UONGOZI WA MAKANISA TANGA WATOA TAMKO

BWANA YESU pekee ndie anaweza kutuweka huru mbali na dhambi pia yeye ndiye pekee anaweza kutufikisha kwenye uzima wa milele {YOHANA 14:6, MATENDO4:12}



MOJA YA KANISA LILILOCHOMWA MOTO MBAGALA SIKU ZA KARIBUNI
Uongozi wa makanisa mkoani Tanga umelitaka jeshi la polisi kuchukua hatua kali kwa kuwakamata wale wote waliotaka kuchoma makanisa jana na kusema maombi yao tu kwa MUNGU ndio yameokoa makanisa kuchomwa moto,Akizungumza na wandishi wa habari Askofu Josan Mwakimage amesema kuwa maombi yao tu ndio yamesaidia watu hao wenye nia mbaya na kanisa kushindwa kufanikisha lengo lao.Naye Mchungaji James wa kanisa la Anglican Makolola amesema  jeshi la polisi lichukue hatua kwa wahusika wote.
NIMEYASIKIA MAOMBI YAKO NA NIMEYAONA MACHOZI YAKO {ISAYA 38:5} JEHOVAH ANAWEZA YOTE.
Pia viongozi hao wamekemea sana kitendo cha mtoto katika kijiji cha Mwakijalo kukojolea BIBLIA TAKATIFU na kusema uchunguzi ufanyike juu ya tukio hilo.

Comments