KAMA UNATESEKA NA MAPEPO NA NDOTO ZA KULA CHAKULA NDOTONI NENDA KANISANI UKAOMBEWE NA UTAKUWA HURU KWA JINA LA YESU KRISTO |
Nini maana ya kulishwa Chakula ndotoni
Wachawi wapo na wanapenda kazi duniani, mfano kwenye vikao vyao usiku
wanajadili mambo ya kuwafanyia watu baada ya mashaka kutumwa.. Duniani
wachawi hata kuvaa vizuri ni sababu tosha kukuangamiza na hapo Jina lako
linakuwa limeshakuwa kwenye vikao vya kichawi.
Kwenye
biblia kuna vyakula vya aina mbili 1 kor 10: 1-3. chakula cha kutoka
mbinguni chakula cha roho , Yohana 6 Yesu anasema " Mimi ni chakula
kitokacho mbinguni" na chakula cha Kutoka chini, majini. Limetoka
kuzimu. Ni muhimu kujua kuna chakula cha kiroho na chakula cha kimwili,
chakula cha kutoka mbinguni na chakula cha Kutoka kuzimu.
Kwahiyo
wachawi wanapokuwekea shetani wa balaa au wa mikosi ndani yako, Zakaria
3:1 shetani anaweza kukaa ndani ya mtu au karibu na mtu kutokea nje au
anaweza ingia ndani... Yaani kupagawa yaani kuwa ( possessed ) na hapo
wachawi watakuwa ili kumlisha Yule pepo aliye ndani yako Matendo 13:6-11
kwahiyo utamwona mtu anatafuna usiku ikionyesha kuwa lile pepo liliko
ndani linalishwa chakula, ili likue na kupata nguvu zaidi.
Mshetani wapo aina mbalimbali
hivyo jambo la muhimu ni kwenda kufunguliwa kanisani katika jina la YESU KRISTO ili uwe huru maana wachawi au majini hawataki ufanikiwe na uende mbinguni ila wanataka utabike na uende jehanamu.hivyo huu ni wakati wa kumpa YESU maisha barikiwa sana
Mshetani wapo aina mbalimbali
Majoka - yaliyo Shushwa pamoja na shetani Kutoka mbinguni.
Majini - wanaofuta mila za kiarabu.
Mizimu - mashetani ya ukoo.
Miungu - mfano sehemu nyingi za Asia nk.
Kwahiyo
muda wachawi wanamtia nguvu Yule shetani, napo mtu yule ataota
anatafuna au analishwa usiku. Watu wa namna hii unakuta tatizo linakua
Kila kukicha kwasababu ya hivyo.
Unaweza hisi ni ndoto tu,
kumbe rohoni wanakutia udhafu zaidi, ili ushindwe kuendelea... Na hapo
tatizo linazidi kuwa kubwa zaidi.
Comments