FAIDA 10 ZA KUMTII MUNGU



Faida 10 za Kumtumikia MUNGU;
Kutoka 23: 25-29

1. Atabariki Chakula Chako
2. Atabariki Maji yako
3. Atakuondolea ugonjwa katikati yako
4. Hapatakuwa na Mwenye Kuharibu Mimba
5. Ataondoa Utasa
6. Hesabu za siku zako ataitimiza
7. Atatuma Utiisho wake mbele yako
8. Atawafadhaisha maadui wote wakufikirio
9. Adui zako watakuonyesha maungo yao yaani watadhalilika.
10. Atapeleka mavu mbele yako; watakao mfukuza Mhivi, na Mkaanani na Mhiti wote watoke mbele yako(Mhivi,Mkaanani na mhiti ni tawala za shetani)
Kutoka 23:25-29 ''Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza. Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao. Nami nitapeleka mavu mbele yako, watakaomfukuza Mhivi, na Mkanaani, na Mhiti, watoke mbele yako.''


Je unamtumikia MUNGU kwa nini?
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuhubiri.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuishi maisha matakatifu.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa matoleo yao kwenye kazi ya MUNGU.
Kuna wanaomtumikia MUNGU kwa kuombea watumishi na Kanisa n.k
Je wewe unamtumikia MUNGU kwa nini?


Mwisho tambua kwamba Ukimtumikia YESU KRISTO hakika MUNGU atakuheshimu.
Yohana 12: 26 ''Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba(MUNGU) atamheshimu. ''

MUNGU akubariki sana kama hujampa YESU maisha yako basi fanya hivyo leo maana saa ya wokovu ni sasa na Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu pia zingatia kwamba hakuna uzima wa milele kwingine nje na kwa BWANA YESU {Yohana 14:6}
MUNGU akubariki sana.

Comments

James said…
Hakika Mungu ni mwema. Kila wakati anawaza jinsi atakavyotubariki. Mungu akubariki brother Peter.
Peter Mabula said…
barikiwa sana mtumishi wa MUNGU, hata hivyo ikiwezekana kama utapata nafasi naomba tuonane kuna mambo unisaidie na kunishauri pia kuna marekebisho fulani ninataka niyafanye kwa msaada wako