KWANINI IDADI KUBWA YA WANAWAKE HUSHIKWA NA MAPEPO KULIKO WANAUME?

Nakusalimu kwa jina la BABA MUNGU, BWANA asifiwe!mi nina swali ambalo kila jumapili huwa napanga kumuuliza mchungji sasa kutokana na muda wa mtumishi kuwa ni finyu sana kwa siku hiyo sipati wasaa huo,sasa mi swali langu ni kuwa hivi kwa nini idadi kubwa ya wanawake hushikwa na mapepo kuliko wanaume?nini kinasababisha wao kuwa na mapepo kuliko wanaume?Asante

MAJIBU YA MAISHA YA USHINDI BLOG
.
Kaka jibu la kwanini  idadi kubwa ya wanawake hushikwa na mapepo kuliko wanaume? ni kwa sababu zifuatazo
1)MAVAZI; Kuna baadhi ya nguo zinaashiria kumtukuza shetani mfano kuonyesha matiti mitaani na kuvaa nusu uchi na hiyo inapepelea watoto wa shetani ambao ni mapepo au majini hudhani kuwa mtu huyo ni mwenzao maana anamtukuza shetani kama wao ni rahisi kuanzisha urafiki naye kwa kumwingia mwilini mwake pia yupo dada mmoja tuliwahi kumwombea kanisani nikiwa zanzibar na mapepo yale yalipokua yanatoka yalisema kwamba yalimwingia kwa sababu alikua amevaa nguo zao hivyo nikajifunza kitu kuwa kuna baadhi ya nguo zina maagano na majini.
2)KWENDA KWA WAGANGA WA KIENYEJI;Hili ni chanzo kikuu sana cha mapepo kuwavaa watu na maana uganga huo huendana na uchawi na uchawi na majini ni watoto wa baba mmoja wa kuzimu. mfano kuna maneno anakutamkia mganga akiwa amepandisha mashetani utashindwa vipi na wewe mteja kupandisha hayo mashetani siku chache zijazo? pia unaambiwa uje na kuku mweusi, kipande cha nywele zako au uje na nguo yako ya ndani.Hayo yote ni kukuunganisha na shetani na kwa hivyo kupatwa na mapepo ni lazima 100% na mambo mengi sana kwenye usangoma lazima tu yakupe zawadi ya mapepo.
3)WIVU NA TAMAA; Wivu nao husabaisha mapepo kwa namna fulani mfano mme wa wake 2 au watatu ni rahisi kwa mmoja wa wanawake hao kwenda kwa waganga na  kwa sababu ya wivu na mgangatakuambia akaleta nguo yake mchanga wa nyayo na hali hiyo ni kumuunganisha na shetani na mapepo ndio wajumbe wake. na kwa sababu huyu anayerogwa kama hajaokoka na hana ulinzi wa MUNGU lazima tu yamkumbe mapepo.Pia kwa kutaka wawe na maisha mazuri wanajikuta wanaenda kuingia mapatano na shetani na hiyo mapepo ndio watumishi waaminifu wa shetani hivyo lazima yatende kazi kwa kuwaingia watu.
4)VIPODOZI NA MAPAMBO; shetani hutaka kuingia katika kila sehemu ya maisha ya mwanadamu iliapate mwanachama hivyo kuna baadhi ya vipodozi hutoka kabisa kuzimu na pia vingine hutengenezwa kabisa na watu wabaya au wafuasi wa ibilisi na humu huwekwa maroho ya kuwapotosha watu na maroho hayo ni mapepo na kumbuka kuwa jini au mapepo ni viumbe wa roho hivyo wanaweza kukaa popote hata kama ni ndani ya jiwe.pia mapambo kama cheni, heleni, bangili,pete,vikuku na shanga ni vyanzo vikuu vya mapepo na wavaaji namba moja wa hivyo ni wanawake hivyo ndio maana wao wanaongoza kuvamiwa na mapepo na kanisani kwenu ni zaidi ya mara 4 inatokea tunamwombea mtu na nguvu ya MUNGU ikiongezeka hata husema kwamba wako kwenye heleni na baada tu ya kumvulisha hereni mtu huyo hupona na pia wengine huchukua muda kupona hadi pale tutakapomwambia avue mapambo hayo na nahakika hata wewe umewahi kuona jambo hilo maana hiyo hutokea sana kwenye maombezi.
5)KUIGA KILA KITU:nalo ni tatizo la kusababisha kuvamiwa na mapepo maana hudhani kabisa mtu huyo ni mwanachama wao. Na ndio maana BIBLIA inatuambia tuige wema na tukatae ubaya wote maana shetani naye hutaka kwenye kila jambo na yeye awepo hivyo wasio na YESU mioyoni mwao kuvamiwa na mapepo ni rahisi sana.
6)UONEVU WA shetani; hili nalo ni jambo kubwa sana la kusabaisha watu kuvamiwa na mapepo, kumbuka wapo wavuga majini au wachawi hutega mitego yao mabarabarani au sehemu zingine kwa lengo lao baya na wanachotega ni majini hayo ambayo huwavaa watu na moja ya watu hao ni wanawake na kumbuka pia kuwa hata shetani alimdanganya Eva maana alijua ingekua ngumu sana kumdanganya Adamu pia BIBLIA inasema kuwa WANAWAKE NI JESHI KUBWA hivyo shetani anajua kwamba akimteka mama ameteka familia nzima au taifa zima huvyo ili kuharibu kazi ya MUNGU huwatumia pia wamama kwa njia hiyo ya mapepo pia kama huna YESU ni rahisi sana kuvamiwa na mapepo na jambo kuu na la muhimu ni KUMPA BWANA YESU MAISHA YETU . na yeye atatuhamisha katika ulimwengu wa roho kutoka mikononi mwa shetani na kutuweka mikononi mwake.na ndio maana yeye peke yako ndiye anayeweza kuondoa mapepo katika miili yetu. na amesema katika Mathayo 11:28 ''Njoni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitawapumzisha''.
MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kwamba hakuna anayeweza kutoa mapepo ila ni BWANA YESU na ndio maana tunapolitamka jina lake mapepo yanasarenda na kuwaachia watu wa MUNGU. Pia katika majibu yangu hapo juu nimezungumzia vipodozi na mapambo, naomba  nieleweke sio kwamba napinga au kukataza kuvaa pete au heleni ila ushauri wangu naomba kila kitu cha namna hiyo ukitakase kwa damu ya YESU ndipo utumie na ndo maana pete za ndoa huombewa kwanza na wachungaji ndipo wahusika hupewa. maana kuna ndoa iliwahi kuwa na mgogoro sababu ya pete kutokuombewa na maana shetani alipanda kwenye pete wajumbe wake mapepo na ilitakiwa watoke kwanza ndipo ndoa itakuwa salama.
Pia tukumbuke kuwa sio kina mama tu ndio wanapatwa na mapepo ila na akina baba pia  ni wengi sana japokua idadi ya wanawake ni kubwa zaidi kwa sababu ya vyanzo hapo juu japokua baadhi ya vyazo huwapata wote mwanamke na mwanaume.
TUMKIMBIE shetani na mapepo yake KWA KUMPA YESU MAISHA YESU ILI TUPATE UZIMA SASA NA HATA MILELE(Yonana 10:10b)

Comments

Unknown said…
Nikweli kabisa Mtumishi,