ROSE MHANDO MALKIA WA NYIMBO ZA INJILI AFRICA MASHARIKI



Unapowazungumzia wasanii wa nyimbo za injli  maarufu zaidi na wanaofanya vizuri zaidi huwezi kuacha kumtaja Rose Mhando ambaye anafanya vizuri sana katika huduma yake ya uimbaji aliyopewa na MUNGU.Malkia huyu wa mziki wa injili Africa mashariki na kati Rose Mhando amezaliwa 1976 katika kijiji cha Dumila, wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, hadi kufika hapo alipo Rose Muhando kabla hajawa mkristo alikuwa Muislam na ni mama wa watoto watatu. Alimpokea Yesu Kristo pale alipokuwa anaumwa na yuko kitandani akiwa na umri wa miaka 9, aliugua kwa muda wa miaka mitatu, na baadae alipona na kubadili dini na kuwa Mkristo.Rose Mhando alianza muziki wa injli katika kwaya iliyoko Dodoma na alikuwa mwalimu wa Kwaya katika kwaya ya Dodoma St. Mary's katika kanisa la Kianglikana la Chimuli:kwa sasa albamu yake ya Utamu wa YESU  inafanya vizuri sana sokoni na ni moja ya albamu bora kabisa za nyimbo za injli kiasi kwamba alipotoa audio watu walikua wanaulizia sana video itatoka lini maana Rose anakubarika sana kwa sababu ya uimbaji wake wa kumaanisha pia sauti na staili nzuri za kucheza kwa utukufu wa MUNGU.Tarehe 31/01/2005, Rose Muhando alizawadiwa tuzo ya Mtunzi mzuri wa nyimbo, Mwimbaji Bora na albamu Bora ya Mwaka. Tuzo hizo zilitolewa katika tamasha Tanzania Gospel Music Awards, 2004  pia Desemba 2005 alihudhuria katika tamasha la Nyimbo za Injili katika kusaidia kuchangia kwa watoto wajane Dar es Salaam.
Februari 2011, Rose Muhando alisaini Mult Album Recording Deal with sony Music. Kusaini huko kulitangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari Dar es Salaam, Tanzania, mwezi Februari na hii in mara ya kwanza kufanyika afrika Mashariki.
Baadhi ya albam za Rose Muhando ni:
1. Mteule uwe macho, 2004
2. Kitimutimu, 2005
3. Jipange sawasawa, 2008 na 4. Utamu wa YESU ambayo hadi sasa inafanya vizuri sana sokoni na kwenye vyombo vya habari kama Redio na Luninga.Hizi ni baadhi tu ya nyimbo ambazo zimewahi kutamba na hadi sana baadhi zinaendelea kutamba; Mteule uwe macho,Jipange sawasawa,Utamu wa YESU,pasipo maono,Nyota ya ajabu,wamama wa leo mbella na Ee MUNGU wangu nitakushukuru.

Comments