MAJINA YA MUNGU NA UKUU WAKE.



Ndugu katika BWANA YESU KRISTO nakukaribisha katika somo hili ambalo tunaangalia Majina ya sifa ya MUNGU wetu. na kumbuka kuwa ''ukiujua ukuu wa MUNGU wako wala hutaogopa chochote''  maana kwa kutumia jina la YESU KRISTO lipitalo majina yote na ambalo MUNGU wa kweli YAHWEH au JEHOVAH amejidhihirisha tunaomba chochote na kupokea. MUNGU akubariki sana na msingi wa somo letu uko katika Zaburi 83:18 inayosema  ''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.''
1:  JEHOVAH ADONAI =MUNGU  Mwenye Enzi Yote (Mwanzo 15:2-8 )

2:  JEHOVAH  EL – SHADAI =MUNGU Ututoshalezae MUNGU Mwenyenzi (Mwanzo 17:1)

3: JEHOAH  EL-OHEENU =BWANA MUNGU Wetu (Zaburi 99:5,8,9)

4:  JEHOVAH   EL- GIBBOR= MUNGU Mwenye Nguvu ( Isaya 9:6-9)

 5:  JEHOVAH  EL-OLAM =MUNGU wa Milele (Mwanzo 21:23)

 6:  JEHOVAH  EL-OHEEKA= BWANA MUNGU Wako (Kutoka 20:2,5,7)

7:  JEHOVAH    EL-ELYON= MUNGU Aliye Juu Sana (Mwanzo 14:18)

8:  JEHOVAH    EL-OHIM =Muumbaji wa Milele (Mwanzo 1:1)

 9: JEHOVAH SABAOTH =BWANA wa Majeshi (1 Samweli  1:3)

10: JEHOVAH TSIDKEMU= BWANA ni Haki Yetu (Yeremia 23:6)

11:  JEHOVAH RAPHA= MUNGU Nikuponyae (Mwanzo 15:26)

 12:  JEHOVAH MEKADDISHKEM =BWANA  Niwatakasae (Kutoka 31:13)

13:  JEHOVAH ROHI =BWANA  Mchungaji Wangu( Zaburi 23:1)

 14:  JEHOVAH JIREH= MUNGU Atupaye /Atoaye (Mwanzo 22:14)

 15:  JEHOVAH HOSEENU= BWANA Aliyetuumba (Zaburi 95:6)

 16:  JEHOVAH NISSI= BWANA ni  Bendera(Beramu) yangu (Kutoka 17:15)

17:  JEHOVAH SHALOM =BWANA  ni Amani Yangu (Waamuzi 6:24)

 18: JEHOVAH SHAMMAH= BWANA  Yupo Hapa (Ezekiel 48:35).

MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka yaani hujampokea BWANA YESU awe ni BWANA na MWOKOZI wa maisha yako ndugu hakikisha unampokea leo maana wokovu ni sasa.
ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula 

               Huduma ya Maisha ya ushindi

Comments