwe iliyokua ndani yenu........]  ndugu kumbuka kile kitendo alichofanya Musa katika KUTOKA 24:8 na linganisha alivyofanya BWANA YESU katika MATHAYO 26:28 {Kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ongoleo la dhambi}  pia soma ZAKARIA 9:11 hivyo ndugu hapo nilikua nakutofautisha kati ya agano la kwanza na la pili na kila agano lilikua na taratibu zake ikiwemo hiyo ya sabato yaani siku ya jumamosi na tukiangalia vitu vingi tu vimebadirika mfano sadaka za kuteketezwa na mengine mengi na ukisoma WAEBRANIA 7:22{Basi kwa kadri hii YESU amekua mdhamini wa agano lililo bora zaidi} Pia soma WAEBRANIA 12:24 . ndugu mpendwa kiukweli kuabudu siku yeyote ni sawa  pia wengine hutumia  kigezo kwamba YESU aliabudu siku ya sabato hiyo ni kweli kwa sababu  alizaliwa chini ya sheria WAGALATIA4:4{Hata ulipowadia utimilifu wa wakati  MUNGU alimtuma mwanae ambaye amezaliwa na mwanamke, AMEZALIWA CHINI YA SHERIA} pia kumbuka kuwa Agano jipya lilianzia Golgota pale msalabani YESU aliposema IMEKWISHA  ila kumbuka jambo moja usije ukasahau kwa maana  watu wengine kwa kuielewa vibaya BIBLIA wanadhani agano la kale yaani maandiko ya agano la kale hayatakiwi kutumika kwani lilifutwa lakini si kweli kilichobadilika hapo ni mapatano kati ya MUNGU na wanadamu na kumbuka popote pale kwenye maelezo haya nilipotumia neno AGANO LA KALE au AGANO JIPYA simaanishi vile vitabu 39 vya agano la kale au vile vitabu 27 vya agano jipya bali mapatano kati ya MUNGU na waisrael kupitia Musa na mapatano mapya ya MUNGU kwa wanadamu kupiti BWANA YESU Hivyo vitabu vyote vya Biblia  bado vinatumika na vitatumika siku zote hadi kurudi kwa YESU. Nikirudi kwenye swali lako la kuhusu siku ya kuabudu tambua ya kwamba unaruhusiwa kuabudu siku yeyote ndio maana kuna makanisa wana ibada jumapili wengine jumatano jioni na kwa wiki nzima ibada zinaendelea kwani jumatatu inaweza kuwa siku ya wamama hivyo kuna kuwa na ibada ya wamama ,jumanne siku ya vijana hivyo kuna kuwa na ibada ya vijana hivyo siku zote ni sahihi kabisa kuabudu ndio maana katika WAKOLOSAI 2:16-17  Biblia inasema mtu asiwahukumu ninyi kwa sababu ya sabato.pia soma WAGALATIA 4:9-11.  MUNGU BABA akubariki sana na umeuliza swali zuri sana ili pia ujumbe huu uwasaidie na wengine ambao watausoma na kujifunza kitu.Amen  {haya yalikuwa ni sehemu ya majibu kwa ndugu Danald kazole kutoka maisha ya ushindi alipo uliza shwari la kwanini baadhi ya Wakristo hawafuati sabato?} hata wewe unaruhusiwa kuuliza swari au kutoa maoni ya kibiblia kuhusu shwari hili katika blog hii au katika www.facebook.com/MaishaYaUshindi.

Comments