Suzana Temba |
Suzana Temba alikuja mkutanoni siku ya sita akiwa amekata tamaa ya
maisha kutokana na matatizo mengi ambayo yalikuwa yanamzonga katika
maisha yake. Suzana ambaye ni mkazi wa Arusha alipata taarifa za mkutano
na kuamua kuja akiamini kuwa Mungu atamponya.
Kuhusu ushuhuda wake, Suzana alikuwa na haya ya kusema, "nilipofika
ibadani nilishangaa kuona kila neno ambalo Mchungaji Gwajima alikuwa
akifundisha lilinihusu mimi" Aliendelea kusema kuwa wakati wa maombezi
ulipofika alisogea mbele na hapo akapokea uponyaji wake kamili.
Suzana Temba akihojiwa na mwandishi wetu mara baada ya maombezi |
Akihojiwa na mwandishi wetu, Suzana alisema kuwa familia yao kwa miaka
mingi ilikuwa katika matatizo ya vifo vya hovyo hovyo ya kwamba misiba
ilikuwa haiishi katika familia yao. Jambo linalotia shaka ni kwamba vifo
vingi ni vya kufanana mfano kifo ambacho baba yake alikufa kinafanana
kabisa na namna ambayo mdogo wake alikufa.
Suzana akiwa na furaha baada ya kufunguliwa na kuwekwa huru kabisa |
Tatizo lingine lililomsumbua na kumfanya akose raha ni maumivu ya
kiunoni ambayo kwa miaka mingi alikuwa anasikia kama moto unawaka
kiunoni mwake. Pamoja na maumivu ya kiuno Suzana aalikuwa anatapika mara
kwa mara bila kuelewa chanzo na kwa maelezo yake hospitali nyingi
hazikuweza kutmtibu moja kwa moja.
Pamoja na hayo yote, Suzana alikuwa anasumbuliwa na mume wa rohoni
maarufu kama jini mahaba; ambaye alikuwa anamsumbua wakati wa usiku hadi
kufikia hali ya kutokuwa na hamu na mumewe kabisa jambo lililopelekea
kuachana na mumewe.
Comments