MASWALI YA MSINGI JUU YA KUNENA KWA LUGHA

Dada Esta akinena kwa  lugha KPC  Kawe


(1) Kunena kwa lugha ni nini? (2) Kunena kwa lugha kuna faida gani (3) Inakuwaje mtu ananena kwa lugha

Ukirejea katika Neno la Mungu, kunena kwa lugha ni ISHARA KWA WALE WAAMINIO, na hili alilisema Bwana Yesu mwenyewe katika Marko 16:17. Na kunena kwa lugha kukaonekana kwa mara ya kwanza siku ya Pentekoste, ambapo wanafunzi wa Yesu wapatao 120 wakiwemo mitume na Mariamu na dnugu zake Yesu, walijazwa na Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, utaona hii habari ukisoma Matendo ya Mitume 1:12-14 na 2:1-4. Pia kukaonekana tena Matendo ya Mitume 10:44-47, ambapo Kornelio na watu wa nyumbani kwake walishukiwa na Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha. Tena Matendo ya Mitume 19:1-7, ambapo wanafunzi waliokuwako Efeso waliwekewa mkono na mtume Paulo na 12 kati yao walijazwa na Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha. Hivyo Bwana aliisema hii kuwa ni Ishara itakayoambatana na wale WANAOMWAMINI, na ikaja kuanza kuonekana pale Roho Mtakatifu anapomshukia huyo mtu aliyemwamini Yesu Kristo. Akina Petro walijua kuwa Kornelio na wenzake wameshukiwa na Roho Mtakatifu baada ya kuwasikia wakisema kwa lugha mpya.

Unenaji wa siku ya Pentekoste ulikuwa wa aina ya lugha za wanadamu, ambapo wale wanafuniz 120 waliojazwa Roho Mtakatifu siku ile waliwezeshwa na Roho Mtakatifu kusema lugha ambazo hawakuwahi kujifunza kabla, lugha za wanadamu wenzao, wale wote walikuwa Wayahudi hivyo lugha yao ilikuwa ni ile ya asili yao, lakini siku ile walisema lugha za mataifa mengine, lugha ambazo walikuwa hawajawahi kujifunza kabisa. Hii ni uwezesho wa Roho Mtakatifu na ni kunena kwa lugha mpya alikokusema Bwana Yesu, ambapo mnenaji ama msemaji anakuwa anasema na watu moja kwa moja na wao wanamsikia kwakuwa anasema kwa lugha yao bila kuhitaji mkalimani ama mtu wa kutafsiri. Kwa mfano mimi ni msukuma , naenda kwa watani wangu wagogo na kuongea lugha ya kigogo tena vizuri tu pasipo kuwa nimejifunza lugha ya kigogo, hiki ndicho kilichotokea siku ya Pentekoste.

Ukija katika 1 Wakorintho 14:, Mtume Paulo ana-address kunena kwa lugha ambako ni kwa aina nyingine na ni tofauti kabisa na kunena kwa lugha kule kulikotokea siku ya pentekoste, ambako wale 120 walinena lugha za wanadamu wenzao na kueleweka moja kwa moja. (sasa haina maana kuna kunena kwa lugha kwa aina 2, la hasha, Bwana Yesu alisema NI ISHARA YA KUNENA KWA LUGHA MPYA, LUGHA AMBAYO SI YAKO, HUJAWAHI KUINENA HAPO KABLA. Kunena kwa lugha anakoongelea mtume Paulo hapa ni kwa lugha ambazo ili kile kinenachwo kiweze kueleweka ni lazima kuwe na tafsiri. Na hapa ndipo mtume anaposema HUYU ANENAYE KWA LUGHA HASEMI NA WATU BALI ANASEMA NA MUNGU MAMBO YA SIRI (1KOR 14:2). Wale 120 siku ya pentekoste walisema lugha za wanadamu ambazo tafsiri haikuhitajika kabisa, BUT kunena kwa lugha mpya kulikokuwa kunaendelea Korintho, mtume alisema kulihitaji TAFSIRI kwa maana hakukuwa kama ule unenaji wa lugha mpya wa Pentekoste.

Kuna karama za Roho Mtakatifu, ziko 9,zimetajwa katika 1 Wakorintho 12:4-11. Katika karama hizi, karama 2 zinagusa ISHARA ya kunena kwa lugha mpya, nazo ni karama ya aina za lugha, na karama ya tafsiri za lugha. Hivyo kunena kwa lugha ni karama, ni gift, ni zawadi itokayo kwa Mungu mwenyewe, na Mungu akitoa kitu anakitoa kwa makusudi, kwa malengo ili kimfaidie yule anayepokea, KWA MANTIKI HIYO KUNENA KWA LUGHA KUNA FAIDA kwake yeye aliyepewa kunena kwa lugha. Mnaweza mkawa waaminio 20 sehemu moja, mkaombewa ujazo wa Roho Mtakatifu na si wote mtajazwa na kunena kwa lugha mpya. Hili ndilo lililotokea Efeso wakati mtume Paulo alipowaombea wale wanafunzi kadhaa pale, ambapo only 12 men walijazwa na Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, Hivyo hii ni karama, ni gift, ni zawadi na mpaji ni Roho Mtakatifu mwenyewe wala si mwanadamu.

Sasa kunena kwa lugha kunakoendelea leo kunapingwa na baadhi ya madhehebu ya kikristo kwa kigezo cha unenaji wa siku ya Pentekoste, na kumekuwa na mabishano mengi juu ya hili. Kumekuwa na kutafsiriwa kwingi kwa andiko la 1 Wakorintho 14:, wale wanaopinga wakijaribu kuonesha uelewa wao juu ya Kunena kwa lugha na Kutafsiri lugha kunakosemwa na mtume Paulo, na kuwaita wanenao kwa lugha kuwa ni watu wanaosukumwa na roho za mashetani kwakuwa ni vurugu na machafuko matupu humo makanisani. Lakini swali la kujiuliza ni hili, hawa wapingao wangewezaje kusema kuwa ni machafuko ikiwa mtume Paulo asingeandika juu ya machafuko na kutokuwa na utaratibu katika kunena huko? Swali jingine la kujiuliza ikiwa mtume Paulo aliwaandikia wale WAAMINIO WA KORINTHO juu ya kuwa na utaratibu na kuepuka alichoita machafuko, hakuwa ameona kuwa walikuwa na utaratibu tayari? na ikiwa walikuwa na utaratibu ilikuwaje akawaona hawana utaratibu hivyo kuamua kuwapa utaratibu? UNAWAPAJE UTARATIBU WATU AMBAO WANA UTARATIBU TAYARI? HIVYO BINAFSI NASHAWASHIKA KU-CONCLUDE KUWA HAWAKUWA NA UTARATIBU NDOMANA AKAWAPA UTARATIBU. Hali iliyokuwako Korintho ndiyo iliyopo leo katika madhehebu mengi ambayo yanakubali kunena kwa lugha, hakuna utaratibu kama ilivyokuwa kwa Wakorintho, kila mtu anataka kunena tena kwa sauti, sasa mwishowe inakuwa ni kama machafuko kama alivyoona mtume Paulo pale Korintho na kuamua kuwapa utaratibu. Kutokuwa na utaratitbu, ama kupuuzia kufuata utaratibu ambao mtume Paulo aliwapa WAAMINIO WA KORINTHO KUMEFANYA KUNENA KWA LUGHA KUPATA UPINZANI USIO NA SABABU KABISA, na wapinzani wanaonekana kushinda kwasababu ni kweli, ikiwa unanena bila kutoa tafsiri ya unenacho mimi sitaelewa ulichosema, lakini ukitafsiri hapo nitakuwa na matunda kwa kile ulichonena, LA HUWEZI KUTAFSIRI BASI NENA UKIWA MWENYEWE KWA KUWA KUNENA KWA LUGHA KUNAKUFAIDIA WEWE ZAIDI. Mtume Paulo hakupinga kunena kwa lugha, tena alisema yeye anamshukuru MUNGU kwakuwa ananena sana kwa lugha, ila alitoa tahadhari ya unenaji wa hadharani pasipo kutafsiri, akasema ni bora aseme maneno matano kwa akili kuliko maneno kumi elfu kwa lugha. Maneno matano kwa akili yataeleweka na wanaomsikia, ila yale kumi elfu ya lugha hayatoeleweka UNLESS atoe tafsiri. Kunena kwa lugha ni gift kutoka kwa Mungu ili kuwasaidia wale waliomwamini Bwana Yesu Kristo katika maisha ya MAOMBI......WAEFESO 6:18,....KUNENA KWA LUGHA NI KUOMBA KATIKA ROHO MTAKATIFU... YUDA 1:20. TENA KUNENA KWA LUGHA KUNAUNGANA NA KUSAIDIWA NA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUOMBA...WARUMI 8:26.

Kuna watu huwa wanauliza hili swali....HIZO LUGHA ZINAZONENWA NI LUGHA GANI?....NA MIMI LEO NINA SWALI MOJA TU; HIVI ILE LUGHA ALIYONENA AMA KUSEMA BWANA YESU PALE MSALABANI NI LUGHA YA WAPI....ELOI ELOI LAMA SABAKTHANI? (Mathayo 27:46-49). Maana tafsiri ilikuja kutolewa na Roho Mtakatifu kwa mtume Mathayo wakati anaandika kitabu cha injili, watu hawakumwelewa alichosema. Tena ninajiuliza swali lingine...yale Maandishi aliyoyaona mfalme Belshaza yalikuwa NI YA LUGHA YA WAPI NA GANI?....MENE, MENE,TEKELI , NA PERESI...(Daniel 5:25-28). Wote tunajua kuwa tafsiri ya hayo maneno, ama hiyo lugha ilitoka kwa Mungu mwenyewe kupitia Daniel. Mifano hii miwili inaonyesha maneno ya hizo lugha yalitoka kwa Mungu mwenyewe na Yeye pekee aliyeweza kutoa tafsiri za maneno hayo. Sasa wanadamu tunamdhibiti Mungu kwa kusema tunazijua LUGHA ZOTE, mbona haya maeneo miwili tulichemka? Sasa leo tunapinga kunena kwa lugha ati kwasababu maneno hayaeleweki. yes hata hawa hawakuyaelewa haya mpaka Mungu mwenyewe alipotoa tafsiri. Na hii ndo faida ya karama ya tafsiri za lugha iwapo itatumika vizuri, karama ya aina za lugha inafanya kazi sambamba na karama ya tafsiri za lugha.

Kunena kwa lugha mpya kuna faida sana katika eneo la MAOMBI, na Shetani anajua umuhimu na nguvu ya maombi. NI rahisi sana kwa Shetani kukutibua ukiwa unaomba kwa akili, lakini Shetani hana ujanja wa kukutibua ukiwa unaomba kwa roho, ndomana mtume Paulo akasema, "Nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba,lakini akili zangu hazina matunda. Imekuwaje basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia....." (1KOR 14:14,15). Mtu akiomba kwa akili ataombea yale anayoyafahamu yeye tu na wakati mwingine hata asiombe vizuri jinsi impasavyo sawasawa na mapenzi ya Mungu kwakuwa hayajui mapenzi ya Mungu juu ya hilo analoliombea. Lakini mtu akiomba kwa roho yaani kwa lugha, ni Roho Mtakatifu anayetoa hiyo lugha, hivyo ni Roho Mtakatifu atakayemsaidia mtu lile la kuombea sawasawa na uhitaji wa huyo mtu, na pia atamsaidia kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu juu ya jambo hilo. (Warumi 8:26,27). Kuomba kwa akili kunachosha mapema na huwa kuna kurudiarudia maneno, mwishowe inakuwa upayukaji tu ili uombe muda mrefu, lakini mtu anapoomba kwa lugha panakuwa na uwezesho wa ajabu wa kudumu katika maombi muda mrefu bila kuchoka, maana si akili inayoomba bali ni roho ya mtu, na roho haijui uchovu wa mwili, ndomana Yesu alisema roho i radhi lakini mwili huu dhaifu, akawauliza yaani mmeshindwa kuomba hata kwa lisaa limoja? Mimi binafsi nina personal testimony, nimeshawahi kuomba for about 5 hours non stop katika lugha, kuomba kwa lisaa limoja ama mawili ni kitu cha kawaida kabisa. Kuomba kwa lugha ni NYENZO muhimu na kubwa katika maombi, ndomana Shetani anawachanganya watu na kuipiga vita mno.

WANAOSEMA WANAMWAMINI BWANA YESU KRISTO WAAMKE.

By Sam Balele

                  

 Bali wote waliompokea(YESU KRISTO) aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; -Yohana 1:12

Comments

Zahoro Kaguo said…
Amen, nimebarikiwa sana na hii article.
Unknown said…
Amen, ahsante sana,, be blessed;!