FAIDA 11 ZA MAOMBI YA KUFUNGA.

 

Na Mwl Peter Mabula 



Bwana YESU KRISTO  atukuzwe ndugu yangu.

Karibu tujifunze kuhusu maombi ya kufunga tunapojiandaa kufunga siku 3 kuanzia kesho.

Kufunga ni nini?

■Kufunga Ni Utii Wa Kujitoa Kwa Ajili Ya BWANA MUNGU, Ili Kwamba, MUNGU Aweze Kutenda Kupitia Wewe Yale Ambayo Asingeweza Kutenda Kama Usingefunga.

●Maombi Ni Mawasiliano Ili Bwana YESU Atende Kwako Yale Ambayo Yasingetendeka Kama Usingeomba.

Maombi ya kufunga ni muhimu sana katika maisha ya wakristo.

Wakristo hawafungi mara moja kwa mwaka, bali inawezekana kabisa mkristo anaweza kufunga hata mara 100 kwa mwaka, na ndio wengi walioshinda wanavyofanya.
Matendo  13:3 "Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao."

Maombi ya kufunga ni muhimu sana kwako ila hakikisha hufungi ili kuwaridhisha watu fulani.

Usifunge ili uonekane wa kiroho bali funga ili ujibiwe mahitaji yako.

Usifunge ili kuwaonyeshea watu.

Maombi mazuri pia ni lazima yaambatane na utakatifu.

Watu Wengi Hutaka MUNGU Awabariki Kiuchumi Huku Utakatifu Kwao Ni 0.001% Yaani Wana Utakatifu Wa Ndani Ya Ibada Tu, Wakitoka Ibadani Wanaendelea Kuwa Watoto Wa Shetani.
Ndugu, Hata Kama Ukivipata Vyote Uvitakavyo Lakini Kama Utakufa Dhambini Ni Hasara Kwako.

Hivyo jambo muhimu zaidi ni utakatifu kisha maombi.

1 Petro 1:15 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;''

Kufunga ni jambo la muhimu sana maana lina faida kuu kwa anayefunga.

Wakristo wote wanatakiwa kuwa watu wa maombi yakiwemo maombi ya kufunga.

Kufunga Sio Karama Hata Useme Huwezi Kufunga kwa kisingizio kwamba kufunga Sio Karama Yako.
Kufunga Hakumo Ndani Ya Karama Za MUNGU Kwetu bali ni agizo jema kwetu.

■Maombi Ya Kufunga Ni Kufungua Pale Pasipoweza Kufunguliwa Kwa Njia Ya Kawaida.

Ndugu, Usiache Kufunga Kwa Madai Kwamba Huna Karama Ya Kufunga.
1 Thesalonike 5:17 ''ombeni bila kukoma;''

Kuna faida kuu katika maombi ya kufunga.

Ni Kweli wakati huu kwako Unaweza Kuwa Ni Wakati Wa Ukame, Lakini Mvua Ya Baraka Itanyesha Hivi Punde baada ya kuomba kwa imani maombi ya kufunga.

Hata Kama Kulikuwa Na Ukame Kiuchumi au katika uzao au katika ndoa au katika kibali au kazi, Kwa Muda Mrefu Lakini Kwa Kumwita Bwana YESU Hakika Mvua Ya Baraka Inaenda Kunyesha.

Maombi Ni Maisha.
Maombi ya kufunga Ni Mkono Mrefu zaidi Wa Kupokea kutoka kwa MUNGU.
Biblia Inasema Kama Huombi Wewe Huna Hitaji.

Kwa YESU Tunaomba Na Kupokea.

''Matofali Yameanguka, Lakini Sisi tutajenga Kwa Mawe Yaliyochongwa; Mikuyu Imekatwa Lakini Sisi Tutaweka Mierezi Badala Yake.-Isaya 9:10.

Nampenda YESU Maana Anatengeneza Vitu Imara Zaidi Kuliko Nilivyowaza.

 Nampenda YESU Maana Yeye Ataleta Baraka Ambayo Ni Imara Na Ya Kudumu, lakini kama tu tukidumu katika utakatifu pamoja na kudumu katika maombi yakiwemo na maombi ya kufunga.

''Utafichwa Na Mapigo Ya Ulimi; Wala Usiogope Maangamizo Yatakapokuja-Ayubu 5:21''.

Ndugu, Inawezekana  kuna Mapigo Ya Ulimi Yalielekezwa Kwako wakati fulani, Mapigo Hayo Ni Maneno Mabaya Unayonenewa Na Watu Wabaya. 
Wanakunenea Magonjwa, Wengine Kwa Vinywa Vyao Wanataka Usipokee Baraka Yako.
Mpendwa, Ulimi Una Mapigo Na Unapiga Ndio Biblia Inavyosema Hapo Juu.

 Maombi yatabatilisha mipango mibaya yote,  Juu Ya Hili, unaweza ukayapeleka Golgotha Maneno Mabaya Uliyonenewa Na Kupangiwa Na Watu Wabaya,  na unarudi Ukiwa Huru.

Fanya maombi yako kwa imani na kwa kufunga na kuomba.

 Faida 11 za Maombi ya kufunga.


1. Kufunga kunasaidia kukua kiroho.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Inawezekana kabisa umekuwa ni mtu wa kudumaa tu kiroho, umejitahidi kwa nguvu zako na akili zako ili ukue kiroho lakini umeshindwa. Neno la MUNGU linasema kwamba mengine huwa yanawezekana tu pale ambapo wewe utakuwa unafunga na kuomba.

 Tatizo la uchanga wa kiroho linaweza likatoka tu kwako pale ambapo utakuwa unafunga na kuomba na utakatifu maana utaona miujiza ambayo MUNGU atatenda kupitia Maombi yako hivyo imani yako itaongezeka, huko ndiko kukua kiroho

2. Kufunga kunakufanya uwe msikivu zaidi wa kuisikia sauti ya MUNGU.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Kuna watu ni ngumu kwao kuisikiliza sauti ya MUNGU.

Kuna watu makali yao ya rohoni hayajanolewa hata waweze kuwa wanaona mambo makubwa ya ki-MUNGU.

Tatizo kama hilo wakati mwingine litaondoka baada ya wewe kuwa unafunga na kuomba.

Tatizo halitaondoka kwako wakati mwingine mpaka kwa kufunga na kuomba.

3. Kufunga kunakusaidia kuutiisha mwili wako.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Japokuwa maombi yana nguvu sana lakini naomba ujue kwamba maombi ya kufunga yana nguvu  zaidi.

Kuna watu miili yao inawatumikisha katika dhambi.

Kuna wanaume akiona tu sura ya mwanamke basi hawezi kujizuia kumtongoza, ni pepo hilo lakini kwa maombi ya kufunga na utakatifu hakika pepo hilo litaondoka.

Kama mwili wako unakusumbua katika dhambi mbali mbali kama uzinzi, uongo, tamaa mbaya n.k nakuomba anza kuwa mtu wa kufunga na kuomba maana mwili wako sasa utaenda kuitii roho yako. Mwili ni dhaifu sana lakini maombi ya kufunga yanaweza kuutiisha mwili wako hata usiweze kukuwashawasha tena pindi uonapo mtu wa jinsia tofauti na yako.

 4. Utamruhusu ROHO MTAKATIFU kukutumia.

1 Kor 12:11 ‘’ lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. ‘’
-ROHO MTAKATIFU humgawia kila mtu huduma kama atakavyo yeye ROHO lakini wakati mwingine huduma unayo lakini haiendelei kwa sababu huombi ndio maana Bwana YESU akasema '' Mengine yatawezekana kwa wewe kufunga na kuomba- Mathayo 17:21''

-Maombi ya kufunga ni muhimu sana na inakuwa rahisi zaidi ROHO MTAKATIFU kukutumia maana hata wewe unakuwa rohoni.

-ROHO pia anaweza kukutumia kwa maombi.

Warumi 8:26-27 ''Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya ROHO ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo MUNGU''

5. Kufunga husababisha ushindi kwako dhidi ya ngome za shetani.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Kuna ngome zingine za adui kuzibomoa kunahitajika nguvu kubwa sana ya MUNGU.

Inawezekana unashindana na wachawi.

Inawezekana unashindana na mwanamke alikuendea kwa waganga ili tu akunyang'anye mume wako wa ndoa.

Inawezekana kuna mtu anakuroga ili ufukuzwe kazi.

Inawezekana kuna mganga amekufunga ufahamu wako hata hujielewi.

Inawezekana kabisa unapambana na mizimu au majini.
Ndugu yangu, yote hayo au moja katika hayo na mengine mengi unayoyajua mwenyewe, ili kuyashinda kunahitajika nguvu kubwa zaidi. Mengine hayawezi yakatoka hadi baada ya wewe kufunga na kuomba, ndivyo Biblia inavyosema hapo juu kwamba mengine hutoka tu hadi pale utakapofunga na kuomba.

6. Kufunga kunakuongezea mamlaka ya kiroho.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Wenye nguvu nyingi za rohoni ni wale waliokaaa katika kusudi la MUNGU.

Wenye nguvu nyingi za rohoni ni wale waombaji, wanaoomba kwa imani na kufunga pamoja na utakatifu.

Kama unataka kuongeza mamlaka yako kiroho katika Bwana YESU hakika pia unatakiwa kuongeza maombi ya kufunga pamoja na utakatifu sana na kujifunza Neno la MUNGU na kulishika.

7. Kufunga kunakupa nguvu mpya ya kiroho.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

Nilipojua siri hii nilifanikiwa sana kiroho.
Kuna wachungaji wengi leo hata huwatuhumu wachungaji wenzao kwa sababu wanaombea watu wanapona lakini wao hawawezi, kumbe tatizo ni kupungukiwa na maombi ya kufunga na utakatifu.

Nguvu mpya rohoni zinaweza kuja kwako baada ya maombi ya kufunga na kuomba na utakatifu.

 8. Kimwili:Kufunga kunasababisha uponyaji wa wa mwili

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

- Hata katika mambi ya kimwili, kufunga kuna faida sana.

 Kufunga kunaweza kukuasaidia kupunguza mafuta mwilini yasiyohitajika, yanayoweza kukuletea magonjwa n.k

-Kufunga kunaweza kukusaidia kuondoa uchafu katika mwili wako.

9. Kimwili: Kufunga kunaweza kukusaidia kuepuka kifungo cha ulafi.

Mathayo 17:21 ''Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.''

-Ulafi sio jambo zuri hata kidogo.
-Biblia inaataza wakristo kuwa walafi.
-Njia mojawapo ya kuusaidia mwili wako kuepukana na ulafi ni kufunga.

Baada ya maombi ya kufunga tumbo hupungua na chakula unaweza kuwa unakula kidogo tu na kushiba, hiyo ni faida nzuri ya maombi katika mwili wako.

10. Macho yako ya ndani yatakuwa yanaona vizuri.

Zaburi 119:18 ‘’ Unifumbue macho yangu niyatazame Maajabu yatokayo katika sheria yako. ‘’

-Mambo mengine ya kiroho kuyajua ni lazima ufumbuliwe macho ya rohoni ndipo utaona na kujua.

-Kuna vitu vingi sana mimi Peter Mabula ambavyo sikuwahi kuvijua wala kuviona lakini baada ya maombi ya kufunga niliona na kushangaa sana.

-Biblia inaposema kwamba ''Unifumbue macho yangu nitazame'' maana yake mwanzo hakuweza kutazama na kuelewa hata kama macho anayo ila macho ya ndani yalikuwa yamezibwa ndio maana hakuona, na katika hilo tunarudi pale pale kwamba ''Mengine yatawezekana tu baada ya kufunga na kuomba''

-Maombi ya kufunga yatafungua macho yako ya ndani na na utaona hata maadui walio sirini ambao wamekutesa kwa muda mrefu

11. Kupokea maana ni ahadi ya MUNGU kujibu maombi yako.

Yeremia 29:13 ‘’Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.'' 

Tena Biblia inasema ''Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;-M
athayo 7:7'' 

na kwa sababu MUNGU analiangalia neno lake alitimize basi hata aliposema tuombe ni hakika atajibu maana yeye hajipingi na Neno lake, labda tu sisi tuombe vibaya na tupungukiwe na imani katika maombi yetu.
1 Yohana 5:14-15 ''Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.''

-Maombi ya kufunga ni mkono mrefu wa kupokea kutoka kwa MUNGU.

Waebrania 4:16 ''Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. "
Naamini umejifunza kitu hivyo utakuwa na juhudi sana katika Maombi ya kufunga.
MUNGU akubariki sana. 
By Peter Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.
+255714252292.
Ubarikiwe sana

Comments